Mei Mosi 2021: Makosa niliyoyaona kwenye Hotuba ya rais Samia na wasaidizi wake

Kupandishwa mshahara ni kuongezeka kwa take home pay ambayo inaweza kuongezwa kwa kupunguziwa kodi. Je wafanyakazi hawajapunguziwa kodi Ingawa kidogo?
Nyongeza ya mshahara ina positive effect kwenye pension ndugu.Nyongeza ni muhimu kuliko posho
 
One similarity between samia and magufuli, wote walipata urais kama zari hawakujiandaa.
 
In USA millions died on the road to democracy..it is also the same to UK, Germany, Russia etc..
USA hakuna demokrasia kule weusi kila siku wanapigwa shaba na police

UK nchi la kifalme hakuna demokrasia napo

Russia napo hakuna demokrasia kabisaaa Putin anaitawala Russia kwa mabavu na mpinzani wake kisiasa kamfunga hahahaaaa

Tanzania well Magufuli alikuwa ni Rais aliyependa maendeleo alifanya vingi na hapa anayepinga ni mpumbavu tu nchi haiwezi kuendelea kwa watu kulalamika lalamika wapige kazi tu

Rais samia Sina shida nae hizi ni siku chache mno watu kumpima uongozi wake ameshaonesha ana nia njema na Tanzania twendeni nae naye anataka kutengeneza legacy yake kitu ambacho ni jambo jema kwake
 

Mkuu sasahivi Hayo Mashirika yanapeleka Mapato yao yooote Hazina/Serikali kuu...
Sasa wanabaki 0!
Lengo serikali kupitia Kapu kuu ili Wagawe kwa taasisi nyingine!na Maendelo kwa Kila sekta zipo sekta ambazo hazizalishi!
 
Watanzania wengi sio watu wa kufanya analysis kiwango kama hivi.

Heko mkuu
 
Kwakweli baada kifo cha mwendazake ilitakiwa uchaguzi ufanyike tupate kiongozi mpya hii hali ya leo imesikitisha sanaFuata katiba acha kujinyima

Kwakweli baada kifo cha mwendazake ilitakiwa uchaguzi ufanyike tupate kiongozi mpya hii hali ya leo imesikitisha sana
Fuata katiba acha kujitoa ufahamu
 
Mkuu hongera sana kwa maada hii na uchambuzi wako murua. Baada ya hotuba ile nami nilikuwa najiaandaa kutoka na uzi kama huu lakini nimeona mengi niliyofikiria umeyagusia hivyo mimi nitaongezea mawli niliyokuwa nimefikira yakiwemo hayo uliyoyajadili mkuu.

Kuna makosa naona yamefanywa na waandaaji wa hotuba ya rais. Rais hakuwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza isipokuwa alialikwa katika tukio la kitaifa na kimataifa lililokuwa linafanyika Mwanza. Kuanza kuwashukuru wanamwanza kwa kuichagua CCM na kuelezea miradi mbali mbali inayotekelezwa na itakayo tekelezwa Mwanza ilikuwa ni kukengeuka na kutoka nje ya lengo la shughuli tena wakati huo ameshawavuruga watu kwa kushindwa kukidhi matumaini makubwa waliyokuwa nayo ya kuongezewa mishahra.

Hiki kipengele hakikupaswa kuwepo katika kabisa hotuba ya Mei Mosi. Hayo yote aliyoyazungumza hayakuwa matarajio na mategemeo ya hadhira yake hivyo ilikuwa ni kuwachosha tu.

Jambo jingine ni mpangilio wa matukio au maelezo katika hotuba ya rais. Suala la mishahara ambalo ndilo lilikuwa hoja kuu iliyoyegemewa na kila mfanyakazi pale uwanjani na nchi nzima halikupaswa kuzungumzwa katikati ya hotuba kwakuwa ni wazi lilikuwa linakwenda kuwanyong'nyeza na kuwakera wasikilizaji wake hivyo lingewekwa mwishoni kisha baada ya hapo ashukuru na kuondoka. Baada ya taarifa ya kutoongezwa mishahara kila mmoja hakuona tena umuhimu wa kumsikiliza rais. Hili ni kosa lililovuruga usikivu wa hadhira.

Kingine ni kama ulivyosema kulikuwa na matarajio makubwa sana yaliyopita kiasi kuwa kutatangazwa ongezeko la mishahara. Sasa kwakuwa viongozi wa juu walikuwa wanajua walipaswa kuwaaandaa watu kulipokea hivyo. Hii ingefika mpaka kwa waandaa mabango yasomeke KAZI IENDELEE badala ya MISHAHARA JUU.

Kingine ambacho kingeweza fanyika pamoja na kuwa ni kigumu ilikuwa ni kwa mama kukwepa tukio lile na kumtuma makamu wake. Hii ni kwasababu inaonesha wazi alishafanya vikao na viongozi wa wafanyakazi na akawapa matumaini makubwa sana. Kila mtu jana alijua kikwazo cha kupanda mishahara alikuwa ni mwendazake. Hivyo ili kulinda angalau hadhi yake mama angetafuta sababu mapeema zaidi ya kutokuwepo jana huo msala umuangukie makamu. Hii ni kwasababu watu walikuwa na matumaini makubwa kuwa yeye ndiye mkombozi wa mkwamo wa kupanda kwa mishahara sasa wataanza kumuona hana tofauti na mwendazake ingawa mama alitumia lugha laini tofauti na mwendazake.
 
We acha mchezo, kwani katiba ndiyo imesababisha tusipate tamko? Watu tunataka nyongeza ya mishahara bwashee, hakuna anayekula katiba.
Ukiona chat inaongelea katiba juwa huyo ni mfuasi wa chadema. Wamekaririshwa hivyo.Katiba ya chadema ilichakachuliwa kipengele cha ukome. LISSU anajua lakini hawezi fungua domo lake
 
Ukiona chat inaongelea katiba juwa huyo ni mfuasi wa chadema. Wamekaririshwa hivyo.Katiba ya chadema ilichakachuliwa kipengele cha ukome. LISSU anajua lakini hawezi fungua domo lake

Hitaji la Katiba Mpya Tanzania sio hitaji la chama ama kundi fulani la watu. Ni hitaji la Watanzania wote.

Just take a moment and reflect on Warioba's commission work. Consider their data collection, collation analysis and their reports. Add on work of the special constitutional assembly.

Hizo kazi zote na yaliyotokana nayo tukisema yalikuwa ni mahitaji ya CHADEMA peke yake ama kundi fulani nchi mwetu tunakuwa hatutendi haki kwa akili zetu.

Ima hukuwa na ufahamu wa kufuatilia mchakato uliozalisha vitini na bango kitita pamoja na ripoti za Tume ya Warioba usione haya kuuliza wakubwa zako.
 
Umechachawa Mkuu au unachanganya madesa? Soma unielewe kabla hujakurupuka...
 
Kuna jamaa alilipa deni lake lote kupitia mwajiri wake kabla hata ya marekebisho ya Sheria yaliyoleta retention ya 6%. Lakini cha ajabu wamemdai retention amount mara 5 ya kiasi wanachodai hajakilipa wakati amewapelekea copy za salary slips zikionyesha alivyoanza na kumaliza kukatwa na mapengo waliyoyafanyia doubt. Bado wanasisitiza awasiliane na mwajiri wake. Angekuwa sio mtunza kumbukumbu mzuri ingekula kwake.
 
Umeandika nini hapa mkuu.

Mimi sitaki kutukana Ila unataka nitukane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…