Meli ya New Victoria yawasili salama Bukoba baada ya ukarabati mkubwa

Hongera JPM aka chuma ila hili la kuongoza milele sikubaliani nalo tuandalie tu mwingine atakae tosho kwenye viatu vyako.
 
Kuna moja matata itakamilika mwakani.
 
Nategemea bei za bidhaa za vyakula kama ndizi,samaki na matunda kushuka.
Nikiwa narudi Mwanza my favourite food ntapata kwa bei rahisi(Ndizi samaki).
 
Tukiwa na huyu Rais ipo siku tutakua Taifa la kwanza Afrika kuwa na mfumo wake wa Elimu kuanzia Primary School mpaka chuo kikuu.
Hapo tutakua tumeishangaza dunia na kuwa na maendeleo ya kasi kama China na Irani.

Mfumo huu wa Elimu ni wa Kikoloni kwa manufaa yao na Mabeberu wa Ulaya na Asia.

Magufuli asipige hata kampeni uchaguzi ujao.
Apumzike zake. Atapata 74% - 88% akipumzika zake.
Akipiga kampeni atapata 94% lakini atajichosha tu bila sababu mana hata 51% zinamrudisha ikulu kujenga nchi na kuwafutilia mbali majizi na mafuska na matapeli na wamiliki wa Vyama vya siasa matapeli wanaojibinafsishia ruzuku za vyama na vyama kuwa NGO zao.
 
Mkuu ule ukarabati wa enzi za Mkapa ile pesa ililiwa na ungeambiwa mchanganuo wake hata wewe ungetoa chozi.


Najua wewe ni mfatiliaji wa mambo yanayojiri nchini, Mkurugenzi wa Marine Service alifunguliwa kesi baada ya Mh.Magufuli kuingia hiyo ni kutokana na matumizi mabaya ya pesa na kampuni ilifia mkononi mwake.

Kipindi cha Mkapa ela ya ukarabati ililiwa, mtu ananunua engine ya Catapiller na nyingine Cummins.Ela hiyo ya ukarabati watu waliwanunulia wake zao Range Rover.

Mkuu kwa kuanza na hizi meli Mv Victoria na ikija inayojengwa Mv Mwanza zitafanya kwenda na kurudi Bukoba-Mwanza.

Tatizo sio kuwa na meli nyingi hiyo shirika inafanya biashara lakini pesa ya ukarabati mpaka wapewe. Kikubwa mifumo ya kuongoza biashara ya kampuni iboreshwe.Raisi anatoa pesa meli zinakarabatiwa lakini baada ya miaka shirika linaomba pesa tena.
 
Dah Magufuli Nimtumishi wamungu alieletwa na Mungu kuiongoza Tanzania Yani ndani ya miaka mitano kafanya mambo makubwa sana ,Mungu endelea kumpa maono Raisi wetu..
 
Mambo kama haya hayana uvyama.kama kuna chama kitabeza jambo hili basi hicho chama hakiitakii mema nchi yetu.kwa hiyo tutakitilia shaka kubwa
 

Huu ukweli unakera lakini ndio ukweli wenyewe.
 

Mkuu sipingi usemacho, je unaonaje Mbao Fc, Ruvu JKT wakijitoa kwenye ligi kisa simba au yangu tu ndio wanaweza kubeba ubingwa? Mimi naona apate ushindani stahiki, lakini atakayeshindana naye aje na kitu mbadala, ili hata akipita ajue wananchi wanamtazamo gani. Ukiniambia kuwa kafanya sawa kwa 100% hapo utakuwa na hoja, kinyume na hapo, haya mapendekezo yako yatakuwa yanaoongozwa na chuki yako binafsi dhidi ya Mbowe.
 
Yap mbona inajengwa hapo mwanza inaitwa MV mwanza
 
Aise hizi neema za mnyaazmungu kwa utawala huu wa Magu.
Gharama zilizotumika kukarabati meli mbovu ya kale zingetumika kununua meli mpya ya kisasa, endeleeni kusifia ujinga wa awamu hii.
 
Haina maana akina mkapa walikuwa sio viongozi wazuri hapana Kila mtu na nyakati yake na jinsi hali aliyoikuta nchini, na magufuli hata afanye mazuri gani muda ukifika aondoke,watu ni wengi wenye akili na uwezo wa kuongoza......raisi wa milele sio kwa Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…