Mechi ya fainali Esperence vs Wydad casablanca yatuvua nguo waafrica.

Sasa kwanini kwanini VAR iwe mbovu???? wakati kwenye match ya kwanza ilitumila bila utata???
 
yeah kweli... CAF wamezingua sana
 
Kwanza Hao waarabu wote washenzi wanatufanyiaga figisu timu za sub Sahara
Wajinga sana Hao
Hamna lolote...waarabu wanakuwaga wana timu mzuri....mbona ukijipanga kama mazembe unawafunga. Tatizo sie wenyewe timu zitu magumashi
 
Sasa kwanini uendelee kucheza wakati unadhulumiwa haki yako??? We unaona walichofanyiwa Casablanca ni sahihi???
 
Goli lililokataliwa lilikuwa goli zuri mno!!! Mfungaji alimtoka mlinzi akiwa amezubaa baada ya mpira kuwa umeshapigwa halafu akauunganisha mpira kwa kichwa hadi nyavuni. Ukiangalia replay huwezi kuamini kwa nini refa alilikataa goli hilo. Kama mnakumbuka goli alilofunga Torres akiwa chelsea dhidi ya Barcelona mechi ya pili ya nusufainali. Alichomoka baada ya mpira kuwa umepigwa akawa peke yake huko mbele na akafunga goli.
 
Hao waliogoma kuendelea na mechi (Wydad) inabidii waadhibiwe (ikiwezekana wafungiwe kushiriki haya mashindano) maana huko ni kukosa nidhamu kwani baada ya mechi wangepeleka malalamiko yao kwa wahusika.
 
Wanasema eti washabiki Africa hawana tabia ya kusafiri. Wanaangalia kuuzika kwa ticket zaidi. Hata mimi naungana na mawazo yako. Halafu wafanye fainali moja tu.
Mbona mashindano yana sponsor mzuri tu ambaye ni TOTAL na wameweka dau la kutosha? Kwani mashabiki wasipokuja wao linawausu nn? Marefa, mpaka waokota mipira wanalipwa na sponsor mbona kule Misri na Nchi nyingine za kiarabu kuna wakati mechi uwa zinachezwa bila mashabiki kabisa kwa sababu ya fujo zao lkn simpira uwa unachezwa? Wasituletee uzwazwa fainali ichezwe moja kwenye neutral ground ata wakiamua wawe wanapeleka uko dubai au falme za kiarabu ambapo juzijuzi walipeleka fainali ya ngao ya hisani.
 
Sasa kwanini kwanini VAR iwe mbovu???? wakati kwenye match ya kwanza ilitumila bila utata???
Hilo neno na ni aibu kwa CAF lakini tuseme AVR mbovu ingeweza pia kuwaokoa Casablaca kungetokea utata mimi maoni yangu pamoja na yote kutoka uwanjani ni kosa kubwa. Mimi nitakwambia tatizo lilianza mechi ya kwanza pamoja na kuwepo AVR wakasema refa hakuchezesha vizuri na CAF walivyokuwa wajinga wakamfungia yule refa wa Egypt miezi 6 hii ikajenga taswira kuwa refa mbovu nao wamekuja huku kosa moja tu la refa wamegoma kucheza kwa kuamini mbona yule alifungiwa wa kwanza. wenzetu kule juu hawafungii refa wanamnyima mechi tu muhimu kwa muda lakini hawamshtumu refa uadilifu wake huku ni kinyume. CAF ndio wawajibike katika sakata hili.
 
Sasa kwanini uendelee kucheza wakati unadhulumiwa haki yako??? We unaona walichofanyiwa Casablanca ni sahihi???
Hapana sio sahihi na lile baada ya kurudiwa lilikuwa goal lakini tujiulize refa hata huko ulaya kwenye league kubwa tu kunafanyika makosa na mengine yanasababisha team kushuka kwa uzembe wa refa na kupoteza mamilioni. Hivi wapi tumeona team inatoka uwanjani sababu tu unahisi umeonewa. umefunga goal refa kakataa nenda funga tena watu wataona tu.
 

Chukua sujaa moja nahsi ndio utakua unatumia

Mawazo butu kuwah kutokea
 
Mapumbavu sana hayo Ma-CAF, ndiyomaana sikuhangaika jana kwenda kuangalia hiyo mechi 7bu ya awali tu ilishanionesha ishara kuwa Esperance FC ndiye atayebeba kombe kivyovyote tu.
 
Kiuhalisia Africa bado sana kimaendeleo.
Figisu za kijinga bado zinaitafuna africa.

Africa mpaka ifike huko ilipo ulaya nadhani bado sana na inatakiwa iendelee kutawaliwa na wazungu.

Uhuru ambao tunao bado ni ujinga mtupu.

Kwanini wasingetumia hata waamuzi watano, wawili nyuma ya magoli , wawili pembezoni mwa uwanja kama kawaida na mmoja wa kati, mambo yangeenda poa tu.

Kwa sisi Africa ushindi huwa ni wamezani hakuna mashindano ya maana wala yenye uhalali.

FAINALI MBILI NDIO UPUUZI ZAIDI.

BORA ZAIDI HATA INGECHAGULIWA NCHI MOJA WAPO MWANACHAMA WA CAF NDIO IKAFANYIKA FAINALI.

Kwann hawajiulizi huko ulaya hakuna fainali mbili?

Hawajui kuwa wenzao pia walipitia mambo kama hayo mpaka kufikia hatua ya kufanya maamuzi angalau sahihi?

Mambo ya miaka kama 100 yaliopita bado tuanayazingatia?

Aisee !!!!!
 
Kwanini wasingetengeneza hiyo VAR kabla ya mechi au waghairi mechi kusubiri hadi VAR kutengamaa ndipo ichezwe fainali?

Esperance ilibebwa kwa mbeleko ya kiwango cha flyover[emoji26]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…