Mdogo wangu kamkataa mke mtarajiwa: Baada ya kujua mama yake alizaa na shemeji yake. Dogo anaona kama anaoa laana

Mdogo wangu kamkataa mke mtarajiwa: Baada ya kujua mama yake alizaa na shemeji yake. Dogo anaona kama anaoa laana

Upuuzi yan mungu mwenyewe hatoi hukumu ya namna hiyo. Kosa la mtu huyu unaenda kumuhukumu yule ujinga kabisa. Minadhani huyo ndugu yako hakua muoaji toka apo ila akitafuta sababu ya kumtua bint wa watu tuu
 
Hamkuwa waoaji nyie mngekuwa waoaji msingeanza kupekenyua hivo ukoo wa huyo dada...unaenda kuoa wewe unaanza kupambana kuwajua watoto wa shangazi au shangazi alizaaje haingii akilini
Hii ni chai ukisoma maelezo utaelewa.[emoji706]
 
Habari wana FF.

Nina ndogo wangu wa kiume hapa ana 27 years.
Sasa alikuwa na rafiki wa kike yani yeye aliona huyu ndo mtarajiwa. Mwaka jana mwanzoni dogo aliitaji kufahamiana sana hasa kifamilia na mpenzi wake.

Sasa baadae akaja kujua Baba yake haishi na mama yake. Yeye alisema kuwa kwa Baba yake yeye ni mtoto wa 4 kutoka mwisho it's means wapo 5 kwa baba, ila kwa mama yake ni wa 3. Inamaana kwa mama yake wapo wengine 2 juu yake ambao ni wakiume.
Dogo akaona fresh tuu haina shida.

Sasa mwanzoni mwa mwaka huu. Dogo alieleza kuwa anahitaji kuoa wazazi wetu wakamshauri jitahidi kujua familia yake huyo dada vizuri.
Ujue kwa Baba yake wapo wangapi yani Baba mkubwa, baba mdogo au mashangazi.
Na maisha wanayoishi na ni watu wa aina gani.
Na hata upande wa mama.
Kwa sababu kuna wengine wanakuwa na matatizo flani ya kurithi jitahidi ujue. Mdogo wangu akasema sawa.

Sasa katika kumuuliza zaidi dada yule na kufuatilia akaja kujua Baba yake ni mkubwa, its means ana Baba mdogo wake.
Dogo bhana akataka kumjua Babamdogo wake binti, binti akamwambia kuwa yupo hapa hapa mjini.
Dogo akamuuliza anaishi wapi, si anafamilia kabisa.
Binti akasema kuwa ndio.

Sasa mdogo wangu akataka kujua kama anawatoto maana home walimwambia ni vizuri ukawajua hata hao watoto wa mashangazi na baba mkubwa au mdogo.

Yule binti akamwambia ndio baba mdogo wake anao 2 wa kiume. Dogo akasema sawa, ila akamwambia nitafurahi nikiwajua watoto wake na wewe ndugu zako upande wa Baba yako, binti yule akasema sawa.

Mdogo wangu akataka kumjua kwa nini mama yake hayupo kwenye ndoa, maana tunaamini taswira ya mama ndo ya binti mwenyewe. Binti akawa kama anasita hivi. Akamwambia mbona kimya hivyo si useme tuu. Akamwambia kuwa walitofautiana tu mengine mimi sijajua.

Ila baadae dogo akamwambia kuwa inamaana mama yako alizaa na mwanaume zaidi ya mmoja maana uliniambia kwa mama mpo 3 na wewe ni wa mwisho. Akamwambia ndio. Ndogo akasema kwa Baba yako ni wa 4 kati ya 5, akashituka akaona mzee wake alichepuka hapa.

Dogo baada ya kufikilia sana akaanza kuisi inawezekana ndoa ilivunjika baada ya mama yake kuzaa nje.

Dogo akauliza majina ya kaka zake waliozaliwa pamoja na mama yake ili awajue. Alivyosikia majina akaona majina ya mwisho yanafanana kasoro majina ya kati tuu.

