Meja Jenerali Charles Mbuge amestaafu na kuagwa jeshini baada ya kulitumikia jeshi kwa miaka 38.
Enzi ya utumishi wake jeshini, aliwahi kuwa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Mkoa na baadae kushika majukumu mbalimbali ya kijeshi.
Anakumbukwa jinsi alivyokuwa kipenzi cha Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.
Ni katika awamu ya tano, ambapo Meja Jenerali Mbuge aliibuka baada ya kazi nzuri ya ujenzi wa ukuta wa Mirerena na kupanda vyeo mfululizo hali iliyoibua minong’ono kwa wengi kuwa alikuwa anaandaliwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi.
Tunakutakia maisha mema ya kustaafu, utumishi wako jeshini umetukuka!
View attachment 3063607
Soma pia:
Kwanini Rais Samia alimuondoa Meja Jenerali Mbuge kama Mkuu wa JKT?