Meja Jenerali Charles Mbuge astaafu utumishi wake jeshini

Meja Jenerali Charles Mbuge astaafu utumishi wake jeshini

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
491
Reaction score
1,907
Meja Jenerali Charles Mbuge amestaafu na kuagwa jeshini baada ya kulitumikia jeshi kwa miaka 38.

Enzi ya utumishi wake jeshini, aliwahi kuwa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Mkoa na baadae kushika majukumu mbalimbali ya kijeshi.

Anakumbukwa jinsi alivyokuwa kipenzi cha Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.

Ni katika awamu ya tano, ambapo Meja Jenerali Mbuge aliibuka baada ya kazi nzuri ya ujenzi wa ukuta wa Mirerena na kupanda vyeo mfululizo hali iliyoibua minong’ono kwa wengi kuwa alikuwa anaandaliwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi.

Tunakutakia maisha mema ya kustaafu, utumishi wako jeshini umetukuka!

IMG_2673.jpeg


Soma pia: Kwanini Rais Samia alimuondoa Meja Jenerali Mbuge kama Mkuu wa JKT?
 
We owe a debt of gratitude to those who have selflessly served our country. Thank you for your service and congratulations on your retirement." "Words cannot express our gratitude for your service and sacrifice. Your retirement is well-deserved and we wish you happiness and joy in this new chapter of your life Sir salute.
 
Pongezi na kwaheri.

Kwa sasa Jenerali anaweza kuwa kafanya kazi jeshini miaka 35 na hajapigana vita ya Tanzania.

Ukiondoa missions za kimataifa na shughuli za kujenga taifa za jeshi kama ufundi na kilimo, na ulinzi wa mipaka, majeshi yetu yanafanya nini hasa?
 
Kulinda mipaka ya nchi vipi ulikua na mapendekezo gani?
Sasa mbona tunawaona sehemu nyingi mbali na mipaka?

Wajikite zaidi kwenye shughuli za kiuchumi, watumike kujenga zaidi, watumike kwenye engineering projects zaidi.

Sasa hivi ukiondoa hizo habari nikizozitaja hapo juu, ambazo haziwezi kuchujua vikosi vingi sana, sielewi wanajeshi wanafanya kazi gani.

Hawawezi kuwa wanafanya mazoezi ya vita siku zote.
 
Sasa mbona tunawaona sehemu nyingi mbali na mipaka?

Wajikite zaidi kwenye shughuli za kiuchumi, watumike kujenga zaidi, watumike kwenye engineering projects zaidi.

Sasa hivi ukiondoa hizo habari nikizozitaja hapo juu, ambazo haziwezi kuchujua vikosi vingi sana, sielewi wanajeshi wanafanya kazi gani.

Hawawezi kuwa wanafanya mazoezi ya vita siku zote.
Marekani ndio wanafanya hivyo mkuu?
 
We unapendekeza yafanye nini?
Wafanye tafiti za kisayansi ambazo zinasaidia kwenye Ugunduzi Mpya na Uundaji wa Silaha zetu wenyewe hapa hapa Tanzania.
Waanzishe Viwanda Vipya vya Kutengeneza na Kuunda Silha za Kisasa kwa ajili ya shughuli za Ulinzi na Usalama, sambamba za Silaha na Mifumo ya Kupigania Vita.
Mathalani, wangeanzisha Kiwanda Cha Kutengeneza Ndege zisizo na Rubani (Drones).
 
Back
Top Bottom