Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kesho, Alhamisi Disemba 19, 2024, mashabiki wa soka watashuhudia Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Mashujaa, mechi ambayo itaamuriwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Sady Mrope. Mwamuzi huyu, ambaye pia ni miongoni mwa waamuzi waliothibitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo wa Ligi.
Klabu ya Young Africans (Yanga SC) inashuka dimbani kesho ikiwinda alama tatu muhimu katika harakati za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC.
Yanga, ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 27 baada ya kucheza mechi 11, inakabiliwa na changamoto kubwa ya kupunguza pengo kati yao na viongozi wa ligi, Azam FC, ambao wana alama 33 baada ya mechi 15.
Huu hapa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC | Disemba 19,2024;
Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu NBC;
Disemba 19, 2024
• Yanga SC vs Mashujaa FC
Saa 10:00 Jioni
🏟️ KMC Complex (Football Stadium)
Disemba 20, 2024
• Namungo FC vs JKT Tanzania
Saa 1:00 Usiku
🏟️ Majaliwa Stadium