Mkuu, nimejifunza sana hapa.
Pia nimetathimini nchi yangu Tanzania na vugu vugu la kiasiasa pamoja na hii Sera yetu mpya ya viwanda maana nikiangalia hiyo movement nashindwa kuelewa kama tuko salama na kwa kiasi gani?
Je, ndege zetu haziwezi haribiwa (bombardier), je viwanda vinavyojengwa vitakuwa salama?
Utawala na serikali yetu zitakuwa salama?
Na hii, ni baada ya serikali yetu kuja na mstakabali mpya wa maslahi ya Taifa kuliko hapo kwanza!
Daaah, maana naona hao jamaa wanatumia njia zote ili kutimiza azima yao ya kuharibu kila namna ya mfumo wa Iran na mipango yake ya nuklia mfano, fedha, siasa, ushawishi (lobbying) vyote vinatumika hadi kuua!!
Sasa, ukiangalia hapo Tanzania, je tuna watu wenye uzalendo huo wa kukataa hela ili wasituletee majanga katika nchi yetu?
Kwa ujumla ni hali ya utata sana , maana daaah, tunahitaji kufanya msasa mkubwa sana na kurekebisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hadi wananchi kuhusu kujenga uzalendo aisee.
Halafu, nimesikitika sana kuwa hao watu wa Iran, walipitisha baadhi ya virutubisho vya nuklia huku kwetu Tanzania japo vilikamatwa ila ni mbaya sana , je sisi hatukujua kuwa hivyo vitu ni hatari kupitishwa hapo Tanzania ?
Ila kwa ujumla , tunapaswa kuwa makini sana hapo Tanzania kwa sasa kuliko wakati wowote kwa kulinda Taifa letu.