Mdogo wangu wa kike anaugua sana kichwa, na watoto wake wapo hoi. Mnisaidie tafadhali

Mdogo wangu wa kike anaugua sana kichwa, na watoto wake wapo hoi. Mnisaidie tafadhali

Jocasta

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
475
Reaction score
600
Mdogo wangu wakike ameolewa kama miaka 10 iliyopita, anasumbuliwa sana na maumivu makali ya kichwa kisichosikia dawa, nimempeleka kamanga hadi bugando kafanyiwa MRI Lakini haijabaini shida yoyote.

Mtoto wake wa kike kafariki juzi baadae ya kuwa chini Kwa muda Sasa, watoto karibia woote wanaugua, mnisaidie nifanyeje.
 
Shida imeshaleta matatizo hapo.. ..!
angalia na kule kwengine.. ... ..
 
Mdogo wangu wakike ameolewa kama miaka 10 iliyopita, anasumbuliwa sana na maumivu makali ya kichwa kisichosikia dawa, nimempeleka kamanga hadi bugando kafanyiwa MRI Lakini haijabaini shida yoyote.

Mtoto wake wa kike kafariki juzi baadae ya kuwa chini Kwa muda Sasa, watoto karibia woote wanaugua, mnisaidie nifanyeje.
Hayo mambo si ya hospital..MRI ndio kipimo cha mwisho..hicho kikitoa majibu negative usihangaike tena na hospital
 
Jiongezeni na nyie huo sio ugonjwa wa hospitalini hapo ni maombi au tiba asili
 
Jiongeze we jamaa atakua analala na madudu humo ndani. Mnashindia Government wakati unaona kabisaaaa huyo karogwa!?
 
Kuna mtumishi mmoja anaombea kwenye simu na unapona kabisa, amemuombea dadangu yupo mtwara kapona kabisa, alikuwa amelala kitandani miaka 3, tulikuwa tunasubiri Mungu afanye yake ila alipoombewa kafunguliwa kabisa, ni mzima anaombea bure kabisa huo ndo wito wake! Ukihitaji namba zake njoo pm nikutumie! Yesu yupo anafungua wapendwa!
 
Mtumishi wa Mungu anaombea bure,kwanini PM!
 
Hayo mambo si ya hospital..MRI ndio kipimo cha mwisho..hicho kikitoa majibu negative usihangaike tena na hospital

Poleni, Mola awaponye upesi.
Umemuelewa

Mojawapo..
nashauri muende kwenye maombi kazana. Au piga simu ya maombi world prayers, KKKT Kijitonyama, Dar. wapo 24 hrs anzia hapo hata muda huu kama bado hawaja anza maombi. .
 
Uko wapi mkuu,? hili jambo lilimkumba mtoto wangu wa kiume wa 7yr,kichwa kilikuwa kinamuuma, madaktari wakimpima hawaoni ugonjwa,nilifika Hindu Mandal na Bugando,nikaamua kumrudisha home,mbaya zaidi tena ikawa akila Chochote anatapika.

Ilibidi niende kwa tiba mbadala,ndani ya siku Moja mtoto anakula na kumywa,na sasa anakimbia tu.

Wakati mwingine tuamini uwepo wa nguvu za giza

By the way pole sana
 
Mtafute Sheikh maalum sio kila Sheikh, Jini hilo linamtesa
 
Labda wamekunywa sumu au nyumba yao ina vimelea vinavyowadhuru kama fangasi(kuvu). Wahame kwa muda.
Niliangalia episode moja ya Forensic Files kuhusu hii kitu kule US. Kuna fungi wakiingia kwenye nyumba solution ni kuhama tu; na nyumba wakati mwingine inabidi ibomolewe. Familia nzima walikuwa wanaumwa vichwa, degedege, vifua na neurological disorders kibao. Mtoto wao wa pekee alifariki hatimaye. Katika kufanya uchunguzi wa kifo hicho ndiyo ikaja kugundulika kuwa nyumba ilikuwa na kuvu hatari sana.

Nyumba walikuwa wamepanga na walienda mahakamani wakalipwa dola zaidi ya milioni 50. Lead exposure pia inaweza kuleta matatizo hayo.

Hebu wajaribu kuondoka wanapokaa kwa mwezi hivi ili waone kama hawatapata nafuu. Shida inaweza kuwa ni kitu cha kawaida tu (spores, lead, heavy metals, plastics, allergy triggers) kimo humo ndani ndiyo kinawapa hilo tatizo. Mungu na Awasaidie 🙏🏿
 
Mdogo wangu wakike ameolewa kama miaka 10 iliyopita, anasumbuliwa sana na maumivu makali ya kichwa kisichosikia dawa, nimempeleka kamanga hadi bugando kafanyiwa MRI Lakini haijabaini shida yoyote.

Mtoto wake wa kike kafariki juzi baadae ya kuwa chini Kwa muda Sasa, watoto karibia woote wanaugua, mnisaidie nifanyeje.
Aende kuombewa....
 
Back
Top Bottom