Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
Wahenga walisema “Muungwana akivuliwa nguo huchutama” na “asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu.“
Tarehe 01 Julai 2021 Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA) akiwa katika kongamano la kudai katiba mpya alitoa matamshi yasiyokuwa na staha yenye kuleta ukakasi na kichefuchefu kwa kila anayeyasikia na kuyasoma ambayo yaliyomlenga moja kwa moja Rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM. Naomba kumnukuu Mdude; “mwambieni huyo mama yenu wembe niliotumia kumnyoa mtangulizi wake nitamnyolea yeye akileta jeuri” mwisho wa nukuu.
Ni aibu kwa kijana wa kitanzania na Chama anachotoka kutokuwa na adabu mbele ya Rais wa nchi na ambaye pia ni mama katika jamii. Pongezi kwa wachangiaji wote katika mitandao ya kijamii hapa jukwaani (Jamii Forums) na kwingineko hasa wale wa kutoka upinzani na CHADEMA walioneshwa kuchukizwa na kutokulizishwa na lugha aliyoitumika Mdude; Tunasimama kwa pamoja na kumueleza Mdude kuwa Rais kama mama anastahili heshima na anatakiwa kukosolewa kwa adabu. Mdude anatakiwa kukemewa kwa nguvu na watu wa kada na vyama vyote na wale wasio na vyama nchini. Sambamba na hilo tumkumbushe kijana huyu kuwa dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Ni wakati sahihi wa Mdude kujitokeza mbele ya umma na kuomba radhi kutokana na matamshi yake yaliyoleta hisia mseto katika jamii kama ambavyo ameaswa/ameonywa na wanajamii. Rais wa JMT alisema tumkosee yeye na Serikali kwa lugha yenye heshima na tutoe ushauri nini kifanyike kwa sababu kila mtu ana doa.
Mdude popote ulipo kumbuka kuwa hauwezi kuacha alama kama unavyojimbanua kwa siasa za namna hii kwa sababu ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno; wakati ukifika utatupa majibu sahihi.
Siasa inahitaji kujibu hoja kwa hoja bora zaidi na sio kuleta vitisho katika jamii.