Ki ukweli bado zinaweza kuwa zinaendeshwa kwa hasara na hili ukitaka kujua vizuri ni pale tunapoweza kuangalia ROI kwa kuangalia muda na rasilimali ilyotumika na tukachukulia kuwa huo ni mkopo wenye riba.
Bado jamii hainufaishi na uendeshaji au uwepo wa hizi stendi katika kuongeza kipato na hii inatokana na kuwa na viongozi wasio wabunifu katika kuwezesha kuongeza kipato - sioni sababu kwa stendi hizi zisiweze kufanya kazi masaa 24 angalau kwa kuwa na mabasi yatakayoenda mkoa mmoja kwa masaa 24 kwa pande nne mfano kituo cha Dodoma kiweze kuwa na safari zifuatazo kwa masaa ishirini na nne.
- Dodoma -morogoro
- dodoma Manyara
- Dodoma-singida
- Dodoma -Iringa
Na kila mkoa ikawa na root angalau za mkoa momoja kwa masaa 24 kiasi kwamba mtu akiwa anaenda arusha anauhakika akifika manyara atapata basi la Arusha na akiwa anaenda mbeya akifika Iringa atapata basi la kwenda mbeya.
Kwa kufanya hivi shughuli zingine zinaweza kuendelea kwa kadri ya mahitaji.
Haikai sawa eti unastend lakini huwezi kusafiri usiku hii haiko sawa.
Hili ni eneo moja lakini eneo lingine kunatakiwa kutengenezwe mazingira yanayovutia kumaliza baadhi ya mikusanyiko ya kijamii hukohuko stendi zikiwepo kumbi za sherehe na mikutano kiasi kwamba watu wakimaliza wanaondoka sambamba na kuweka hotel pamoja na lodge kwa wenye kipato cha kati na kawaida ili ikiwezekana akifanya shughuli zake aweze kulala stend na kuondoka.
Mighahawa mizuri na sehemu zenye bustani nzuri na michezo ya watoto inaweza kuongeza tija wakati watu wanasubiri wageni wanaweza kupoteza muda kwa kuwa maeneo hayo au mtu akavutiwa kwenda kutembea na familia badala ya kwenda bar.