Mechi ya Ligi, Yanga na Mashujaa kuamriwa na Polisi kesho Disemba 19

Mechi ya Ligi, Yanga na Mashujaa kuamriwa na Polisi kesho Disemba 19

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kesho, Alhamisi Disemba 19, 2024, mashabiki wa soka watashuhudia Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Mashujaa, mechi ambayo itaamuriwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Sady Mrope. Mwamuzi huyu, ambaye pia ni miongoni mwa waamuzi waliothibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo wa Ligi.
IMG_1779.jpeg

IMG_1785.jpeg
Klabu ya Young Africans (Yanga SC) inashuka dimbani kesho ikiwinda alama tatu muhimu katika harakati za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC.
IMG_1780.jpeg

Yanga, ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 27 baada ya kucheza mechi 11, inakabiliwa na changamoto kubwa ya kupunguza pengo kati yao na viongozi wa ligi, Azam FC, ambao wana alama 33 baada ya mechi 15.
IMG_1781.jpeg

Huu hapa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC | Disemba 19,2024;
IMG_1783.jpeg

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC;

Disemba 19, 2024

Yanga SC vs Mashujaa FC
Saa 10:00 Jioni
🏟️ KMC Complex (Football Stadium)

Disemba 20, 2024
• Namungo FC vs JKT Tanzania
Saa 1:00 Usiku
🏟️ Majaliwa Stadium
 
Huyu mmeshamnunua nini mbona maelezo mengi wakati tulikataza kujielezea sana
Upolisi wake ni ajira...
Uamuzi ni kipaji....

Wala hakabi nafasi kwanza ishu ya urafarii bongo ni kazi ambayo Iko wazi imajini kina Tatu Malogo wanapata nafasi...
 
Hii dhana ya kizamani ya kuingiza askari polisi kwenye uamuzi wa mpira tukiaminishwa ni wasafi imepitwa na wakati.
U referee ni professional
Yuko pale kwasababu sababu ya taaluma Ile kazi ya uamzi ameisomea na ana performance nzuri mno
Hachezeshi kwakuwa ni askari mle uwanjani hamna vibaka
 
Hii dhana ya kizamani ya kuingiza askari polisi kwenye uamuzi wa mpira tukiaminishwa ni wasafi imepitwa na wakati.
Kwenye mpira hawaingii kama askari polisi, ni kama refa anaetambulika. Uaskari ana uacha huko
Tuna timu za majeshi ziko ligi kuu, na baadhi ya askari wanachezea ligi kuu
Tuna wana riadha wa majeshi mpaka wanawakilisha nchi kimataifa. Ila huto sikiia wakijifia kazi nyingine

Bottom line is hata refaree wana kazi zingine za kuwaingizia kipato. Refaree si kazi ya kudumu
 
U referee ni professional
Yuko pale kwasababu sababu ya taaluma Ile kazi ya uamzi ameisomea na ana performance nzuri mno
Hachezeshi kwakuwa ni askari mle uwanjani hamna vibaka

Kwenye mpira hawaingii kama askari polisi, ni kama refa anaetambulika. Uaskari ana uacha huko
Tuna timu za majeshi ziko ligi kuu, na baadhi ya askari wanachezea ligi kuu
Tuna wana riadha wa majeshi mpaka wanawakilisha nchi kimataifa. Ila huto sikiia wakijifia kazi nyingine

Bottom line is hata refaree wana kazi zingine za kuwaingizia kipato. Refaree si kazi ya kudumu
Sasa kama ni hivyo mbona huu uzi umejaa wasifu wake wa kuwa yeye ni Polisi? Kwa nini tusingestick na fani yake ya uamuzi mengine yakawekwa pembeni?
 
Sasa kama ni hivyo mbona huu uzi umejaa wasifu wake wa kuwa yeye ni Polisi? Kwa nini tusingestick na fani yake ya uamuzi mengine yakawekwa pembeni?
Kuwa mwamzi hakumvui upolisi wake
 
Hawa ndo wanakaba ajira za watu wengine
Huu mtazamo inabidi uondokane nao. Maana hauna uhalisia. Waamuzi duniani kote wana shughuli zao binfasi wanazofanya! Na hawapo kwa ajili ya shughuli ya uamuzi pekee.

Na kama kuna waamuzi wa aina hiyo, basi watakuwa wanapatikana Tanzania pekee.
 
Ngoja tuone kama hakutakua na makosa ya kibinadamu
 
Back
Top Bottom