Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Huyo katumwa, ina maana mchungaji alivyochafuliwa hadharani hakuona, hata alivyolala selo hukuona?,
Let time decide, ni mapema sana kusema gwajima is completely clean, kama anatumia cover ya uchungaji inahitajika juhudi ya ziada na muda ili kumpata na hatia, naimani hata hiyo mamlaka iliyoundwa itakuwa inaendelea kumtazama kwa karibu. Halafu namshauri rais huyu jamaa wamchunguze kwa karibu kuhusu vyanzo vyake vya mapato asituone watanzania mambumbumbu, na kwa mtu mwenye akili timamu ukimtazama mara moja tu utagundua huyu anatumia dini kama cover, am telling you guys huyu gwajima siku zake si nyingi atakuwa exposed, mark my words kuna siku mtaikumbuka hii comment, za mwizi always ni arobaini , watu tuache kuwa misukule tufungue macho sio "tunapopelekwa tu tunakwenda kama ming'ombe"
 
Ni kweli mdogo wake au sio kweli? Tuanzie hapa
Akiwa mdogo wake inatusaidia nini sisi? Kinacho takiwa ni Makonda aoneshe vyeti vyake tu basi! Vinginevyo atumbuliwe hadharani au aondoke akiwa amevaa kandambili.
 
Anatafuta kiki tuu huyu pimbi tuu.kwanza sijui katokea wapi kutafuta ufamous au anataka kutoa nyimbo
 
ALIPSEMA YEYE NI KADA WA CCM ulitegemea angesema nini? yaani chama kinanguvu kuliko Damu? asee Mungu hayupo jamani HII KUFURU YA MWAKA
 
Wameshampa chake huyo.

Nadhani hana hata ubini na Gwajima.

Huwezi kufurahia ndugu yako wa damu kuitwa drug dealer.
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.


vipi kuhusu vyeti
 
Aende kwa gwajima, kweli kwenye familia nyingine huwa kuna machizi!
 
Amipwa ngapi huyu? Kama tunasikia hata wabunge wa chama fulani wanahongwa sembuse huyu?
 
Huyu naye ana matatizo; yaani Gwajima atuhumiwe hadharani kuwa drug-dealer halafu anyamaze tu? How? Very very wrong approach ya kujisafisha na tuhuma za wizi wa vyeti ... Tuhuma za kugushi vyeti zinasafishwa kwa kuweka vyeti hadharani na sio kwa kum-attack Gwajima personally.


Naona ukiwa Kada wa Lumumba unaweka mkopo akili. Mwanasheria tena ndugu haona haya kuja na hoja nyepesi?. Vyeti vya Makonda tuwaachie waliomteua kweli? .
Anyway Kada amepata nafasi ya kusikika!
 
Kihiyo1997, Bashite 2017, baada ya miaka 20 ijayo,........2037.
 
Sisi watz tumechoka na ujinga wenu hoja ya msingi hapa ni.madawa ya kulevya ni siyo ujinga wenu .
Hoja ya msingi zaidi ni kushughulikia wahalifu wote; wanaojihusisha na madawa ya kulevya na wale wanaofanya udanganyifu katika taaluma. Unapokuwa na viongozi wa serikali waliofanya udanganyifu wa kitaaluma, ni rahisi kuvuruga hata mapambano yenyewe dhidi ya madawa ya kulevya!
 
Huyu naye ana matatizo; yaani Gwajima atuhumiwe hadharani kuwa drug-dealer halafu anyamaze tu? How? Very very wrong approach ya kujisafisha na tuhuma za wizi wa vyeti ... Tuhuma za kugushi vyeti zinasafishwa kwa kuweka vyeti hadharani na sio kwa kum-attack Gwajima personally.
Kweli mkuu
 
Hoja ya msingi zaidi ni kushughulikia wahalifu wote; wanaojihusisha na madawa ya kulevya na wale wanaofanya udanganyifu katika taaluma. Unapokuwa na viongozi wa serikali waliofanya udanganyifu wa kitaaluma, ni rahisi kuvuruga hata mapambano yenyewe dhidi ya madawa ya kulevya!
Hapo umenena
 
Ah gwajima bar kazidi sawa katuhumiwa angejisafisha tu kwa kusema sijihisishi but sasa imekuwa vita mpk anataka kumuabisha mwenzake sasa nd mini huyu kwel kiongozi wa dini au michambo.
 
Ameongea vzr....lakini ameonesha pia kapikwa(kaandaliwa)...kama ni kada wa ccm na makonda ni kada unategemea atamsema makonda vibaya? ..lakini zaidi kajitambulisha kwa taaluma yake na kumsifia sifia rais anatafta kiki ya kusaka umaarufu na hata kujitambulisha kuwa yeye ni kada wa ccm anatuma maombi kwa rais ili rais atambue kuna mtu anaitwa mdgo wa gwajima!!!..

Issue ya vyeti na issue ya madawa zote zina uzito sawa juu ya kuharbu mwelekeo wa taifa.Tunajua gwajima alienda police na hata kwa mwanachemia mkuu ili kumpima kama anatumia madawa na kumuachia kulituaminisha kuwa ameonewa kutajwa...wewe unataka akae kimya ili REPUTATION YAKE ISHUKE LAZIMA AJITETEE!!...

MBONA HATA WW UNATAKA KUMLETEA GWAJIMA MAKOSA YA KIIMANI AMBAYO KISHERIA HAYANA LOGIC HUKU UMESEMA UMWANASHERIA...KWANI KAMA ALISEMA ATAMFUFUA BABA WA YATIMA UMEJUAJE KAMA HATAMFUFUA? ..ALISEMA ATAMFUFUA LINI?,MLIPEANA SIKU? ...HATA WEWE UNATAKA KUTUHAMISHA KWENYE MADA....

MAKONDA NAE KAMA TU ALIVYOSHUTUMIWA NAE AENDE POLICE AKACHUNGUZWE PIA VITA YA VYETI FEKI NI MOJA YA AJENDA MAHUSUSU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO...KAM IIIVYO YA MADAWA YA KULEVYA...MSITAKE KUIFANYA N DOGO ATI KWA SABABU MAKONDA AMEWAHITI WAPINZANI TU...
 
Nabii wa kweli tutamtambua kwa matendo yake
IMEANDIKWA
" Ndiyo,’ yenu iwe ‘Ndiyo’ na
‘Hapana’, yenu iwe ‘Hapana.’ Lo lote zaidi ya hili
latoka kwa yule mwovu.’’
" akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la
pili pia" (MATHAYO 5:31-39)

Kwa kutumia kifungu hiki tu unatambua yupi mtumishi wa Mungu kwa Wakristo nawakumbusha hili
 
Back
Top Bottom