Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes, ila kama nakumbuka vizuri ya Ikpeba ndiyo iliamua matokeo.
Nigeria nilikuwa nawaelewa sana kipindi kile.
Yes, alianza kukosa kanu ndio akaja kukosa ikpeba.
Enzi hizo ilikuwa nigeria, france na arsenal huniambii kitu.
Liverpool Vs Chelsea(1-1)...Msimu wa Mwaka jana. Daniel Sturridge anasawazisha GOLI dkka ya 93 anapiga 90º(degree)... hii Game nakbuka mpira ulipigwaa Sanaaaa! KLOP Akawa anacheka tU akamfata Masigara wa chelsea Akamuliza "Are u Enjoying"....hakika mpira Ulipigwa Sanaa.....Nakumbuka hadi Barca dakika za mwisho wanasubiria mechi kuisha wakaanza kuchana nyavu..
Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
Mimi nilikuwa namfuatilia De Jong na Xabi tu ila timu zote sikuwa nazishabikia kwenye hiyo world cup final.Bercelona na Man United.. UEFA final 2011
Spain na Nertherland world Cup S. Africa 2010..
Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
We jamaa ni shabiki wa man U1. Man. City vs Man. United 2 - 3
Hii kwangu ndio the best na ninayoikumbuka muda wote, nilikata tamaa baada ya kipindi cha kwanza nikiamini tayari tumewapa City ubingwa. Mwisho wa siku ilipigwa comeback ya nguvu second half.
2. PSG vs Man. United 1 - 3
"Mountains are there to be climbed" Solskjaer alionyesha ni jinsi gani hupaswi kukata tamaa, tumeona hata walichofanya Liverpool dhidi ya Barcelona.
3. Tanzania vs Uganda AFCONQ
Sikumbuki kama kuna game ya Taifa Stars nilishangilia kama hii, kushuhudia timu ya taifa langu kushiriki michuano mikubwa kama ile ilinipa furaha sana.
4. Kenya vs Tanzania AFCON
Hii iliniumiza sana tulistahili kushinda kwa jitihada wachezaji wetu walizoonesyesha uwanjani.
5. Man. United vs Chelsea 4 - 0
Hii ni special sana kuanza msimu tu na kumla mtu 4 kuliniaminisha mengi huenda msimu huu ni wetu tunabeba kombe kumbe sivyo.
6. Real Madrid vs Liverpool UCL Final
Kitendo cha Salah kuchezewa rafu ile kiliniuma, Liverpool walipambana sana kufika pale. Kiupande wa kishabiki nilifurahi Ronaldo kuongeza UEFA nyingine.
7. Uruguay vs Ghana WC 2010
Daaah kila nikimumbuka ile penalty ya Asamoah Gyan na ile shangilia ya Suarez naona kama waafrika hatuna bahati WC.
8. Man. United vs Arsenal 8 - 2
Hii sitasahau kumpiga mtu 8 EPL sio jambo dogo tena Arsenal.
9. Ajax vs Man. United 0 - 2
Baada ya kimya kirefu kule UCL timu yangu pendwa angalau tukabeba kombe letu la kwanza la UEFA Europa League.
10. Juventus vs Man. United 1 - 2
Daah ile free kick ya Mata sitaisahau tuliuaminisha ulimwengu hata kama sio bora sana ila tunapambana.
Die-hard fan kabisa mkuu.We jamaa ni shabiki wa man U
komesha korona