Meli ya thamani inateketea, wanamsaliti Nyerere

Meli ya thamani inateketea, wanamsaliti Nyerere

We lazima ni mbeba box katika nchi fulani hivi za wenzetu, siyo kwa akili kama hii tegemezi....Pole sana
Mbona hujiulizi kwa nini Afrika Kusini wametupita kimaendeleo wakati sisi tulitangulia kupata uhuru? Tena wao walitawaliwa na makaburu wabaguzi wa rangi, sisi tulikuwa chini ya malkia wa Uingereza?
 
Kwa hilo namtetea Nyerere. Hata tungekaa miaka 10 zaidi Waingereza hawakuwa na mpango wa kuendeleza chochote. Lawama kwa Mwalimu ni kutuachia Katiba ya Kifalme kwenye mfumo wa vyama vingi.
Rudia mfano wa Afrika Kusini. Kwa nini wana maendeleo kuliko sisi tuliopata uhuru zamani?
 
Rudia mfano wa Afrika Kusini. Kwa nini wana maendeleo kuliko sisi tuliopata uhuru zamani?
Ni kwa kuwa kaburu mzungu aliwekeza kwa kutumia akili kwa ajili ya watu wenye akili.

Wameachiwa nchi mwaka 1994 takriban miaka 27 kufika sasa tunachokiona ni uharibifu wa uchumi, chuki dhidi ya Waafrika wenzao, ulevi na zinaa, na uizi kama ule uliotokea mwaka huu baada ya Jacob Zuma kufungwa jela.
 
Wakumlaumu ni huyo huyo Nyerere. Alikuwa na kiherehere cha kuongoza kabla ya nchi kuwa tayari. Matatizo mnayoyaona sasa hivi ni matunda ya kujitawala kabla hatujawa tayari.
Ulitaka nchi iwe tayari baada ya kipindi gani labda?.
 
Nashangaa hadi sasa mleta mada hajajibiwa na ile hoja ya kijinga kwamba yeye binafsi kaifanyia nini Tanzania?🤪🤪
 
Nashangaa hadi sasa mleta mada hajajibiwa na ile hoja ya kijinga kwamba yeye binafsi kaifanyia nini Tanzania?🤪🤪
Hoja mfu sana hyo ambayo huwa inatumiwa na wanasiasa uchwara.
 
Ulitaka nchi iwe tayari baada ya kipindi gani labda?.
Hoja siyo mimi nilitaka lini tuwe tayari, hoja ni hatukuwa tayari. Ukiniuliza tungekuwa tayari mwaka 1970 au 1980 au 1990 siwezi kujibu hilo swali leo.
 
Haya ndio mawazo ya kizalendo, na sio mtu kujiita mzalendo kisa kapewa V8 ya umma. Kulitakiwa kujengwe viwanda ili vitoe ajira kwa vijana, na sio serikalini kujaa magari ya bei kubwa huku wananchi wanateseka kwa kukosa ajira.

Hatuna visionary leaders mana ukiwa Na vision ndo utapata hela, pesa haiji pasipo vision.
 
Wewe ni kichwa maji kweli halafu unajitia ujuaji! Gharama ya kuibadilisha gesi kuiweka kwenye mtungi si ndio huo mradi wa LNG ambao mwendazake alileta ubabe wawekezaji wakajitoa? Unaijua gharama yake? Mradi wa Trillionzaidi ya 50 tunazitoa wapi km makusanyo yetu ya mwaka ni 20T? Umeshirikisha ubongo au ndio kufanyia kazi kikundi chenu kinachowalipa?
 
Kwa ujinga wako, kaamua kukaa kimya mana busara kwake ni mhimu kuliko kubishana Na juha ka wewe
🤣 Division 1 O-level, Division 1 A-level, distinction degrees, successful career, successful businesses 🤣. Taratibu bro. Hunijui, sikujui.
 
Wewe ni kichwa maji kweli halafu unajitia ujuaji! Gharama ya kuibadilisha gesi kuiweka kwenye mtungi si ndio huo mradi wa LNG ambao mwendazake alileta ubabe wawekezaji wakajitoa? Unaijua gharama yake? Mradi wa Trillionzaidi ya 50 tunazitoa wapi km makusanyo yetu ya mwaka ni 20T? Umeshirikisha ubongo au ndio kufanyia kazi kikundi chenu kinachowalipa?
Hatari sana kwa watu wa aina hiyo.Ujinga na ujuaji uliopitiliza wa kishamba ndiyo uliotupilia mbali mradi wa gesi kwa chuki tu.
 
