Tetesi: MELT group walikopa Billion 250 kutoka benki ya Maendeleo ya Africa Kwa kutumia Kiwanda Cha Musoma textile Mills?

Tetesi: MELT group walikopa Billion 250 kutoka benki ya Maendeleo ya Africa Kwa kutumia Kiwanda Cha Musoma textile Mills?

kipindi cha mabadilko kutoka ujamaa kwenda ubepari,wajanja wengi walitajirika kizembe sana wakishirikiana na watawala.Si ajabu miaka ijayo kukuta ndani ya makampuni ya bakhresa au mo kuna hisa za mzee mwinyi au kikwete.
Umemsahau na yule alisajili ANBEM akiwa ikulu....
Na Marehemu alivyouza nyumba za serikali kwa ndugu na mademu wake!
 
Mkuu, kama alikinunua si ni mali yake na anaweza kufanya anavyotaka?? Mfano, mimi nimenunua nyumba Mbagala ilhalia tayari nina nyumba Mbezi Beach. Sasa nikiamua kuchukua mkopo Bank kwa kuweka rehani nyumba ya Mbagala ili nipanue ile ya Mbezi, kosa langu lipo wapi?

CC: peno hasegawa
Na ndiyo maana nimempa sifa ya ujanja ujanja ambayo watu wengine hawana. Binafsi sina tatizo juu ya hicho kitu alichofanya.
 
Hii nchi ukiwa na ngozi ya rangi nyeupe na ukija na bilion yako moja tu unakuja kuvuna mabilioni ya kutosha kwa kigezo cha mwekezaji

Picha linaanza waziri wa mipango na uwekezaji ni kitila mkumbo mzee wa fursa.
 
Ndugu zangu wana Mara katika Utafiti wangu nimegundua kuwa Mo aka Metl group walikopa Billion 250 kutoka benki ya Maendeleo ya Africa Kwa kutumia Kiwanda Cha Musoma textile Mills,

Lengo la mkopo kupanua kiwanda hicho cha Musoma Textile lakini Fedha zile Mo walienda kujengea kiwanda Cha Mo energy Vingunguti,

Wanamara wote, Kwa Pamoja tuamke kulipigania hili Kwa sababu Wabunge wa Mkoa wa Mara wamekaa kimya,Mkuu wa mkoa amekaa kimya, Uongozi wa mkoa umekaa kimya miaka inaenda Kiwanda Cha Musoma hakijengwi Wala kuendelezwa,

NINAOMBA YAFUATAYO:

1: Nimtake Mo na Kampuni yake warudishe hicho Kiwanda mikononi mwa serikali Ili wawekezaji wengine wapewe kuendeleza,

2: MO ashitakiwe kama mhujunu uchumi Kwa sababu amefanya Financia loan diversion kisheria ni mhujumu uchumi

3: Nimtake Mo atekeleze lengo la mkopo ule au atulipe Watanzania Kwa kuchukua asset ya Watanzania na kuifanyia biashara kinyume na taratibu za serikali,

4: Ashitakiwe Kwa kuwakosesha wanaMara Ajira za moja Kwa moja zisizopungua 100,000 Kwa maana wakulima wangeuza pamba, serikali ingekusanya Kodi, Technolojia ingekuwa,na Mapato yangeongezeka Kwa asilimia 120 ndani ya mkoa wa Mara

4: Mkoa wa Mara tunalia Vyanzo vya Mapato kumbe Vyanzo Hivi vinahujumiwa na watu wachache.

5: Wananchi wote tuungane kuwapinga watu kama hawa Tanzania

6:. Mo aombe radhi na kutekeleza pendekezo namba 3 nililotaja hapo juu.

7: Serikali ya mkoa itoe tamko juu ya hili na kuwaomba wananchi Radhi Kwa kutokuwa makini na kutofuatilia uwekezaji wa namna hii

8: Mkopo huu umeingizwa kwenye Deni la Taifa kupitia Mikopo inayochukuliwa na sekta binafsi,Tanzania

B: Kama hayatafanyika hayo

1: Natoa siku 60 kuifikisha Kampuni hii Mahakamani ukiwa ni pamoja na kuwataarifu Benki ya Maendeleo juu ya default ya mkopo ya namna hii regardless unarejesha.

2: Serikali ianzishe uchunguzi wa hili suala kama haitafanya wananchi tutaishitaki serikali na Kampuni husika.

Ç: Naomba kuwasilisha hoja kujadiliwa Kwa upana na kupata maoni juu ya hili Kwa pamoja tupate maoni.

Wenu Mzalendo Mara

B.Marela
Unazunguamzia Bilioni 25 au 250?maana sioni hio MUTEX ikawa na hio Bei
 
Hujitambui, MUTEX ingekuwa na mitambo ya maana isingekufa
MUTEX, MWATEX, URAFIKI na viwanda vyote vilivyokuwa chini ya serikali ya kijamaa ya mwalimu Nyerere vilifuka, si kwa uchakavu wa mitambo, bali kwa kuendekeza siasa kazini pamoja na globalization/new world order. The USSR was coming to its demise and EU/NATO was taking over the throne.
 
Matapeli ifike mahala sisi kama watanzania tuanze kuwanyonga ndio waatacha kutuchezea chezea na hizi mali za umma- Wanyongwe bila huruma sio hizi dana dana za utapeli wa kukopa huku na huku na kutofanyia malengo ya mkopo. Munyongwe tu- china style
 
Ndio unajua leo..

Unamzungumzia MO aliechukua mkopo wa $800M , ( kwa mujibu wa Maguful)

Alivotekwa mlipiga kelele.. ila MO hayupo mwenyewe..

Kuna yule wa Morogoro anaetoa mabas kupeleka mwil kwenye mazishi

Kuna mfadhili wa wananchi, na nchi akahama.

Wahindi karibu wote wametoboa kwa namna hiyo..

Na hii ni kwa msaada mkubwa wa waswahili wenzenu.. kupenda vihela vidogo vidogo...

Nyie mnashauriwa mkalime kebeji.
Hawa wafanyabiashara wakubwa wa kiindi wapigaji sana wametafuna sana nchi hii
 
Back
Top Bottom