Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Kalamu1 kama umesoma vizuri hadi elimu ya juu katika sayansi, kitu gani kinakufanya uendelee kuajiriwa huko kwa wazungu?Ni ajabu sana, kwa sababu wewe ni mtu wa pili kunipa jibu kama hili. Ninasikitika sana mkuu wangu, kwa jinsi tunavyojidharau na kujidhalilisha kiasi hiki.
Mkuu wangu, ngoja nikwambie ukweli, na utadhani sisemi kweli, lakini nakupa ukweli mtupu hapa. Mimi binafsi nina elimu ya juu kabisa katika eneo langu la kitaaluma katika sayansi, na nimefanya kazi sehemu mbalimbali duniani kwa miaka/miongo kadhaa. Nimefanya kazi katika mashirika/vyuo, n.k., na watu/wazungu hao unaowasema hapa.
Kwa hiyo ninao upeo mkubwa kabisa wa kusemea haya mambo, siyo kwa kubahatisha bali kwa uelewa.
Pili kwa kisomo chako ni mchango gani umetoa katika ugunduzi wa kisayansi ambao umeufanya na ukaonekana? Maana unaweza ukawa mpaka na PhD lakini kazi yako ni kukariri machapisho ya wazungu tu