Meir Dagan na ujasusi wa Mossad dhidi ya Iran kumiliki silaha za nyuklia

Meir Dagan na ujasusi wa Mossad dhidi ya Iran kumiliki silaha za nyuklia

hongera mkuu
pamoja na challenge hizo naona iran inasonga mbele
Shukran Mkuu, ngoja tuone mambo yaendavyo lakini unavyosema kusonga mbele katika nini? kwenye umiliki wa silaha za nyuklia sidhani kama wanasonga mbele kimsboy
 
Aaah, ni kweli unachosema.
Sasa katika hali hiyo, ndiyo sasa nchi zetu/ yetu wananchi wanapaswa kuwa wazalendo hasa na kuilinda nchi yake/ yetu.
Naelewa kuwa hao USA na wazungu koko wenzake huwa wanatenda vitu vingi kutuangusha mara zote.
Kwa hiyo, tushikamane kama nchi kujiimalisha
uzalendo muhimu na pia serikali ihakikishe hakuna mianya ya kuruhusu hayo kutokea Poise
 
Mkuu, nimejifunza sana hapa.
Pia nimetathimini nchi yangu Tanzania na vugu vugu la kiasiasa pamoja na hii Sera yetu mpya ya viwanda maana nikiangalia hiyo movement nashindwa kuelewa kama tuko salama na kwa kiasi gani?

Je, ndege zetu haziwezi haribiwa (bombardier), je viwanda vinavyojengwa vitakuwa salama?
Utawala na serikali yetu zitakuwa salama?
Na hii, ni baada ya serikali yetu kuja na mstakabali mpya wa maslahi ya Taifa kuliko hapo kwanza!

Daaah, maana naona hao jamaa wanatumia njia zote ili kutimiza azima yao ya kuharibu kila namna ya mfumo wa Iran na mipango yake ya nuklia mfano, fedha, siasa, ushawishi (lobbying) vyote vinatumika hadi kuua!!

Sasa, ukiangalia hapo Tanzania, je tuna watu wenye uzalendo huo wa kukataa hela ili wasituletee majanga katika nchi yetu?

Kwa ujumla ni hali ya utata sana , maana daaah, tunahitaji kufanya msasa mkubwa sana na kurekebisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hadi wananchi kuhusu kujenga uzalendo aisee.

Halafu, nimesikitika sana kuwa hao watu wa Iran, walipitisha baadhi ya virutubisho vya nuklia huku kwetu Tanzania japo vilikamatwa ila ni mbaya sana , je sisi hatukujua kuwa hivyo vitu ni hatari kupitishwa hapo Tanzania ?

Ila kwa ujumla , tunapaswa kuwa makini sana hapo Tanzania kwa sasa kuliko wakati wowote kwa kulinda Taifa letu.
Kazi kweli kweli Mkuu
 
Checking...100%
Searching...100%
Network connected !

Near by Soweto Mbeya.
 
Back
Top Bottom