Meja Jenerali wa Kirusi auawa huko Ukraine

Meja Jenerali wa Kirusi auawa huko Ukraine

Unakuaje chambo kwa mfano? Ni jambo gani ukilifanya unahesabika umekubali kuwa chambo??
Unapokubali kutumiwa kumchokoza jirani yako kwa manufaa ya hao wanaokusukuma ufanye hivyo, unakuwa ni chambo.
 
Najua huyajui ndio maana najaribu kupanua ufahamu wako.
kama unajua siyajui, mizungusho ni ya nini sasa! Si mwaga tu hapa tukusome, tukubaliane nawe au tukatae.
 
Angalia na kusikiliza taarifa za habari kutoka vyombo vya kimataifa na siyo kuishia kuangalia Clouds!
ma-CCM mengi hata hiyo Clouds hayaisikilizi! Yenyewe hilizika na kuangalia Matangazo ya TIBISI tu.
 
Je kati ya Ukraine na Urusi nani aliyemvamia mwenzake nakuanzisha vita vya kichokozi?
Urusi haikuamka tu siku moja toka usingizini na kuamua kuvamia Ukraine bila ya sababu yoyote. Hili ndilo unalotakiwa kulifahamu.
 
Akirudi nyumbani Urusi atalazimishwa ailipe fidia UKRAINE kwa uharibifu na Putin atapelekwa the Hague kwa mauaji ya waukraine wasio na hatia
Duuuuuuh. Hiii vita Putin angetumia akili ilikuwa ni vita ya kushinda siku Moja tuuu kama angetumia akili kama ifuatavyo;

Kwanza waukraine na warusi ni wamoja kabisaaa. Kwahiyo jamaa angejitaidi kupanda mapandikizi yake jeshi lote la Ukraine, zaidi kabisa hata raisi wa Ukraine angejitaidi akapandikiza raisi atokanaye na yeye, ndioo Sasa angelianzisha kama lakuvamia wale wanajeshi wote WA Ukraine wangejifanya kusurender na raisi wao kumbe ni mpango uliosukwa mda mrefuu. Sasa yeye jamaa katumia mabavu ambapo ni vigumu kuwamaliza waliowamojaa. Kwakweli jamaa aliboronga pakubwaa.
 
Sasa waulize kinachowazuia ni kitu gani kwenda kummaliza huyo mRusi moja kwa moja, na badala yake wanamtumia chambo wao Ukraine kufanya kazi ambayo wao wangeimaliza harakaharaka na kuondoa tatizo.
Kwamba na Nchi za NATO nazo zifanye Uvamizi dhidi ya Urusi? Mbona ushabiki wenu kwa Dictator Putin unatukera sana? NATO inatumia kanuni ya kuutolea mwiba pale pale ulipoingilia.
 
Urusi haikuamka tu siku moja toka usingizini na kuamua kuvamia Ukraine bila ya sababu yoyote. Hili ndilo unalotakiwa kulifahamu.
Putin amezivamia na kubadiri viongozi wa nchi kadhaa zilizokuwa kwenye Soviet union ya zamani kwa lengo la kuirudisha Soviet Union. Sasa kwa kujazwa Propaganda haya huwezi kuyajua. Ukraine ilianza kuvamiwa na Urusi tangu 2014 ambapo walifanikiwa kuipora Cremia na kuanza kuwafadhili waasi wa makundi ya Majimbo matatu yaliyo tangaza kujitenga na Ukraine. Sasa Akili za Ukraine kuwa chambo ya nchi za NATO nyie mnaikuta wapi?
 
Kwamba NATO haina Mandege? Akili yako ina uwezo wa Kushangilia uuzwaji wa Bandari za Tanganyika? Hivi US na Mandege yake ilijitoa lini kwenye shirika la NATO?
Sasa kwa kauli yako mwenyewe hayo madege ni ya NATO au US? Hi dunia kweli ni mviringo 🤓
 
Kwamba na Nchi za NATO nazo zifanye Uvamizi dhidi ya Urusi? Mbona ushabiki wenu kwa Dictator Putin unatukera sana? NATO inatumia kanuni ya kuutolea mwiba pale pale ulipoingilia.
"...unawakera" wewe na nani?
Hicho kinachowazuia NATO kumvamia Urusi ni kitu gani?
Hujawahi kusikia NATO wakishirikiana kwenda kuwapiga mJahidin wa Afghanistan? Walikuwa na maslahi gani huko?
Nisisahau: usije na moto sana hapa, tutauziama tu.
 
