T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Umeanza kwa kudhihaki mstaafu kutumia miaka 35 jeshini bila kwenda vitani. Nimekujibu kazi kubwa ya jeshi ni kuepusha vita through deterrence. Hauamui tu upigane vita ili uonekane una Airforce au Navy au Army nzuri, unapigana ukilazimika tu.Sasa hapo Tanzania mtu akitaka kukutwanga mvua ya mabomu hao wanajeshi wasio hata na air force ya kueleweka wanazuiaje?
Kama deterrence haifanyi kazi vita ungeona haijalishi kuna Airforce ya maana au hakuna. Israel ina Airforce kubwa yet inakuwa vitani mara kwa mara. China ina Airforce kubwa na haijaenda vitani miaka zaidi ya 50.
Afrika ndio bara lenye vita zaidi sasa sijui idea ya kusema hakuna vita kisa umaskini unaitoa wapi.Usichanganye Africa kutokuwa na vita kwa sababu kila mtu anapambana na umasikini wake na ufanisi wa wanajeshi wetu.
Sudan, Ethiopia, Somalia, Libya, DRC zina vita ya miaka. Uko Western Africa kuna vita active dhidi ya ugaidi kwa Chad, Niger, na Mali.
China ni nchi ya pili kiuchumi duniani na haina vita wala haijashiriki kwa miaka zaidi ya 50.Vita ni biashara yenye gharama kubwa ambayo nchi nyingi masikini za Africa haziwezi ku afford.
Switzerland mara ya mwisho kushiriki vita ni 1847 hadi leo wakati silaha za kisasa wanazo na wanatengeneza na kuuza.
Nchi maskini kama Myanmar na Congo DR zimepigana miaka nenda rudi na zina njaa.