Mechi ya Yanga FC Vs TP Mazembe - Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Mechi ya Yanga FC Vs TP Mazembe - Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Kesho ktk magazeti wataandika Yanga yafa kiumeee hehehe
 
Mimi kama mdau wa mpira wa miguu nimefuatilia sana mchezo huu wa leo kupitia luninga. Niseme ule ukweli mpira wa YANGA kwa sasa hivi uko juu sana na kwa kweli wamecheza kwa ustadi mkubwa sana licha ya kufungwa. Goli walilofungwa ni goli ambalo timu yeyote inaweza kufungwa na inajulikana mpira ni dakika tisini. Mimi binafsi nimewakubali sana YANGA.
Unajuwa ukiwa mshabiki wa damu huwezi kuchambua mpira sasa mimi huo mpira wa juu ni kama sielewi mpira wa aina gani maana unaona kabisa Mazembe wanajuwa wanafanya nini uwanjani. Sijaona hata clear chance moja ya kusema Yanga wangefunga zaidi ya Mazembe kukosa magoal japo machache. Mazembe unaona kama kabisa wanatafuta nini sasa sisi Tz ndio maana hatuendelei tunaangalia square pass wanazopiga Yanga ambazo hazina madhara yoyote na mchezaji gani asiyeweza kupiga pass kama hizo ndio maana kuna watu kama kina Iniesta wakichomeka pass ni balaa, hebu tusemeni ukweli ni wakati gani uliona Yanga wanaitishia Mazembe na ndio maana ukaona hata washabiki wa Yanga kuanza kuondoka uwanjani maana walikuwa hawaoni goal litatoka wapi.
 
Wewe jifariji tu lakini kipigo kiko pale pale.

Hata kama Katumbi angekuwa amekufa kabisa kushindwa kuwalipa wachezaji ndani ya muda mfupi hivi ni ndoto.

Hayo mambo yako bongo tu kwenye soka la magazetini yaani Muro kawa maarufu kuliko Amis Tambwe na Kamusoko.
Umenivunja mbavu kwa kicheko, ulijuaje?
 
Umenivunja mbavu kwa kicheko, ulijuaje?

Mazembe kuifunga Yanga wala haihitaji unabii ni kitu kiko dhahiri sema huyo kijana alikuwa analeta siasa kwenye soka.
 



Wakuu wote wa JamiiForums,

Leo jumanne jioni ya saa 10 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam itapigwa mechi kati ya Yanga ya Tanzania na TP Mazembe ya Congo DRC!

Ni mechi ya kimataifa, Kombe la Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF! Tayari Yanga ina rekodi ya kufungwa katika mechi ya kwanza na MO Bejaia ya nchini Aljeria.

Mechi ya leo Yanga imejigamba kushinda na imefanya mkakati wa kuingiza wanachama wake bure ili kutia nguvu. Tutakuwa Live hapa JF kuwaletea matukio yote kabla na baada ya mechi.

Pia Azam TV na Super Sport itakuwa live. Asubuhi na mapema mashabiki wa Yanga na wapenda kabumbu kwa ujumla wameanza kumiminika Taifa kushuhudia kipute
yctp-jpg.360844

Kikosi kamili cha Yanga leo



Tatizo la mashabiki wa Yanga ni kwamba hawatumii akili na mifano hai. Mungu wao (Mze Akilimali) akiwadanganya kuwa watashinda, wao wanaamini hata bila kufikiri. Miaka nenda rudi Yanga wao ni kusindikiza tu hamna zaidi na mjadala hapa. Viongozi na mashabiki wao wanafikiri mpira ni magazetini tu na kipindi cha michezo huku wakijigamba. Wanajiita wa kimataifa, kumbe ni wacheza shoo tu. Waliniacha hoi mashabiki wao baada ya mechi, eti walikuwa wanasema Mungu wao (Mze Akilimali) aliwaahidi ushindi mnono na wakamuamini. Wana Yanga, inabidi muishi kwa mifano, jiulizeni ni lini timu yenu ilifanya vizuri kimataifa? Mtakwenda Uturuki sijuwi wapi na kuwatia hasara wafadhili bure lakini hamfiki kokote. Si mmeona wa kimataifa wanavyocheza mpira? Watalii wenu walitegemea offside, wa kimataifa (Mazembe) wakategua mtego wao wa kijinga na kuwatundika bao. Tena waliwaonea huruma tu ilibidi mfungwe hata 4 - 0 nyumbani kwenu, haibu kweli.
 
Manji alisoma alama za nyakati ndomaana akaamua waingie bure tu ili kupoza machungu yapesa yao


Mani ana avili sana.....Tatizo la cana Yanga ni kwamba sana avili za mkato. Yaani wanashindwa kujuwa kuwa timu yao ni wasindikizaji miaka nenda miaka rudi....mpaka leo wana Yanga wanategemea kamati ya maadili na wazee wa club ili wapate ushindi.
 
Eti Yanga iliwapa wakati mgumu sana TP Mazembe!!! But at the end of the day everyone knows what the score boards were reading.
 
Yaaaniii wamshukuru sana yule refaaa, jana tungewabugiza tatu bila!!!! Tena tena bahati yao kweli kweli, ila wajiandae tunaenda kuwafunga huko huko kwao, pambaf zao
Aahaaa kumbe naota tuuu, all in all zile njemba zile jana zilitu komesha kweli Yaani zimetulaza saa na nusu, alooo natamani nimtandike shabiki wamatopeni mmoja nondo ya kiuno adi akate pumzi, yaani leo sitaki kabisa utani!
 
Back
Top Bottom