Ma Jenerali wengi bila vita ni u jenerali wa mchezo tu. Nchi yenyewe uchumi mdogo, ma jenerali wengi wa nini?
Rwanda pale ilipo ina four star Generals wanne na iko nchi eneo dogo. Tanzania tuna four star General mmoja, Lt. Gen. mmoja, Major Gen. na Brig. Gen. wachache. Huo wingi unaulinganisha na nchi gani maskini kama sisi, au ulitaka wawe wangapi ndio wasiwe wengi?
Unatetea vipi wingi wa Ma Jenerali katika nchi masikini ambayo hata haiweki wazi military spending yake?
China haiweki wazi military spending yake, nayo ina Majenerali wachache?
Hao majenerali wengi ni wangapi na unashauri wawe wangapi kwa vigezo vipi. Mbuge alikuwa mkuu wa JKT, JKT ni mojawapo ya kamandi 6 za jeshi. Taja nchi ambayo mojawapo ya kamandi zake kuu haiongozwi na at least Brigadier General au relevant rank.
Kwahiyo unataka Army, Naval Wing, Defence HQ, jeshi la akiba viongozwe na nani kama sio at least Brigadier General. Nchi gani hiyo Luteni anaongoza Army au Reserve?
Deterrence una m deter nani (nation state) anataka kupigana vita na Tanzania sasa?
Deterrence kwa yeyote anayetaka kujaribu kuvuruga amani. Kwa kuwa humjui haimaanishi hayupo, na kwa kuwa humjui hiyo ni mojawapo ya mafanikio ya jeshi nchi kutokuwa na adui. Au wewe ndio nyinyi mnaolipa bima ya afya alafu mnatamani kuumwa magonjwa makubwa ili malipo yenu ya bima yasiende bure.
Mojawapo ya kazi ya jeshi ni kufanya mazoezi kujipanga na vita ikitokea, sio kulazimisha vita itokee ili jeshi lionekane lipo.
Mkuu wa majeshi kalalamika watu wasio Watanzania wameshika nafasi nyeti serikalini, maana yake wanausalama na wanajeshi wameshindwa kulinda nafasi za serikalini zisishikwe na watu wasioeleweka, let alone ku deter vita.
Sio kazi ya JWTZ kudhibiti waajiriwa serikalini. Kuna mamlaka za uhamiaji na mamlaka za ajira. Soma majukumu ya JWTZ uelewe.
Unahakikishaje hatupigani vuta kwa sababu ya deterence na si kwa sababu hakuna anayetaka kupigana vita na sisi tu?
Kwa sababu jeshi lina deter na adui hatokei, hivyo likefanikiwa. Ukiwa na headache ukatumia painkillers na ukapata nafuu, unaanzaje kusingizia kuwa kichwa kimeacha chenyewe kuumwa wakati umetumia jitihada za kukiponya.
Unahakikishaje hatupigani vita kwa sababu hakuna anayetaka kupigana na sisi na si kwamba hakuna anayekuja kutuvamia sababu ya deterrence?