YANGA VS SIMBA
GOLI LA MORISOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOON HADI LEO NATAMBA NALO
MIKIA KIMYAAAAAAAAAAAAAAAAA
Hii mechi kwangu mm, ndiyo iliyobeba mechi zote 10 bora na kali.
1- dk 1- 12 hapa Mikia walistahili kupigwa goli 3 safi.
2- Tshitshimbi , Balama, Feisal hawa waliwakamata, Mkude, Chama, Kahata hapa kielelezo angalia rafu za kiwango cha KINESI toka kwa wachezaji wa mikia
3- dk ya 44 goli Mujarabu, mpaka kipa wa Simba Aishi Manula analithibitisha hilo.
4- ushangiliaji wa goli lile na vurugu za kurusha chupa za maji, naam ni burudani.
5-ulinganifu wa Jersey, hapa kuna tofauti kubwa hongera GSM
6- Metacha Mnata huyu alijuwa vyema kufanya kazi yake , hainitoki kichwani. Nadhani Mikia watamchukua kama BENO.
7-EEEEH BABA HARUNA NIYONZIMA kisu cha buchani kinakwisha na makali take. Fanya kazi kubwa na ya ukweli.
8- Angalia na tafakari NYONI aliumiaje umiaje? na aliumizwa na nani? ukipata jibu utajua hii ilikuwa mechi 10 ndani ya 1
9- Ditraaaaam, anadokoa mpira Wawa linapita kama Guruwe pori, Manula mpira unampiga usoni ni bahati tu.
10- wooooooo woooh PS machine ana drive kwa kasi kuelekea goli la Simba pasi kwa Kaseke anaachia mkwaju unakula nguzo.
Ditram tayari aliamini ni goli anasubiri kushangilia tu. Bahati yao .
Mh JPM, rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania - ALIKUWEPO
Mh AHMAD AHMAD - rais wa Caf ALIKUWEPO
MH WALACE KARIA- rais wa TFF ALIKUWEPO.
mechi ilichezeshwa na Marefaree 6.
Jamani Hii ilikuwa 1(10)