Media za Bongo na Mwijaku ifike sehemu lazima wawe serious sasa tumemchoka huyu jamaa

Mkuu unajipata tabu bure ukiona mtu anakuboa unaacha kumfuatilia, mimi Mwijaku ananiboa kiasi kwamba sifuatilii kipindi chochote anachohusika yeye.
Kuna kipindi nilikuwa nimemfollow Le Mutuz Instagram, nikawa nakasirika na mambo yake, baadae nikajitafakari nikagundua yeye hana tatizo mwenye tatizoni mimi ninayejifanya namchukua wakati nimemfollow maana anaishi maisha yake. Nikafanya kumu unfollow, kuanzia siku hiyo uwa nasahau hadi kama kuna mtu anaitwa Le Mutuz maana sikutani naye tena mtandaoni kama ilivyokuwa awali.
 
Alifukuzwa kwa ishu gani?maana wiki kadhaa baada ya kupata sifuri za wajumbe alihojiwa na Azam TV akasema ndio mara ya kwanza anapata sifuri kwenye maisha yake,maana UD katoka na First class
 

Hongera kwa kuwa mjanja vipi mpaka sasa bado umekaa kitapeli tapeli ?
 
Hongera kwa kuwa mjanja vipi mpaka sasa bado umekaa kitapeli tapeli ?

Hapana sijakaa kitapeli.. shida elimu ya zamani vyuoni walizoea kuona mwaka wa kwanza wapo kizembe zembe rafu rafu hivi...
Mzumbe first year huwa wanatuita form one.. kulikuwa na ujinga flani wa kutuona first year washamba sana...
sasa walivyotuona sisi tumeripot na tukaenda bar siku hizo hizo za orientation na hatujavaa kishamba shamba.. wakatuona tofaut na first year wengine.. ndio maana mwijaku akaanza kutuzingua bar.. anashangaa mwaka wa kwanza tumeagiza konyagi na bia za kutosha kama wazoefu vile.. na mziki ukipigwa pub tunaucheza bila aibu.. wakatushangaa why tunajiamini wakati wageni ndio.tumeripot chuo jana tu
 
Huyo ni paid actor, hapo anamtumikia Kafir apate mradi wake...hizo mic zote ni part ya dili.

Clouds wanamlipa kum harass Diamond na WCB, ndio maana huwezi kumsikia akiongea chochote kibaya cha Kiba au Harmonize maana hao ni Watiifu wa Clouds. naye anawakilisha Clouds.
 
Heeeeeeh kumbe n tapeli na mwizi konki, tena jambazi la kutisha khaaaaaah, duuuuh hatariiiih sana
 
Huyo anaumwa anaweka ushabiki mbele sasa ibra unawez ukamfananisha daimond platnum dah kaishiwa point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…