Mechi ya Simba vs Nyasa Big Bullet itakuwa ngumu sana, na huenda Simba ikafungwa lakini itavuka

Mechi ya Simba vs Nyasa Big Bullet itakuwa ngumu sana, na huenda Simba ikafungwa lakini itavuka

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Hii ni taa ya tahadhari,

Big Bullet walifungwa kwao goal mbili kwa bila, lakini haimaanishi ni wabovu. Matokeo yao hayo yalichagizwa pia na uwanja wao wenyewe, siyo mzuri Sana Kama ule wa Mkapa.

Uwanja wa Taifa ni mzuri kiasi kwamba team yeyote inaweza kuutumia. Mechi ya marudiano kati ya Simba na Big Bullet itakuwa na matokeo ya kikatili Sana kwa team mojawapo, kati ya Simba au Big Bullet kwasababu zifuatazo:-

1. Simba anaingia kwenye mchezo huu akiwa hana pressure ya mechi na kutokana na sifa zitakazochagizwa na mashabiki plus wachambuzi nchini, hii itatoa mwanya kwa wageni kujituma zaidi kwa uchungu wa kuforce kufuzu

2. Big Bullet ni wazuri bado, zile Tambo za mashabiki adui wa Simba kwamba Simba kashinda team ya kawaida Sana, usiwapumbaze wachezaji na benchi la Ufundi.

3. Muda waliocheza Big Bullet, saa tisa mchana uliwa cost wenyewe, walizani wanacheza na waarabu, sasa kwa asili ya team zetu nchini, mechi hii kivyovyote itakuwa jioni muda tulivu, hivyo kuna maajabu yanaweza kutokea.

4. Shamla za Mashabiki wa team ya Simba zitawatia nguvu Big Bullet kujitutumua zaidi ili wasiaibike mara mbili, huenda wakatolewa kwa aggregate ya tofauti ndogo Sana ama kwa penalty

NB: Maajabu ya mpira wa miguu siyo mageni sana, tuombe tarehe yenyewe ifike.

Simba inatakiwa kufanya bidii kuliko wakati wowote na wasibweteke kabisa, huenda ikawasaidia kufuzu.

Benchi la Ufundi litulie, lisipange kikosi kwa kubahatisha ikiwemo kuweka wachezaji kwa maana tu kila mtu aonekane kachangia kufuzu hatua inayofuata.

Pamoja na matokeo mabaya iliyoyapata Simba uwanja wa Taifa ambayo imepelekea kupungua kwa mashabiki kuingia uwanjani, bado nawashauri viongozi wa Simba kuhamasisha mashabiki wajitokeze uwanja wa Taifa, ikiwezekana, yale matangazo ya WAR IN DAR yangerudishwa, naona siku za hivi karibuni mashabiki wamepungua Sana kuingia uwanjani, hii nikwasababu hakuna uhamasishaji wa kutosha, siku hizi uwanja wa Taifa unajaa mechi za derby tu, tuhamasishe kwa kampeni motomoto ili team zetu zifuzu kwa kishindo.

Tunawaombea mfanikie katika hatua hii muhimu Sana Simba.

Mjumbe hauawawi,
 
Simba hawezi kurudia makosa ya makirikiri pia Mgunda hasubiri half time kumuonya mchezaji anayetaka kuchomesha nyumba anamuita anamuonya mara moja.

Wachezaji wanahaha kutengeneza cv za kuwasaidia kupanda thamani.

Moses Phiri atakuwa wa Moto sana na atatupia, Sakho atakuwa wa moto, Chama utakuwa mwiba safu ya ulinzi itahitaji ipate cleansheet nyingine tena.

Simba anashinda zaidi ya goli 5.
 
...Pamoja na matokeo mabaya iliyoyapata Simba uwanja wa Taifa ambayo imepelekea kupungua kwa mashabiki kuingia uwanjani, bado nawashauri viongozi wa Simba kuhamasisha mashabiki wajitokeze uwanja wa Taifa, ikiwezekana, yale matangazo ya WAR IN DAR yangerudishwa, naona siku za hivi karibuni mashabiki wamepungua Sana kuingia uwanjani, ...
ni matokeo gani mabaya ambayo Simba ameyapata?
 
Inawezekana saa 9 ya Malawi kuna baridi maana kule ni karibu na Mbeya
 
Nachojua mimi,
SIMBA
LUNYASI
WEKUNDU
TAIFA KUBWA
MWANA KULITAKA
MWANA KUIPEWA
WAZEE WA KIDEDEA
WATETEZI WA KWELI
WATOTO WA CAF
Yaan timu inayosakata kabumbu la viwango vilivyopitishwa na baba yao kipenzi CAF na kudhibitishwa na babu yao FIFA, na tena timu iliyo barikiwa na mwenyezi MUNGU tayari imeshafuzu makundi bila kupingwa! hata big bullet na festo do agosto wanalijua hili! wanaojitoa ufaham niwale misukule wa yule mbwa wa pinki
 
Ile timu ni mbovu! Na hata rekodi zake kwenye haya mashindano ni za kusikitisha. Hivyo siwapi kabisa nafasi.

Ninachofahamu kama mwanamichezo, wakija Bongo wanaweza hata kufungwa goli zaidi ya 3, iwapo tu watakosa nidhamu ya mchezo.
 
Alikufa nkana
Akafa al ahly
Akafa as vita
Akafa platnumz

This is another level simba inatisha simba anaua wakati huo AZAM tv wanarusha ndege la kivita angani ila simba ile ilikuwa ya moto sana kwa kweli mpira ulikuwa unapigwa kweli kweli.
 
Back
Top Bottom