Mei Mosi (labor day) ndo ilitakiwa iwe siku ya wajinga duniani

Mei Mosi (labor day) ndo ilitakiwa iwe siku ya wajinga duniani

Nashauri Ile siku ya wajinga ambayo huwa ni tarehe 1 April Sasa iwe mei Mosi

Lengo la mei Mosi ilikuwa ni kujadili na kupata suluhu ya changamoto za wafanyakazi

Huku kwetu ni tofauti
1. Watumishi wanaandaliwa lisala ya kusifia serikali
Badala ya kulalamikia

2. Watumishi wamepewa Fulani na kofia, kesho watakuwa viwanjani kama mijusi kafiri

3 maslahi duni ya wafanyakazi hasa polisi na walimu
Hawa watu wanalipwa mishahara ya house girl ila kesho wataimba tenzi za kumtukuza Kizimkazi

4. Vyama vya wafanyakazi kutetea maslahi ya serikali
CWT, tucta n.k hao ni wana CCM

5 Mazingira magumu ya wafanyakazi
Hasa polisi na walimu ambao wanaishi kwenye mabanda, huku wabunge ambao hawana kazi ya maana wakilipwa mamilion ya pesa

6 Serikali kupuuza changamoto za wafanyakazi
Serikali imewaona wafanyakazi kama mazuzu licha ya kuelezea changamoto zao ila imepuuza

7 Kusalitiana baina ya wafanyakazi
Wafanyakazi hasa walimu hawa husalitiana, wengi wanalalamika maslahi duni, wengine wanamchukulua form ya urais mwanasiasa

Binafsi nadhani mei Mosi ndo iwe siku ya wajinga au mazuzu duniani
Ondoa Hilo neno Duniani
 
Back
Top Bottom