Meja Jenerali Charles Mbuge astaafu utumishi wake jeshini

Meja Jenerali Charles Mbuge astaafu utumishi wake jeshini

Meja Jenerali Charles Mbuge amestaafu na kuagwa jeshini baada ya kulitumikia jeshi kwa miaka 38.

Enzi ya utumishi wake jeshini, aliwahi kuwa Mkuu wa JKT, Mkuu wa Mkoa na baadae kushika majukumu mbalimbali ya kijeshi.

Anakumbukwa jinsi alivyokuwa kipenzi cha Rais wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli.

Ni katika awamu ya tano, ambapo Meja Jenerali Mbuge aliibuka baada ya kazi nzuri ya ujenzi wa ukuta wa Mirerena na kupanda vyeo mfululizo hali iliyoibua minong’ono kwa wengi kuwa alikuwa anaandaliwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi.

Tunakutakia maisha mema ya kustaafu, utumishi wako jeshini umetukuka!

View attachment 3063607

Soma pia: Kwanini Rais Samia alimuondoa Meja Jenerali Mbuge kama Mkuu wa JKT?
Akakutane na kikokotoo, kimkokotoe vzr
 
Wafanye tafiti za kisayansi ambazo zinasaidia kwenye Ugunduzi Mpya na Uundaji wa Silaha zetu wenyewe hapa hapa Tanzania.
Waanzishe Viwanda Vipya vya Kutengeneza na Kuunda Silha za Kisasa kwa ajili ya shughuli za Ulinzi na Usalama, sambamba za Silaha na Mifumo ya Kupigania Vita.
Mathalani, wangeanzisha Kiwanda Cha Kutengeneza Ndege zisizo na Rubani (Drones).
Hyo pesa unayo? Acha kujitekenya basiii
 
Sasa mbona tunawaona sehemu nyingi mbali na mipaka?

Wajikite zaidi kwenye shughuli za kiuchumi, watumike kujenga zaidi, watumike kwenye engineering projects zaidi.

Sasa hivi ukiondoa hizo habari nikizozitaja hapo juu, ambazo haziwezi kuchujua vikosi vingi sana, sielewi wanajeshi wanafanya kazi gani.

Hawawezi kuwa wanafanya mazoezi ya vita siku zote.
Wanakaa chini ya miembe kupiga stori na kuwatisha raia na kombati zao
 
Kila la heri kwenye maisha yake ya Kustaafu

Ni jambo la kushukuru Mungu kufikia umri huo wa kustaafu.

Wengi huishia njiani Kwa sababu mbalimbali ikiwemo Mauti.
 
Yani ndiyo umepata vocha baada ya wiki au vipi?

Sikukujibu au sikukujibu ulivyotaka wewe?

Kwa nini swali kiwe Marekani ikiwa Marekani na Tanzania hazipo sawa?

Unalinganisha vipi vitu ambavyo havilinganishiki?
Mkuu umeulizwa marekani wanafanya jibu ni yes au no.
 
Pongezi na kwaheri.

Kwa sasa Jenerali anaweza kuwa kafanya kazi jeshini miaka 35 na hajapigana vita ya Tanzania.

Ukiondoa missions za kimataifa na shughuli za kujenga taifa za jeshi kama ufundi na kilimo, na ulinzi wa mipaka, majeshi yetu yanafanya nini hasa?
Sijategemea nisome comment hii kutoka kwako? Au kuna mjinga amehack simu yako
 
Mkuu umeulizwa marekani wanafanya jibu ni yes au no.
Hapana,

I reject the premise that America is valid in this conversation.

Hunipangii jinsi ya kujibu.

Unaweza kuuliza sauti yangu ina rangi gani, na kukawa hakuna jibu la yes or no.

Jibu la yes or no hata kama lipo, inawezekana lisiwe na maana kwa sababu Marekani si kipimo, na Marekani ni tofauti sana na sisi, na Marekani si mfano mzuri wa kuiga, sasa kwa nini uchague Marekani?
 
Back
Top Bottom