Kwamba NATO haina Mandege? Akili yako ina uwezo wa Kushangilia uuzwaji wa Bandari za Tanganyika? Hivi US na Mandege yake ilijitoa lini kwenye shirika la NATO?
🤓 Kwahiyo ayo madege ni ya NATO au US?
 
Putin amezivamia na kubadiri viongozi wa nchi kadhaa zilizokuwa kwenye Soviet union ya zamani kwa lengo la kuirudisha Soviet Union. Sasa kwa kujazwa Propaganda haya huwezi kuyajua. Ukraine ilianza kuvamiwa na Urusi tangu 2014 ambapo walifanikiwa kuipora Cremia na kuanza kuwafadhili waasi wa makundi ya Majimbo matatu yaliyo tangaza kujitenga na Ukraine. Sasa Akili za Ukraine kuwa chambo ya nchi za NATO nyie mnaikuta wapi?
Mimi nilishwe 'propaganda', halafu wewe ndiye uwe nani? Putin atairudisha vipi Soviet Union kama huko siyo kukosa akili moja kwa moja?
Inaelekea hata kulikoanzia kuvunjika kwa Soviet Union hukujui, na makaubaliano yaliyofikiwa wakati huo, ambayo hao hao NATO ndio wanayoyavunja makubaliano hayo hujui?
 
Warusi za Buza watakwambia hii habari ni fegi ..
Hiyo inaitwa "Kalale peponi kamanda...."
 
Kbs huyo mwehu , hajui anajidharirisha kujifanya hajui lolote
ma-CCM yanamshabikia sana Dictator Putin kwa sababu ndiye Rais mwenye kuziunga mkono serikali zenye kuingia Mdarakani kwa chaguzi wizi wa Kura.
 
Mimi nilishwe 'propaganda', halafu wewe ndiye uwe nani? Putin atairudisha vipi Soviet Union kama huko siyo kukosa akili moja kwa moja?
Inaelekea hata kulikoanzia kuvunjika kwa Soviet Union hukujui, na makaubaliano yaliyofikiwa wakati huo, ambayo hao hao NATO ndio wanayoyavunja makubaliano hayo hujui?
Sasa kwa akili yako unafikiri lengo la Dictator Putin kuzivamia nchi zilizokuwa kwenye Soviet union zamani ni nini? Putin kuzivamia Ukraine na kupora Cremia ni nini? Putin kuvuruga Uchaguzi wa Belarus na kumuweka madarakani Lukashenko?

Kwamba wewe hujui kuwa US ilifanikiwa kumtumutumia Rais wa Mwisho wa Soviet Union The late Gorbachov kuisambalatisha Soviet Union, jambo ambalo Putin hakubaliani nalo ndo maana hata kwenye Msiba wa Gorbachov Putin hakuhuziria?
 
Sasa kwa kauli yako mwenyewe hayo madege ni ya NATO au US? Hi dunia kweli ni mviringo 🤓
Ndo maana kuna swali la kujiuliza kwa mtu yeyote mwenye akili timamu: US imejiondoa lini kwenye shirika la NATO?
 
Kwamba wewe hujui kuwa US ilifanikiwa kumtumutumia Rais wa Mwisho wa Soviet Union The late Gorbachov kuisambalatisha Soviet Union, jambo ambalo Putin hakubaliani nalo ndo maana hata kwenye Msiba wa Gorbachov Putin hakuhuziria?
Sasa angalia ujha huu hapa. Wewe hapa unanifundisha kitu gani, na kumbe unaingia kule kule nilikokufundisha hapo juu?
Hukuona Gorbachef alivyokufa kifo cha aibu sana, kana kwamba hatambuliki kabisa kuwa aliwahi kuongoza nchi? Hujui hata kabla ya kifo chake yeye mwenyewe alishakiri kuingizwa chakani na hao unaodhani ni wajanja sana?
Putin, na warusi wameyakataa hayo, ndiyo maana wakachora mstari wasichezewe tena.
 
Back
Top Bottom