Mechi za Simba SC kuonyeshwa Dstv

Huo mkataba Azam na yanga wameingia unahusu nini ambao Simba hawakuingia ?Azam ana rights za kuingilia Mambo ya Simba wakati hana mkataba?
Kwenye ligi kuu lazima Azam ataonesha mechi zote hata za sinazohusu Simba kwasababu ndio ana broadcasting right kwenye ligi kuu. Azam hawatohusika na Simba kwenye matukio binafsi yahusuyo Simba Kama vile Simba day na mechi za klabu bingwa hatua kabla ya makundi
 
Yani Azam anunue game ya Yanga ya Away? Acha kudanganya, kwamba yanga ana Haki na game ya Away Champions League?
 
Yani Azam anunue game ya Yanga ya Away? Acha kudanganya, kwamba yanga ana Haki na game ya Away Champions League?
Preliminary round ya CAF champions league haioneshwi kwenye Dstv mkuu na hata second round Pia, ila kuanzia makundi huko ni uhakika Dstv ndo wanaonesha live
 
Na wewe bado Upo kwenye EGO TRAP ! Hatusolve matatizo kwa kuombeana mabaya ; Bali tuna solve matatizo kwa kukumbushana na sio kwa kuapizana na kuombea Shari wengine. It takes a lot of akili kuwa binadamu.

Think
 
Huo mkataba Azam na yanga wameingia unahusu nini ambao Simba hawakuingia ?Azam ana rights za kuingilia Mambo ya Simba wakati hana mkataba?
Azam kaingia na Bodi ya Ligi kuu kuonyesha Ligi kuu.
Pia ana mkataba wa miaka 10 na Yanga exclusively kuonyesha matukio ya Yanga (Yanga TV).
Na Simba exclusivey kwa miaka miwili (bado mmoja).
 
Na wewe bado Upo kwenye EGO TRAP ! Hatusolve matatizo kwa kuombeana mabaya ; Bali tuna solve matatizo kwa kukumbushana na sio kwa kuapizana na kuombea Shari wengine. It takes a lot of akili kuwa binadamu.

Think
Hilo lipo kwenye akili yake kwa kudhani matatizo kama hayo kuna watu wameumbiwa au wanachagua kuumbwa hivyo.Hakuna namna bora ya kumweleza mtu anaueandika upuunzi wa mibaguzi wa kimaumbile koasi hicho.Tofauti za kiitikadi na mitazamo mbalimbali ziziingezwe kwenye maumbile , anayeswa na udhaifu aliozaliwa nao mnamuongezea mzigo mwingine wa ubaguzi na kujiona kuwa yeye sii binaadamu
 
hiyo hiyo bingwa mara nne mfululizo
Ndugu yangu hamka toka usingizi usipende kudanganywa kupita kiasi.

Hadi sasa kwa bongo Africa Mashariki hamna league inayoweza kuingia mkataba na Dstv na ikaleta faida kwa wote wawili.
 
Hicho kitu hakiwezekan matangazo n Mali ya bodi ya ligi na azam
 
ni kuanzia hatua ya makundi huku wanpoanzia ngumi za utangulizi haki za matangazo unachagua umpe nani
 
Kunywa maji mengi mzee
Kabla ya kutaka kuombwa radhi na Azam, mlitakiwa kwanza mumshinikize Ismail Aden Rage, aifute ile kauli yake ya kuwaita "mbumbumbu"

Maana mpaka leo hii kauli inawatafuna kweli kweli! Na bado inaishi.
 
Kabla ya kutaka kuombwa radhi na Azam, mlitakiwa kwanza mumshinikize Ismail Aden Rage, aifute ile kauli yake ya kuwaita "mbumbumbu"

Maana mpaka leo hii kauli inawatafuna kweli kweli! Na bado inaishi.
mechi zetu hazioneshwi na watukanaji
 
Reactions: mmh
Azam tv wapo hadi morocco kwenye camp ya Yanga
 
Attachments

  • 2888529_azamsports2_1629428496217627.mp4
    4.5 MB
Azam media ni ujinga mkubwa walifanya kumruhusu mlevi mmoja kutukana taasisi,tukio ilo limeonyesha udhaifu mkubwa kwa management ya Azam media chini ya Tido Muhando.
Walipaswa kuieshimu taasisi ya Simba ambayo imekuwa mdau wao wa miaka mingi, Simbasc,imechangia sehemu kubwa kwenye mafanikio ya Azam tv.
bado tuna kumbukumbu aliewahi kuwa mwenyekiti wa club ya Young African SC,bw Yusuph Manji alipokataa kushirikiana na Azam kuonyesha mechi za yanga kwa madai Azam media kutoa pesa kidogo ambazo hadhikidhi mahitaji na ukubwa wa Yanga,madai ambayo yalikuwa ni kweli.
Simba SC ikasimama upande wa Azam media na kukubali kiasi cha pesa kitolewe sawa kwa timu zote shiriki za ligi kuu wakati huo, kwa manufaa ya mpira wa nchi hii.

Kama bado aitoshi Simba SC wakaipatia nafasi Azam kuonyesha matukio ya Simba day toka kipindi inaanzishwa kabla ya timu zingine kuiga idea hio nzuri,bado Simba ikawapa Azam nafasi ya kuonyesha michuano ya club bingwa kwa hatua za awali mechi zote za nyumbani,Simba ilifanya vizuri hivyo kituo cha Azam kuendelea kuwa na biashara nzuri
MO Dewji kupitia Simba ameleta mafanikio makubwa kwenye ligi za mabingwa wa africa kwa vilabu,kufanya vizuri kwa simba kumeongeza nafasi za ushiriki na kuongeza ubora wa ligi yetu,kitendo ambacho kimeipa Azam umaarufu na biashara nzuri kwa watu kununua visimbuzi ili kuangalia ligi yetu,hivyo hawakupaswa kuruhusu mlevi mmoja kuwatukana watu ambao ni washirika wenu kibiashara!!

Nashauli Simbasc ichukue hatua kali ikiwemo kukataa kushirikiana na watu wa Azam media mpaka pale watakapoomba radhi,Simba ni taasisi kubwa lazima ipewe heshima na hadhi zinazo takiwa.
 
Kabla ya kutaka kuombwa radhi na Azam, mlitakiwa kwanza mumshinikize Ismail Aden Rage, aifute ile kauli yake ya kuwaita "mbumbumbu"

Maana mpaka leo hii kauli inawatafuna kweli kweli! Na bado inaishi.
Kama vile kauli ya Luc kuwa nyie ni uneducated,ni kima na mnachoweza ni kuzomea zomea tu inavyozidi kuwatafuna na itaishi milele na milele.
 
hapa Azam walizingua sana,waombe msamaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…