Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Mdude ni MWONGO na anajuwa kuwa kaandika uwongo. Hiyo statement haimaninishi Spika wa Bunge ambaye ni mbunge wa Mbeya (M). Angeandika Tulia Ackson basi ndiyo angechukuliwa hatua. Huyo Tulia aliyemuandika yeye anaweza kuwa Tulia Mdude au Tulia Mbowe au Tulia Lissu.Kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa X, anadai Tulia anapanga mipango ya kumuua. Huyu Mdude anapenda ku trend kwa mambo ya kizushi.
---
Kupitia ukurasa wake wa Twitter (X) Mdude Nyagali anaandika haya:
Nimepata taarifa za siri kutoka kwa msamalia mwema kwamba Tulia amefadhili kikundi cha GreenGuard kutaka kuniua. Kwamba Green Guard hao wameanza kuuliza ninakoishi na nikakoshinda ili iwe rahisi kufanya unyama juu yangu. Na mimi nimeanza kupeleleza majina ya green Guard hao wote.
Pili ni kwamba Tulia anapaswa kujua kuwa Mdude analindwa na damu ya Yesu, Mungu Mwenyezi yupo pamoja na Mdude ndio maana kila hila zikipangwa juu ya Mdude zinakwama. Mwisho kabisa ni kwamba hizo levo za kuvamiwa na Green Guard + polisi zilishazivuka niko mbele sana.
Hata ukimpeleka mahakamani atakushinda maana utaulizwa wapi kasema Tulia Ackson.
Anyway muacheni huyu mwehu, ameathirika kimahabusu mahabusu