MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Ninaandika uzi baada ya kusoma habari mitandaoni inayosema kuwa kijana Dominik mmiliki wa room of jeans kuwadanganya wateja wake kuwa watauziwa suruali Tsh 5000 ila walipofika akawapa bei tofauti ambayo ni kubwa zaidi. Hii mimi naona haijakaa sawa. Dominik kateleza. Uongo wa aina hii kwenye biashara ni mbaya sana. Inaua kabisa jina zuri ulilopambania. Huu uongo hauna tofauti na ule uongo wa William Miller aliyewadanganya wafuasi wake akiwemo mmiliki wa kanisa la SDA Hayati Mama Ellen G White mwaka 1844 kuwa Yesu atakuja kumbe ni uongo mtupu. Watu waliuza vitu vyao wakijua ni mwisho wa dunia kumbe uongo mtupu.
Media sio mbaya ikitumika kiusahihi. Ila kwa uzoefu wangu wafanyabishara wadogo wanaoinuka hapa Tanzania wengi wamejipoteza kupitia media. Hawa vijana wafanyabiashara ninawashauri waongee na vyombo vya habari kunapotokea ulazima sana. Huyu Dominik baada ya hili sakata nimeona anatangaza atatoa tamko. Anakuwa hana tofauti na mwanasiasa. Media tuwaachie wanasiasa na wasanii kwa sababu kwa kazi zao habari mbaya ni kama habari nzuri.. cha muhimu waongelewe.
Vijana kuweni waaminifu na mpige kazi. Acheni mboyoyo za kujifanya motivational speakers. Piga kazi mafanikio yako ndo yataongea. Unapojiweka sana mbele ya camera ni upuuzi.