LGE2024 Mdude amburuza kortini RPC Songwe, Mwabukusi kumuwakilisha katika kesi hiyo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwanaharakati na Rais wa TLS Boniface Mwabukusi amefungua shauri chini ya hati ya dharura katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Mbeya, akipinga kushikiliwa kwa Mdude Nyagali na Jeshi la Polisi.

Pia, Soma: Makosa Matatu ya Mdude Nyagali: Kujeruhi, Matusi na Kuvuruga Uchaguzi, Wakili Boniface Mwabukusi kumtetea

Shauri hilo, linalohusu madai ya kushikiliwa bila msingi wa kisheria, linatarajiwa kusikilizwa kesho, Novemba 26, 2024. Mwabukusi ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha haki ya Nyagali inalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ingekua uchanguzi hii fomu inge-enguliwa mapema sana
 
Inasikitisha sana SIRIKALI kupambana na raia ambao wanatoa maoni ambayo yanasaidia TAIFA ila wanaonekana MWIBA.....wawaige wamarekani kwenye uhuru wa maoni maana mifano yao wanapenda kuitumia marekani kwa kusema "mbona hata marekani wanadaiwa".
 
Huyu Mdude huwa hatoi maoni bali anatukana. Mbona hujashikwa wewe??
 
Mwanaharakati na Rais wa TLS Boniface Mwabukusi amefungua shauri chini ya hati ya dharura katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Mbeya, akipinga kushikiliwa kwa Mdude Nyagali na Jeshi la Polisi.

Pia, Soma: Makosa Matatu ya Mdude Nyagali: Kujeruhi, Matusi na Kuvuruga Uchaguzi, Wakili Boniface Mwabukusi kumtetea

Shauri hilo, linalohusu madai ya kushikiliwa bila msingi wa kisheria, linatarajiwa kusikilizwa kesho, Novemba 26, 2024. Mwabukusi ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha haki ya Nyagali inalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
You are REQUIRED, inakuaje barua rasmi tena ya mahakama kama hiyo inakua na typing error
 
Back
Top Bottom