Akamuuliza mbona majina yenu ya mwisho yanafanana , binti akamjibu sisi ni ndugu. Ila binti alionyesha kukosa ujasiri kabisa. Akamuuliza tena kwani Baba yao hawa kaka zako, mzee wao aliwakataa mpaka mbadilishe majina, akasema hapana.

Dogo hakuelewa akaja kuniuliza mimi, mimi nikamwambia hivi ngoja tutafute majina ya Baba yake dada huyo, na majina ya Baba yake mdogo (majina la Baba wa kaka zake). Tukaja kuona kuwa majina yao ya kati na mwisho yapo sawa.
Mimi nikamwambia kuwa basi kama ni kweli yapo hivyo. Basi mama yake alizaa na shemeji na ndoa ikavunjika.

Mimi nikamwambia fuatilia kwa kumuuliza dada huyo ili tupate umbea ilikuwaje.
Akaja kujua kuwa Baba yake mdogo alisafiri miaka ya 90 huko akaenda nje kusoma alikaa kama 2 years hivi. Alivyorudi alimkuta mkewe anaujauzito wa miezi 8 ambaye ni huyo dada. Ila yule Baba akasema tuu sawa. Ila akataka kumjua ujauzito wa nani?
Katika kumuuliza mama bhana akasema ( japo mimi naamini alifanya kosa mama kumtaja shemeji) , kwa nzia siku ile ndoa iliisha hapo. Nasikia alimwambia tuu bola ungezaa na mwingine, waligombana na kaka yake na hata ukaribu na kaka yake ulikufa mpaka leo.

Dogo akaamua kupiga chini akaona hii ni laana yani, mama yako alizaa na shemeji yake.
Nikaona daaa,
Alisimulia home ila dogo.
Story yako fupi saana ila umejaribu kurefusha mwisho hata wewe hujaielewa

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Nyoka hazai mjusi,huyo mke mtarajiwa nae inawezekana akawa amerithi tabia za Mama yake,

Dogo kafanya vizuri kuipiga chini hiyo ndoa,atafute familia inayojielewa,

Yangu ni hayo tu kwaleo.
 
Huu Uzi Ni mgumu Sana kuelewa ila mdogo wako yupo sawa kbsa kuachana na huyo dada.
 
Ukimchunguza sana bata

Ingekuwa hivi watu wasingeolewa woii huyo ndugu yako alikuwa sio muoaji na alikuwa hampendi dada wa watu, alikuwa anatafuta sababu hivi unajua ukimpenda mtu hata usikie nini
 
mchagua jembe si mkulima

Ukimchunguza sana bata hutomla

Huyo dogo yeye ana uhakika kwenye familia yao wako sawasawa?

Binti hana dhambi, wenye dhambi ni walioitenda!
 
Ukimchunguza sana bata

Ingekuwa hivi watu wasingeolewa woii huyo ndugu yako alikuwa sio muoaji na alikuwa hampendi dada wa watu, alikuwa anatafuta sababu hivi unajua ukimpenda mtu hata usikie nini
Nakuusia, kwenye kuoa, upande wa mwanaume sahau kuhusu mambo ya kupenda kabisaaa yaani kabisa. Hicho tu, watu wanapenda mdada anamweka mchepuko ila kuoa anaoa mwingine, hapo wadada mjitafakari.
 
Nakuusia, kwenye kuoa, upande wa mwanaume sahau kuhusu mambo ya kupenda kabisaaa yaani kabisa. Hicho tu, watu wanapenda mdada anamweka mchepuko ila kuoa anaoa mwingine, hapo wadada mjitafakari.
[emoji1787][emoji1787] Huyo unayemuusia sasa ni mzee nishavuka huko mkuu wausie mabinti sio kibibi gagula mimi
 
VIjana wa siku hizi wanatafuta sbb ndoa ihairishwe
 
Back
Top Bottom