GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Binafsi pamoja na kuwa ni Mpinzani wako ( nikiwa mwana Simba SC ) ila nilipenda na nimependa mno ambavyo umeleta Mabadiliko makubwa katika hiyo Idara ya Usemaji wa Yanga SC. Najua kuwa kuna muda huwa Unanikera / Unatukera wana Simba SC kwa Madongo yako ila kwakuwa Sisi ni Wanamichezo na Watani wa Jadi huwa sichukii sana sana huwa nacheka na kufurahi tu kwani ndiyo Simba na Yanga zilivyo.
GENTAMYCINE nilijua tu fika na hata hapa JamiiForums nilishaandika mno kuwa uwepo wa Haji Manara hapo ni HATARI sana Kwako kutokana na kumjua mno alivyo na Michezo yake ya kupiga Majungu, Kufitinisha na kupenda mno Ushirikina. Hivyo wala Sikushangaa kuona ndani ya Wiki moja tu tokea Kifungo chake Kumalizika na Kurejea ndani ya Yanga SC kukaibuka Mizozo huku Mambo ya Kiushirikina yakiibuka.
Mdogo wangu Ali Kamwe hiki Kilio kikubwa cha wana Yanga SC Kwako kwa kukutaka ubatilishe Uamuzi wako wa Kujiuzuru na Kuulazimisha Uongozi wa Yanga SC ufanye juu chini Kukurejesha nakuomba ujue kuwa ni Deni Kubwa sana la Kiutendaji ulilonalo Kwao. Na njia rahisi ya Wewe kuwashukuru ni kwa kufanya Kazi kwa bidii, kuwa Mbunifu kama ulivyokuwa katika Idara na kubwa zaidi ni Kumuepuka sana Haji Manara.
Hata hivyo kuwa Makini hasa na Maisha yako kwani Adui yako uliyenaye yuko nawe na ni mzuri wa Mikakati ovu. Wewe na Ahmed Ally mmeleta ladha yenu ya Kipekee katika Idara zenu na Mnatuchangamsha mno Wanamichezo. Huu siyo wakati wa Wakongwe ambao hawana tena jipya katika Usemaji kuendelea kuwepo ndani ya Vilabu vikongwe na wakitaka Ajira basi wawe Walinzi wa Milangoni tu.