Mdogo wangu wa kike ndiyo kamaliza Form 6, safari ya chuo imekaribia. Nawaza ataukwepa vipi "Ukware" wa vyuoni?

Swali la kujiuliza;
- Wewe ulishirikije kwenye huo mtindo wa chuo,.. Positively/ Negatively ?
Jibu lake kwa kiwango kikubwa litakupa mwanga juu ya maisha ya mdogo wako yatakavyokuwa pia.

Jambo la kufamu ni kwamba tabia ya mtu kwa asilimia kubwa inachangiwa na malezi.
 
Kupigwa miti hakukwepeki muache akapate haki yake
OK; Nadhani muda ukija kujaliwa kuwa na binti wa kumzaa ww mwenyewe au mdogo wako wa tumbo moja na akafikia hatua hiyo ya kujiunga chuo, ndipo utaweza kuelewa kwa nini kuna hali ya wasiwasi kama aliyo nayo huyu mwenzetu mwenye mdogo wake (binti) anayekwenda chuo. Ni rahisi sana kulichunga kundi la ng'ombe 100+, kuliko kumchunga mtu/binadamu mmoja tu mwenye akili timamu. Unaweza kuchizika aisee.
 
Nanukuu:
"Jambo la kufamu ni kwamba tabia ya mtu kwa asilimia kubwa inachangiwa na malezi."
Ila Jambo la kufahamu pia ni kwamba, hakuna hata mzazi mmoja atakaye mlea mwanae (Ke) akawe ni cha wote popote pale. Mazingira yana mchango wake muhimu katika kujenga Tabia ya mtu. Mazingira ya chuo yanaweza kumlazimisha mtu akajivika Tabia ambayo hukudhania anaweza kuwa nayo.
 
Acha kuwaza vitu vya ajabu ambavyo havikwepeki kwenye maisha ya mwanadamu. Timiza wajibu wako

1. Mkalishe chini, mpe elimu ya kutosha kuhusu maisha ya huko, atakacho kutana nacho, madhara yake na faida zake kama itakulazimu kuzieleza.

2. Jitahidi sana mdogo wako apate kila kitu kwa wakati hata kama sio kwa ukubwa lakini apate mahitaji yake ya mhimu tena kwa wakati (hii ndiyo sababu kubwa inayo-wapeleka huko kwenye hayo mambo)

3. Awe na usimamizi na ufuatiliaji wa maendeleo yake ya chuoni (ila usimchunge, yaani USITHUBUTU kufanya hili kosa kwa sababu atahitaji kukuonyesha who is in charge)

The rest muombee
 
Jukumu lako ni kumpa nasaha za hali halisi za huko na namna gani aishi ili kuweza kufukuzia ndoto zake.

Uamuzi wa kufuata ni wake mwenyewe.

Hadi hapo hautakuwa na lawama tena juu yake na atakuwa hakudai chochote
 
Hakuna namna ni ku play your part mengine huna uwezo nayo
 
Nipe namba yake niwe mentor wake na hakika hutojutia kunikabidhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…