Muda Kawa nao tokea 2015 mpk sasa, kama ni kujifunza alipaswa awe kishafuzu vinginevyo ni kichwa maji hata mfanyeje kamwe sio wa kuelewa!
Baki na mawazo yako mgando kama ya wale wa zama za Mwinyi waliokuwa hawajui mzee Mwinyi anaitoa nchi katika umaskini na kuipeleka katika maisha bora.Walimponda sana Mwinyi,lakini wenye akili zao walitembea na falsafa yake na leo ndiyo matajiri tegemewa wa nchi hii.
 
Huko ndani hawataki kumpa muda wanasema ufisadi umezidi, na yeye anasema hajafanya ufisadi bali ni awamu zilizopita, sasa sijui awamu zilizopita yeye hakuwepo
Isome katiba juu ya nafasi ya maamuzi ya makamu Rais juu ya nchi ni yepi kisha ndiyo urudi kumjumlisha.
 
UNAPOTOA MAWAZO YENYE MAANA KWA NCHI KAMA HAYA HAWACHELEWI KUSEMA UMETUMWA NA MABEBERU KUMBE UZALENDO WAKO NDIO UNAKUTUMA UTAPIKE NYONGO YAKO!!!
Kuna nchi zimepata uhuru miaka ya 1980s lakini hazijanufaika na uchelewaji wa kupata uhuru. Maendeleo ya nchi yanahitaji vitu vingi siyo tarehe tu ya kupata uhuru.
 
Tatizo ni kuwa wenye mawazo kama haya ndiyo wengi wameshika hatamu...Hakika tunahitaji substitution ndiyo hapo na mimi nakubali sasa tuwe na katiba mpya...Bila hivi hawa matarishi watatuuza mazima mchana kweupe pasipokujitikisa kwakua wametufunga mikono na miguu kisha wanasema hatuwezi kujisaidia
"Tatizo ni kuwa wenye mawazo kama haya ndio wengi wameshika hatamu"
Nikiangalia uongozi tulionao ndani ya serikali, ninakubaliana na wewe moja kwa moja.
 
Hivi unafikiri kuna mtanzania mwenye elimu tosha kufanya hayo?
Hiyo elimu atakuwa kaipata wapi?
Hivi unafikiri kuna mzungu yupo tayari kutoa elimu yenye kukidhi mahitaji ya utafiti na ugunduzi kwa mwafrika?
Tuache kujidanganya kuwa tunawasomi sahihi wa kuyafanya haya kwa elimu nusu waliyopewa na hao hao wazungu.
Ni ajabu sana, kwa sababu wewe ni mtu wa pili kunipa jibu kama hili. Ninasikitika sana mkuu wangu, kwa jinsi tunavyojidharau na kujidhalilisha kiasi hiki.

Mkuu wangu, ngoja nikwambie ukweli, na utadhani sisemi kweli, lakini nakupa ukweli mtupu hapa. Mimi binafsi nina elimu ya juu kabisa katika eneo langu la kitaaluma katika sayansi, na nimefanya kazi sehemu mbalimbali duniani kwa miaka/miongo kadhaa. Nimefanya kazi katika mashirika/vyuo, n.k., na watu/wazungu hao unaowasema hapa.
Kwa hiyo ninao upeo mkubwa kabisa wa kusemea haya mambo, siyo kwa kubahatisha bali kwa uelewa.

Kwa bahati mbaya sana nchi yetu imekuwa kama tunarudi kinyumenyume badala ya kwenda mbele, na matokeo yake ndiyo matunda ya watu kama wewe hapo na mwenzako mkuu 'Stuxnet'. Badala ya taifa kuwa na watu ambao sasa wanajiamini kufanya mambo makubwa zaidi, badala yake elimu yetu inazalisha watu tegemezi kwa kila kitu katika maisha yao kama nyinyi. Na hii yote ni baada ya miaka 60 baada ya kujitawala wenyewe na kusema tunataka tuendeshe mambo yetu wenyewe!

Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom