Mdude CHADEMA: Tunaiandikia FIFA barua ili Simba ifungiwe kwa kujihusisha na siasa

Mdude CHADEMA: Tunaiandikia FIFA barua ili Simba ifungiwe kwa kujihusisha na siasa

Msemaji wa Simba ndo Simba! Chadema komaeni ili ifungiwe hata wiki 6.... Itakuwa fundisho Kwa wengi sana wanaochangsnya siasa na majukumu yao.
 
Hapo ndio unajua Chadema ilivyojaza vilaza

Yaan dah

Hawa ndio vijana wa kupambana na CCM kwenye field ya ushawishi?

Kumaa Mae
 
Wakufungiwa ni Ahmed Ally sio Simba wala Tff, semaji amenikera sana na huo upumbavu aliofanya
 
Wafungiwe hao wana changanya mpira na siasa mwiko kabiisa
 
Kwa namna siasa za nchi hii zilivyo hasa za hawa CCM, ni vizuri sana viongozi wa hizi timu za mpira kuchukua tahadhari mapema kwasababu hawashindwi kushinikiza ilimradi mambo yao yaende

Inaweza isiwe leo, inaweza isiwe katika hili la UVCCM na Ahmed Ally lakini mwaka huu na mwakani ambayo ni miaka ya uchaguzi tahadhari ni muhimu sana maana kuna viumbe wao akili walishatumbukiza shimoni wanachojua nchi hii ni yao peke yao na wanaweza kufanya lolote, popote na wakati wowote bila kizuizi

Haiingii akilini kuwa wasanii wote wale wa tasnia tofauti tofauti, kina semaji la shirikisho na wengine wamehudhuria ule udubwana kwa kupenda kwao. External force inapotumika mahali haijifichi
 
Afungiwe Ahmed Ally sio Simba. Mdude acha bangi. Mwamedi Ally acha wazimu
Wote mnaoshabikia hii mipira ya Yanga na Simba ni wendawazimu. Hizi timu zinatumiwa na magabachori kupumbaza watanzania ili wao na wanasiasa waendelee kupiga mali ya nchi.
 
1720329071036.png
... pale Mdudu anapoamua kiji'dudufy' jumla!
1720330700798.png
 
Chadema wanajifanya wajuaji sana malimbukeni na Matapeli mimi naomba waendelee na mtaji wao wa kuwahamasisha vijana twitter wakamatwe, wajiteke wenyewe kwa wenyewe ili wapate kuchangishana michango 😂😂😂 ndio wanachokijua kwa sasa
 
Mdude ashakuwa mwenda wazimu awahi mirembe!
Wewe ndo mwendananihii mpira na siasa wapi na wapi? Tuache, ushabiki wa timu unachanganya watu wengi sana kama Misikiti na Makanisa. Kwahiyo naye Sheikh mkuu aseme pigia chama fulani? Au Kardinali? Acheni hizo. Kama CCM mmeona hamueleweki ndo muda umefika msiforce. Mmeforce kumpeleka Makonda Arusha eti aue Chadema, mmeforce kuweka nafasi isiyorasmi ya naibu waziri mkuu eti watu wa Kanda ya Ziwa wamuelewe, mmeforce kuiita awamu hii ni ya 6, mnaforce kugawa Pikipiki karibu kila mkoa mmeforce kubandika mabango kila mji na kila barabara kuu. Kaz mnayo mpaka 2025 mwezi wa kumi itajulikana tu. Afe kipa afe beki!!!! Mngekuwa mmelitendea taifa hili mazuri mabango ya nn na kazi zingekuwa zinajieleza. Mnaandika eti Mikopo Kwa wanafunzi wa Chuo kikuu imeongezeka mm mwananchi wa kawaida inanisaidia nn! Nitaenda vyuoni kuuliza pesa zilizopelekwa? Msitake tuongee . Acheni siasa na Michezo. Wananchi wa 2024 siyo sawa na 1947
 
Un
Chadema wanajifanya wajuaji sana malimbukeni na Matapeli mimi naomba waendelee na mtaji wao wa kuwahamasisha vijana twitter wakamatwe, wajiteke wenyewe kwa wenyewe ili wapate kuchangishana michango 😂😂😂 ndio wanachokijua kwa sasa
Rejea kauli ya mwenyekiti vijana Ngara CCM mpaka leo kafanya nn?
 
Ila upinzani wa hii nchi, bora tuandamane kama Kenya bila kuwahusisha hawa wachumia tumbo.

Sasa hapo Ahmed ana tatizo gani, hapo kaenda kama Ahmed na sio msemaji wa simba.
 
Sasa ni Simba ama Ahmed ndio kajihusisha na siasa?!
Yeye ni muajiriwa tu, ana maisha binafsi.

Ingelikuwa Simba kwenye mechi wameingia na mabango kuhamasisha siasa hapo kuna mashiko.

Ndiyo hapo sasa. Achague siasa au mpira.....!!

Anyway, CCM wasichekelee sana kuingiza siasa za Simba na Yanga kwenye mpira. Simba na Yanga hawajawahi kuwa upande mmoja ... ndiyo maana hizo team zikicheza mashindano ya kimataifa utakuta upande moja unashangilia wageni. Sasa kama siasa zitaingia kwenye mpira ni Kama Simba watachagua CCM basi Yanga lazima wawe upande wa pili .... that is simple.
 
Back
Top Bottom