Meli ya thamani inateketea, wanamsaliti Nyerere

Kalamu1 kama umesoma vizuri hadi elimu ya juu katika sayansi, kitu gani kinakufanya uendelee kuajiriwa huko kwa wazungu?

Pili kwa kisomo chako ni mchango gani umetoa katika ugunduzi wa kisayansi ambao umeufanya na ukaonekana? Maana unaweza ukawa mpaka na PhD lakini kazi yako ni kukariri machapisho ya wazungu tu
 
Kama sisi wananchi wenye tabu na mateso hatuna uchungu, raia tukachukua hatua, usitegemee hao kenge wanaokula keki ya taifa wawe na uchungu wakati wananeemeka. Huku kulia lia hatutusaidii, tumekaa kama mazozo.

"Mwenye shida hamjui mwnye njaa" hatma ya tanzania bora sio viongozi, ni NGUVU YA UMMA.
 
Mkuu!Naona bado haujajibu maswali niliyouliza.Na kwa kuthibitisha uozo wa elimu tuipatayo toka kwa wazungu,ni wewe mwenyewe kutoionesha elimu uliyonayo katika ubunifu na ugunduzi.Ebu rudi tena kwenye maswali yangu na uje na majibu sahihi.
 
Nilitegemea majibu kama haya toka kwako, kwa sababu naelewa wazi hujui taratibu za haya mambo. Kwani kila mzungu aligundua kitu?
Ngoja nikwambie, nimechangia vitu vya maana sana katika eneo langu na kwa hili najivunia sana.

Umejuwaje kuwa nimeajiriwa huko. Kwani nimesema bado niko huko nje?
Mwanzo nilidhani ni utani, lakini kumbe hizi ni fikra zilizoota ndani kabisa mwa waTanzania!

Kutojiamini ni jambo moja baya sana kwa raia wa nchi yoyote, na hii inatokana na hali ya mwenendo wa siasa wa nchi hiyo. Sasa CCM imetuduwaza sana kuliko wakati ule ilipokuwa inatupa matumaini ya kwamba uwezo tunao wa kufanya jambo tunalonuia kulifanya kwa mafanikio makubwa.

Mwalimu aliposema tunakwenda kumpiga Nduli, na kweli tulimtandika, na wala hapakuwepo na , eeehehee eheehe sijui tutafanyaje. Uwezo wetu ulikuwa mdogo, lakini tulishiriki kwa heshima kubwa katika ukombozi wa bara letu kuliko hata nchi zilizoonekana kuwa bora zaidi yetu.

Sasa kila kitu tunalia, hatuwezi kufanya, mpaka mzungu aje atufanyie?

Stuxnet, sijui background yako na elimu yako ikoje, lakini kutokana na haya unayoweka hapa, inakatisha tamaa sana.
 
Mkuu!Naona bado haujajibu maswali niliyouliza.Na kwa kuthibitisha uozo wa elimu tuipatayo toka kwa wazungu,ni wewe mwenyewe kutoionesha elimu uliyonayo katika ubunifu na ugunduzi.Ebu rudi tena kwenye maswali yangu na uje na majibu sahihi.
Maswali ni ya kipuuzi ndiyo maana siwezi kupoteza muda kujibu maswali kama hayo.
Hata hapa tulipofikia naona nimekupa heshima sana ya kuendeleza majibishano kwa upuuzi kama ule.
 
Sasa ume soma lakini haki iyo utaki mwenzako apate, uyo mjamzito ukisha mnyima elimu una mkomoa nani?
 
Maswali ni ya kipuuzi ndiyo maana siwezi kupoteza muda kujibu maswali kama hayo.
Hata hapa tulipofikia naona nimekupa heshima sana ya kuendeleza majibishano kwa upuuzi kama ule.
Tuliza mshono mkuu!Ubavu wako ni mdogo sana juu ya hoja zangu.
 
Sasa ume soma lakini haki iyo utaki mwenzako apate, uyo mjamzito ukisha mnyima elimu una mkomoa nani?
EeenHeeeeeeee, vipi mkuu, mimi na huyo "mjamzito" wapi na wapi? Sielewi hii unaitoa wapi mkuu wangu.

Kama unataka kujua ninasimamia wapi kuhusu jambo hilo, si bora uniulize tu moja kwa moja ili nieleze?
 
Kuna nchi zimepata uhuru miaka ya 1980s lakini hazijanufaika na uchelewaji wa kupata uhuru. Maendeleo ya nchi yanahitaji vitu vingi siyo tarehe tu ya kupata uhuru.
Kama unaongelea Zimbabwe, ile nchi ilikuwa na maendeleo ilipopata uhuru. Enzi zile Harare inaitwa Salisbury ukifika ni kama umefika Cape Town. Nchi iliporomoka pale Mugabe alivyoingia madarakani akisaidiwa na wanamapinduzi wenzake wakina Nyerere na Samora Machel. Na mpaka yule mzee alipong'atuka Zimbabwe ilikuwa ni failed state kabisa. Na Mugabe kama Nyerere alianza kuwa mwalimu na baadaye akageuka kuwa mleta mapinduzi bila ya kuwa na uzeofu wa kuongoza nchi akiachiwa aiongoze. Matokeo yake aliharibu nchi.
 
Hawatafika mbali kwa unafiki wao
 
Mugabe kamaM7 tu. Wote wahuni.
tofauti ndogo
 
Sawa hongera sana Kalamu1 kwa kuwa mtanzania msomi mwenye akili kubwa ya ugunduzi. Japo sijajua ulichogundua
 
Sawa hongera sana Kalamu1 kwa kuwa mtanzania msomi mwenye akili kubwa ya ugunduzi. Japo sijajua ulichogundua
Agundue nini na kwa elimu ipi?.
Mzungu hajawahi toa elimu kwa mwafrika anayetaka kuifanyia kazi Afrika.Mzungu akitoa elimu stahiki kwa mwafrika basi ni kwa ajili ya kumtumia wao wenyewe.
 
Haya ndio mawazo ya kizalendo, na sio mtu kujiita mzalendo kisa kapewa V8 ya umma. Kulitakiwa kujengwe viwanda ili vitoe ajira kwa vijana, na sio serikalini kujaa magari ya bei kubwa huku wananchi wanateseka kwa kukosa ajira.
Akili hii CCM hawajawahi kuwa nayo toka walipohalalisha ufisadi na rushwa😅!!!
Wao na familia zao hawako kwenye tabu yeyote ile😅 wanamenya tu
 
Tuna mali lkn hatuna teknolojia hyo ndyo laa a pekee inatutesa waafrika hata atawale nan tutaishia propaganda tu hakuna kinachoweza kubadilika bila mkono wa mzungu
 
Wabongo wanachoweza kuonesha achokidhindwa mwenzie jpm Kaa madarakani miaka mitano hajaweza kuibadilisha hyo gesi kwa matumizi ya nyumbani lkn ssh kakaa miezi nane wanamlaumu kwa kushindwa kujenga huo mradi na wafuasi wa jpm [emoji23][emoji1787]hii nchi kuendelea mpaka tufe sote ianze upya tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…