Mechi iliyochezwa muda mrefu zaidi duniani

Mechi iliyochezwa muda mrefu zaidi duniani

We jamaa akili huna kabisa umefanya nimeonekana chizi hapa nnapopata lunch[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shilingi ikafanyaje? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahahaha jamaa hata kama anajifunza kuongopa aisee sio kwa namna hii kwamba mpaka watu wakalala uwanjani.
dah, yaani nilivoisoma hii jana nilicheka kinyama, mbaya zaidi ilikua night kali,

bado nawaza huyu jamaa aliwaza nini kutulisha matango pori hivi
 
Wengi hamuijui hii,

MECHI ILIYOPIGWA MUDA MREFU ZAIDI DUNIANI,


Hii ilikua mwaka 1942 fainali ya AMERICAN CUP ENZI HIZO, kati ya ARGENTINA na MAREKANI

Kipute kilipigwa dk 90 wanaume wakatoka mbili kwa mbili, zikawekwa 30 wanaume wakamaliza hivyo hivyo.

Refa KOLLAR DE QUISOR akasema twendeni kwenye matuta, kwenye 5 za kwanza wakatoka 4 kwa 4 akawaambia wapige zingine wakatoka 5 kwa 5, basi wakapigiana penalty karibu mia wakatoa sare.

Kwa kuwa walikua wamechoka akawaomba wapumzike wakaenda mapumzko kurudi mambo yakaenda mpaka penalty mia zingine ikawa draw, zikapigwa hamsini zingne ikawa sare na watu njaa zinauma sana, basi bwana KOILLAR akawaambia wakapate msosi kwenye mgawaha wa karibu.

Waliporudi ikapigwa penalt mpaka karibu na kesho na watu wakaambiwa laleni uwanjani, asubuhi zikapigwa tena kitu sare na ikawa hivo kwa siku 4 ndipo ikarushwa shilingi bado ikatua imesimama zaid ya mara kumi na 9, refa akawaomba wakate kombe nusu kwa nusu

By Deadbody

Pamoja na kuwa ni uongo ila necheka sana.
 
Umefunga mwaka.......Hakuna atakugusa mkuu.....Nimecheka hadi watu wamenishangaaaa kudadeki we noma
 
asubuhi zikapigwa tena kitu sare na ikawa hivo kwa siku 4 ndipo ikarushwa shilingi bado ikatua imesimama zaid ya mara kumi na 9, refa
upload_2017-5-12_20-9-33.png
 
Back
Top Bottom