Meli ya Iran yachanganyikiwa na kufyatulia nyingine makombora na kuua wanajeshi 19 wa Iran

Meli ya Iran yachanganyikiwa na kufyatulia nyingine makombora na kuua wanajeshi 19 wa Iran

Jamaa huwa siwaelewi moja ya sifa kubwa ya Jeshi imara ni usahihi wa vitendo (Practical accuracy) sasa wao mara wadungue ndege yenye abiria, mara wanajichanganya wanamweka hatarini Generali wao Souleiman anauwawa kizembe zembe leo tena wanajilipua wenyewe. SASA hawa kwa huo Uoga walionao wakisikia midege ile ya US inaelekea kwao si watakufa wenyewe ?? Au watasema ni Friendly Fire?
 
Ajari kama ajari nyingine tu. Hata friendly fire zinakuwepo majeshini. Kwa waliozoea mambo ya jeshi si kitu cha ajabu hata.
Kwenye Gulf war mwaka 1991 friendly fire iliua 25% ya waliokufa vitani. Na military drills zinaletaga vifo, ndio kama hivi sasa.
 
The Indo-European languages are a large language family native to western Eurasia. It comprises most of the languages of Europe together with those of the northern Indian Subcontinent and the Iranian Plateau. A few of these languages, such as English, have expanded through colonialism in the modern period and are now spoken across all continents. The Indo-European family is divided into several branches or sub-families, the largest of which are the Indo-Iranian, Germanic, Romance, and Balto-Slavic groups. The most populous individual languages within them are Spanish, English, Hindustani (Hindi/Urdu), Portuguese, Bengali, Punjabi, and Russian, each with over 100 million speakers. German, French, Marathi, Italian, and Persian have more than 50 million each. In total, 46% of the world's population (3.2 billion) speaks an Indo-European
 
Wanamaji 19 wameuawa na wengine 15 wakajeruhiwa katika tukio la ajali lililohusisha meli za kijeshi za Iran katika Ghuba ya Oman, jeshi la Iran limesema.

Vyombo vya habari vya Iran vimesema kwamba meli hiyo kwa jina Konarak ilishambuliwa na kombora jipya lililokuwa likijaribiwa na meli ya kijeshi ya Frigate Jamaran wakati wa zoezi la kijeshi siku ya Jumapili.

The Konarak ilishambuliwa na kombpora jipya Jumapili mchana wakati wa zoezi la kijeshi katika maji ya Bandar-e Jask kusini mwa pwani kulingana na runinga ya taifa katika tovuti yake.

Wanamaji hao walisema kwamba meli hiyo ilivutwa hadi ufukweni na kwamba uchunguzi umeanza.

Kisa hicho kilitokea karibu na mkondo wa bahari ya hormuz , eneo muhimu la kimkakati ambapo kiwango kikubwa cha mafuta duniani hupitia.

Uchanganuzi wa mwandishi wa BBC Jonathan Marcus

Sio mara ya kwanza kwa jeshi la Iran kufanya makosa hayo.

Mwezi Januari , kitengo cha ulinzi wa angani kilirusha kumbora kutoka ardhini kikilenga kitu kisichojulikana, hatua ilioangusha ndege ya kampuni ya Ukrain na kuwaua wote waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.

Makosa hayo yalifanyika wakati wa hali ya wasiwasi huku Iran ikisubiri kombora la kulipiza kisasi kutoka kwa Marekani.

Lakini tukio hilo la siku ya Jumapili lilifanyika katika hali tofauti - wakati wa zoezi la wanamaji - na linaibua maswali mengi kuhusu uongozi na udhibiti na utaalam wa jeshi la wanamaji wa Iran.

Iran inataka kupanua operesheni zake na kuimarisha silaha katika meli zake, Frigate Jamaran ambayo ni miongoni mwa vyombo vilivyoundwa nchini humo ikitarajiwa kuweka rekodi mpya.

Lakini ni jeshi lisililotiliwa maanani . Ni jeshi la wanamaji wa Revolutionary Guard lenye boti zinazopiga doria katika eneo hilo ambalo linahusika mara kwa mara katika kuhangaisha na kuchunguza meli za Marekani na nyenginezo katika Ghuba hilo.

"Siku ya Jumapili jioni...wakati wa zoezi la wanamaji ambalo lilihusisha vyombo kadhaa vya wanamaji katika maji ya Jask and Chabahar , tukio moja lilifanyika likihusisha meli ya Konarak , na kuwaua baadhi ya wanajeshi jasiri wa jeshi hilo, wanamaji hao walisema katika taarifa siku ya Jumatatu.

Taarifa hiyo iliongezea kwamba meli hiyo ya Konarak ilikuwa imepelekwa katika bara moja kwa uchunguzi wa kiufundi, lakini haikutaja tukio la ajali hiyo.

Vyombo vya habari vya Iran awali vilikuwa vimeripoti kwamba meli ya Konarak ilishambuliwa kwa bahati mbaya na kombora moja lililifyatuliwa kutoka katika meli.

Meli hiyo ilishambuliwa baada ya kupita katika eneo ambalo kombora hilo lilikuwa likirushwa baada ya kushindwa kupita mbali, runinga ya serikali ilisema katika tovuti yake.

Chombo cha habari cha Tasnim kilituma ujumbe wa twitter kwa kiingereza kwamba Konarak ilizamishwa katika tukio hilo.

Kiliripoti kwamba meli hiyo iliharibiwa vibaya. Haijulikani kulikuwa na wanamaji wangapi ndani yake wakati huo.

Meli ya kivita ya Konarak ina urefu wa mita 47 na ilitenegenezwa nchini Uholanzi na kununuliwa na Iran kabla ya mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

BBC Swahili
 
Hujielewi Kwanza umewaita waarabu pili unasema watoto wa Ishmael unazidi kupuyanga watoto Ishmael Ni waarabu

Sent using Jamii Forums mobile app
duuuhhh kwa hiyo watoto wa Ishamael ni wajapan?.

Ishamel ni Baba wa Waarabu ...

Hao wairan ni waajemi , ( origin yao sijui vzuri).

Gugo inaonyesha kuna wa Iran-wakurd ...wairan-waPersians.wairan-Azers .

Wewe wa elewa nini kuhusu wairan Mkuu?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani mleta hoja una tatizo na Iran sio bure. Meli ni chombo kimeundwa kwa chuma. Huongozwa na watu wala hakijiongozi chenyewe. Nnani aliye changanyikiwa kati ya meli na askari hao wa Iran??
 
Jamhuri ya kishia ya Iran ina nia ovu. Wacha wajipige wenyewe kwa wenyewe, ni laana imewasibu.
 
Back
Top Bottom