Iyerdoi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2012
- 2,717
- 3,895
Ni kumuasa tu akafocus na kilichompeleka, awe na mpenzi mmoja mwaminifu na maisha yaendelee, hayo mengine hayazuiliki kamwe.Unaweza kuwa sahihi kwa baadhi ya situation. Kwa kesi ya mleta mada ni ngumu sana kulithibiti hilo linalomtia hofu. Labda amfungie ndani asiende chuo wala asichangamane na jamii kabisa au ampe ushauri wa namna ya kwenda kuishi huko chuoni. Hilo la pili ni gumu kwani litafanikiwa kutokana na misingi ya malezi na makuzi ya mtoto, na si kwa nasaha na mikwara kibao. Ni kumuasa tu akafocus na kilichompeleka, awe na mpenzi mmoja mwaminifu na maisha yaendelee, hayo mengine hayazuiliki kamwe.
Sentensi hii nimeipenda ila hapo kwenye awe na mpenzi.... inakuwa kama umemruhusu vile. Hapo ni bora umwambie au umtanabahishe matokeo ya kujihusisha na mapenzi ilhali kusudi na lengo la kilichompeleka hapo chuoni ni kusoma na kupata elimu.
Ni kweli, ukweli mtupu kwamaba hayo mengine hayazuiliki kamwe na hakuna hata mmoja aliye wahi kufaulu huo mtihani.