Mechi ya Simba vs Mtibwa na Ihefu, siyo kipimo sahihi kwa kwa mchezaji Jean baleke na kuanza kumuita "the goal machine"

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Najua matusi na kejeli zitamwagika Kama mvua ya mawe baada tu NALIA NGWENA kuzungumza ukweli huu mchungu usiopingika.

Zimeibuka kelele nyingi zakumtukuza Jean Baleke kuwa ni "talk of town" wengine wakikata mayenu Kama Pape osumane sakho alivyokuwa akimburudisha sadio mane na wenzake ndani ya timu ya taifa ya Senegal.

Makelele ya Jean baleke kuwa ni goal mashine yamenishitua mwamba nakwenda kupekua wasifu wake nione je huko alikotoka ana uchembe chembe wakufunga magoli?? Maana ni Jambo la kushangaza kumtukuza kwa kuifunga ihefu na mtibwa Tena mpira wote tumetazama, mpira uliochezwa na mtibwa na ihefu ni wa kiwango Cha chini sana hata babu yangu mzee NGWENA ukimpa jezi anafunga.

Jean baleke alicheza Lebanese leage timu inayoitwa nejmeh jumla ya michezo 11 dakika 519 jumla ya magoli yote ni 3 na assist 1.

Akiwa TP Mazembe mwamba Jean baleke alicheza michezo 5, dakika 196 hakufanikiwa kufunga goli Wala assist yakufutia machozi.
Kwa takwimu hizo mbovu na ndiyo maana tp Mazembe waliamua kumtoa kwa mkopo kuja katika league yetu hii tia maji tia maji.

My take, bado Jean baleke hajafikia hatua yakuitwa "the goal machine" Kwa kuifunga mtibwa na ihefu, timu zilizocheza mpira kwa kiwango dhaifu sana, Nasema siwezi kumpamba au kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa huo ni upuuzi.
View attachment 2581894View attachment 2581895
 
huu ni ukweli simba juzi walitupa maburineti mochwari
Kweli mkuu mpira ni mchezo wa wazi kabisa, kiwango walichokionyesha mtibwa na ihefu huwezi kuanza kumpamba mtu wakati galasa tu.
 
Mkuu kazi ya mshambuliaji ni kuweka kambani tu haijalishi atafunga dhidi ya timu gani.. Hata hao wakina Messi Na Ronaldo ukisikia wamefunga magoli mia saba ujue pia kuna matimu ya ovyo walifunga na rekodi zinaandikwa!
 
Mkuu kazi ya mshambuliaji ni kuweka kambani tu haijalishi atafunga dhidi ya timu gani.. Hata hao wakina Messi Na Ronaldo ukisikia wamefunga magoli mia saba ujue pia kuna matimu ya ovyo walifunga na rekodi zinaandikwa!
Upo sahihi lakini msitulazimishe tumpake mafuta kwa mgongo wa chupa nakumuita the goal machine for nothing.
 
Alicheza na top score wa sasa huko congo hebu cheki nani aliibuka na kiatu cha dhahabu.
Kaka Amewafunga horoya na raja sio ihefu zile..
Kumbe alicheza na top scor Mimi nilidhani yeye ndiyo alikua top scor Sasa kucheza naye ndiyo cv yakuja kututambia hapa [emoji41]
 
Kwa maneno haya unamaanisha ligi kuu sio kipimo sahihi cha kusema Mayele sio mshambuliaji hatari.
Kama alivyosema msemaji wa Simba kuwa ligi yetu ni dhaifu au umesahau.
 
Najua matusi na kejeri zitamwagika Kama mvua ya mawe baada tu NALIA NGWENA kuzungumza ukweli huu mchungu usiopingika...
Ligi ya lebanon dakika 519 kufunga goli 3 na assist 1 ni takwimu bora sana kwa striker maana ni sawa na kucheza mechi 5 tu na kufunga goli 3 ambayo ni sawa na asilimia 60 ya uwiano wa goli kwa mechi alizocheza
 
Ligi ya lebanon dakika 519 kufunga goli 3 na assist 1 ni takwimu bora sana kwa striker maana ni sawa na kucheza mechi 5 tu na kufunga goli 3 ambayo ni sawa na asilimia 60 ya uwiano wa goli kwa mechi alizocheza
Unajua ni kwa Nini Lebanese walimrudisha huyo mwamba mbayemuita the goal machine
 
Wenye akili ni wawili tu huko... unashindwa kujibu swali rahisi hivi
Aheshimiwe sana rage aliyesema wanasimba wote mbumbumbu [emoji41]
Sasa umeuliza swali au umeongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…