Sawa hongera sana
Kalamu1 kwa kuwa mtanzania msomi mwenye akili kubwa ya ugunduzi. Japo sijajua ulichogundua
Nadhani huelewi ninachokieleza mkuu Stuxnet, na pengine siyo kosa lako.
Tuachane na mchango nilioweka katika nyanja yangu ya kitaaluma, kwa sababu hiyo siyo hoja hata kidogo katika mjadala kati yangu na wewe.
Turudi kwenye yale uliyoandika wewe huko mwanzo, yaliyonisikitisha na kunisononesha moyo kujuwa kwamba hadi hii leo bado kuna waTanzania wenye aina ile ya mawazo?
Hapana, huenda unatania, ni kawaida ya watu kuja hapa JF na kujifurahisha tu kwa kuweka michango ya ajabu ajabu sana wakijuwa kwamba itaamsha mizozo. Hiyo ndiyo furaha yao.
Kiufupi nikuulize: Hivi Tanzania hatutaweza kuendelea bila sisi wenyewe kugundua vitu vyetu vya kipekee ambavyo itabidi ndivyo vituletee maendeleo?
Hivi hatuwezi kuwa na mahospitali mazuri yenye kutoa huduma nzuri kwa wananchi wetu bila ya sisi kugundua yote yanayohitajika kwenye mahospitali hayo?
Hivi wakulima wetu huko vijijini haiwezekani kabisa tukawasaidia wakawa na kilimo kinacholeta tija hadi tugundue mahitaji yote yanayotakiwa kuwasaidia katika kazi zao za kila siku?
Ninaweza kuendelea kukuuliza maswali ya namna hiyo hiyo katika nyanja zote na sekta zote tunazozitegemea kuzitumia kuiletea maendeleo nchi yetu.
Maana yako ni kwamba, maadam hatujagundua chochote, na pengine hatuwezi kutumia kilichogunduliwa na wengine (na siyo lazima wawe ni wazungu), basi hatutaweza kupata maendeleo?
Ngoja nimalize haraka kabla sijaandika gazeti hapa kwa haya yafuatayo.
Hapa tulipofikia sasa hivi kama waTanzania, kitu pekee tunachokosa ili tuweze kuibadilisha Tanzania ni uongozi tu; uongozi ambao hauna dira nchi yetu inapaswa kwenda wapi. Tunao wasomi wa kutosha kabisa ambao kama wanaweza kupangwa vyama na kupewa nyanja za kufanya kazi zao na mipango madhubuti ikawepo, hawa watu tulionao sasa hivi wanatosha kabisa kuleta mabadiliko makubwa sana katika kila nyanja.
Kwa bahati mbaya sana, hatuwatumii ipasavyo, kwa kuwanyima fursa ya kutumia elimu yao kuifaidisha nchi hii.
Leo hii watawala wakisema tunataka tuwatumie watu wetu (wataalam) tulionao na tusimamie kilimo chetu barabara, kilimo chetu kitakuwa ni tofauti na kilivyo sasa.
Leo hii serikali wakisema tunaweka mkakati wa kuwatumia wataalam wetu wa madawa tulio nao tuimarishe ujuzi wetu na uzalishaji katika eneo hilo, na kusimamia kazi hiyo, hali ya uzalishaji wa madawa nchini utakuwa ni tofauti kabisa na ilivyo sasa.
Na usije ukafikiri nahimiza serikali ifanye kila kitu, bila kushirikisha sekta binafsi, hapana; lakini huo ni mjadala mwingine. Kinachotakiwa ni serikali kuweka mikakati, na kuisimamia mipango inayohusika.
India, China, Korea (zote mbili), Vietnam, na nchi nyingi tu nyingine, wamelazimika kuwaleta wazungu na elimu yao kufanya waliyofanya walipoamua kufanya? India wakatengeneza bomu la nuclear, na sasa mambo mengi mengine.
Basi bhwanah, kama hatuelewani, hatuwezi tukaelewana hata nikiandika kitabu.
Nimetiririka tu, sikurudi nyuma kusahihisha. Kama utaona makosa ya kiuandishi, juwa sikusahihisha.