Media ni Mhimili Muhimu kama ile mitatu ila ni dhaifu kiuchumi. Je, imefika wakati wapewe Ruzuku au iachwe ipambane na hali yake?

Media ni Mhimili Muhimu kama ile mitatu ila ni dhaifu kiuchumi. Je, imefika wakati wapewe Ruzuku au iachwe ipambane na hali yake?

Yaan waandishi wa habari wamekuwa hovyo haswa...
 
Ruzuku wapewe JF tu

Hiki ni Kisima cha Habari za Dunia nzima kwa kila dakika inayokatika

Vyombo vingine wanasubiri teuzi tu lakini JF Akina Lucas, Mzee Mgaya, Erythrocyte nk wao wako kizalendo zaidi 😂😂
100%
Vilivyobaki viko mfùkoni mwa sisiemu
 
Wanabodi

Wiki hii nzima, nimekuwa jijini Dodoma kuhudhuria mikutano 3 muhimu ya mambo ya habari. Tulianza na Mkutano Mkuu wa 13, wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, Mgeni rasmi ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dotto Biteko. Ukaja Mkutano wa Baraza la Habari Tanzania, MCT, mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, na Ijumaa tukaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa habari, Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Hivyo mimi kama kawa na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali, maelezo, kisha jibu, utatoa wewe msomaji mwenyewe. Swali la Hoja ya leo ni Media ni Mhimili Muhimu kama Ile Mihimili 3, Ila uko Dholfu Bin Taaban Kiuchumi. Jee Ufike Wakati Media Iwezeshwe au Tuendelee tuu Hivi Hivi Tulivyo?.

Jana ilikuwa ni Siku ya Uhuru wa Habari Tanzania, Je kuna Uhuru wa Habari, Bila Uhuru wa Kiuchumi wa Media/Waandishi wa Habari?. Mtu mwenye njaa anaweza kuwa huru?. Media yenye njaa inayomtegemea source kwa usafiri na waandishi wa habari wenye njaa na umasikini uliotopea, kiasi cha kutegemea zile bahasha, wanaweza kuwa huru?!.

Tuna mihimili mitatu rasmi ya Serikali, Bunge na Mahakama, na mhimili wa nne usio rasmi wa Media. Mihimili hii mitatu ni well funded, well taken care of, well respeted, lakini huu mhimili wa nne wa media kiukweli uko kama mtoto yatima and nobody cares!.

Kitu muhimu number moja kwa nchi yetu ni Mwananchi, ndie mwenye nchi, mwenye katiba na mwenye kila kitu. Ni Mwananchi kupitia kura yake, ndie anamuajiri rais wa JMT na ile mihimili yote mitatu, na ni kwa kupitia kodi yake ndie anawalipa mishahara yao wote kuanzia mshahara wa rais wa JMT na serikali yake yote na mihimili yote, na kutoa fedha za kuendesha serikali na kugharimia kila kitu, lakini kwanini huu mhimili wa 4, umeachwa kama mtoto yatima?.

Kwa Mwananchi, ni mhimili gani ni muhimu zaidi kwake kati ya serikali, Bunge, Mahakama na Media?.

Wakati nikiishi Uingereza, niliajiriwa na taasisi ya FCO ya Uingereza, kwenye salary slip yangu, nikajikutwa nakatwa fedha zinaitwa Radio Levy, kwa ajili ya kugharimia Shirika la utangazaji la Uingereza, BBC. Pia kuna kodi ya TV set.

Nikamfuata mtu wa admini nikamwambia mimi kwangu sina redio, wala sisikilizi BBC, na hata kama ningekuwa nayo, ningesikiliza RTD na sio BBC, hivyo naomba kwenye slip yangu nisikatwe Radio Levy wala TV Set. Ndipo nikaelezwa malipo hayo ni statutory, lazima ulipie uwe unasikiliza BBC au hausikilizi, as long as uko UK, and you make money, una wajibu wa kugharimia media, utake usitake!.

Sisi Tanzania pia tuna statutory payments kugharimia mambo mbalimbali, kwenye mafuta, kwenye umeme, kwenye maji, kuna SDL etc na tunatoa ruzuku kwenye maeneo mengi tuu ikiwemo ruzuku kwa vyama vya siasa, nani muhimu kati ya media na vyama vya siasa hadi kustahili ruzuku?.

Jee ufike wakati Tanzania tuintroduce media levy, huu mhimili wa 4, nao ugharimiwe kama ile mihimili mitatu mingine, au media iendelee kuachiwa hivyo hivyo ipambane na hali yake?.

Paskali
Wakati nasoma hii makala nikawa natafuta ni wapi ungesema hela zipelekwe. Ninachoona hakuna center zaidi ya RTD na TBC. Kwanza hii taasisi hata hivyo inaendeshwa kwa kodi zetu ambapo ni ruzuku tosha. Sasa hapa utatengeneza mtafaruku mkubwa sana wa kimaslahi kwani media imegawanyika sana japo lengo lake ni moja. Hapo itabidi tena iundwe mamlaka ya kusimamia media (au ndio MCT?). Hata ikiwepo hiyo mamlaka ni wazi kwamba focus itaondoka. Kwa hili ibaki tu kusema media tunawapenda ila kwa ishu ya ruzuku, no!
 
BBC ni chombo cha umma, Kama serikali ikiiga utaratibu wa UK ni wazi pesa hizo zitaenda TBC.
Pia iwapo serikali ikianza kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari ni wazi ile sifa ya Muhimbili usio rasmi itapotea mifano halisi tunayo.
Wakati vuguvugu la vyama vingi linaanza vyombo vya habari binafsi vilifanya kazi kubwa kufichua maovu magazeti Kama Family mirror, motomoto hata wewe mwenyewe ulikuwa na kipindi kinaitwa kitimoto ingawa ungekuwa nacho Hadi Sasa ingebidi ubadilishe jina.
Hata baba wa Taifa aliwahi kusifia vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri kuliko vyama vya siasa.
Sasa hivi vyombo karibia vyote vimepoteza uhuru na vimebaki na kazi ya kusifia. Hata humu ukiandika habari inayogusa viongozi wa serikali hata Kama una ushahidi itaondolewa. Kuwalipa itakuwa matumizi mabaya ya Kodi za wananchi.
 
Back
Top Bottom