Tetesi: MELT group walikopa Billion 250 kutoka benki ya Maendeleo ya Africa Kwa kutumia Kiwanda Cha Musoma textile Mills?

Tetesi: MELT group walikopa Billion 250 kutoka benki ya Maendeleo ya Africa Kwa kutumia Kiwanda Cha Musoma textile Mills?

B 250 kiwanda cha Musoma
Hiyo ni hela aliyokopa sio thamani ya kiwanda, thamani ya kiwanda may be kinaweza kuwa tilioni moja kabisa, we kiwanda kinatoa ajira za moja Kwa moja laki moja unazani ni kiwanda cha kuzalisha uongo au vitenge tu?
 
We unajua kiwanda cha bilioni 1000? Kilikuwa kinazalisha KWA kiasi gani? Halafu unaposema ajira za moja kea moja laki moja ni walioko kiwandani au mpaka wakulima wa pamba unawahesabu?

Dangote anasema kiwanda chake Mtwara katumia dola 600 milioni

"Aidha, Kampuni hiyo imesema kuwa imechagua kuwekeza Tanzania katika ujenzi wa Kiwanda hicho na huduma za upakiaji na upakuaji mizigo katika eneo lenye ukubwa wa hekta 25 katika Kijiji cha Mgao, kilichoko karibu na kiwanda hicho, kwa gharama ya dola za Marekani milioni 600 kwa sababu ya sera nzuri za Serikali na mazingira mazuri na rafiki ya kufanyia biashara yaliyojengwa na Serikali ya Tanzania."

Source Michuzi blog
 
We unashangaa hiko, hujiulizi kwanini mashamba ya mikonge kule Tanga walihodhi makubwa halafu wanaweka miche miwili mitatu kuzuga ila huo mkopo unaochukuliwa hiyo Ardhi ni balaa, then wanaenda ku-finance viwanda vyao huko kwingine

Mzee Baba alipoanza kufuta leseni na kuchukua mashamba yasiyoendelezwa (maeneo mengi yalikuwa yanamilikiwa na serikali kupitia zile mashirika ambayo yalikufa ) na kupewa wananchi akaonekana ana chuki na matajiri, je hii ni kweli?

Yaani ni kama hivi, umechukua shamba la hekari 300 Tanga, unapanda mikonge au kingine etc Hekari 30, afu heka 270 zinabaki vichaka vya miba, unaenda kuchukulia mkopo benki mamilioni ya fedha then unaenda kujenga/ kuendeleza kiwanda huko Mwanza

Wakazi wa maeneo jirani na shamba, ajira hawapati maana shughuli hakuna, kibarua hakuna, kulisha mifugo hawaruhusiwi, ka-eneo ka kulima hawana lakini ardhi ipo tu inawaangalia.
Daah aisee huun urasimu sio kabisaaa...kumbe yale mashamba hati zake ndo zinatumika hivii duuh msala sanaa walahii...!! sasa mgeni akipewaa hayo mashamba alafu akikopa then hati ikafutwa BANK inafanyaje???? kwelii hili shamba la bibi mamaeee
 
Ndugu zangu wana Mara katika Utafiti wangu nimegundua kuwa Mo aka Metl group walikopa Billion 250 kutoka benki ya Maendeleo ya Africa Kwa kutumia Kiwanda Cha Musoma textile Mills,

Lengo la mkopo kupanua kiwanda hicho cha Musoma Textile lakini Fedha zile Mo walienda kujengea kiwanda Cha Mo energy Vingunguti,

Wanamara wote, Kwa Pamoja tuamke kulipigania hili Kwa sababu Wabunge wa Mkoa wa Mara wamekaa kimya,Mkuu wa mkoa amekaa kimya, Uongozi wa mkoa umekaa kimya miaka inaenda Kiwanda Cha Musoma hakijengwi Wala kuendelezwa,

NINAOMBA YAFUATAYO:

1: Nimtake Mo na Kampuni yake warudishe hicho Kiwanda mikononi mwa serikali Ili wawekezaji wengine wapewe kuendeleza,

2: MO ashitakiwe kama mhujunu uchumi Kwa sababu amefanya Financia loan diversion kisheria ni mhujumu uchumi

3: Nimtake Mo atekeleze lengo la mkopo ule au atulipe Watanzania Kwa kuchukua asset ya Watanzania na kuifanyia biashara kinyume na taratibu za serikali,

4: Ashitakiwe Kwa kuwakosesha wanaMara Ajira za moja Kwa moja zisizopungua 100,000 Kwa maana wakulima wangeuza pamba, serikali ingekusanya Kodi, Technolojia ingekuwa,na Mapato yangeongezeka Kwa asilimia 120 ndani ya mkoa wa Mara

4: Mkoa wa Mara tunalia Vyanzo vya Mapato kumbe Vyanzo Hivi vinahujumiwa na watu wachache.

5: Wananchi wote tuungane kuwapinga watu kama hawa Tanzania

6:. Mo aombe radhi na kutekeleza pendekezo namba 3 nililotaja hapo juu.

7: Serikali ya mkoa itoe tamko juu ya hili na kuwaomba wananchi Radhi Kwa kutokuwa makini na kutofuatilia uwekezaji wa namna hii

8: Mkopo huu umeingizwa kwenye Deni la Taifa kupitia Mikopo inayochukuliwa na sekta binafsi,Tanzania

B: Kama hayatafanyika hayo

1: Natoa siku 60 kuifikisha Kampuni hii Mahakamani ukiwa ni pamoja na kuwataarifu Benki ya Maendeleo juu ya default ya mkopo ya namna hii regardless unarejesha.

2: Serikali ianzishe uchunguzi wa hili suala kama haitafanya wananchi tutaishitaki serikali na Kampuni husika.

Ç: Naomba kuwasilisha hoja kujadiliwa Kwa upana na kupata maoni juu ya hili Kwa pamoja tupate maoni.

Wenu Mzalendo Mara

B.Marela
Mmh
 
Garama za mitambo na aina ya uwekezaji katika proposal yake aliyowapa Benk inaweza zidi ata hiyo
Kwa logic ya kawaida Mie nikija na kisimu changu cha elf50 kama dhamana ili nikope elf50 huwezi Nipa, sana Sana umenionea huruma utanipa elf15 so kama mo alikopea bilioni 250 basi hicho kiwanda kutakuwa na thamani ya tilioni moja.
 
Sijitambui??? Unajua kilichoiuwa Urafiki Textile?mitambo iliyosimikwa MUTEX miaka 40+ iliyopita bado ingalipo active na inafanya kazi huko ilipo??Mo pia anamiliki 21 st Century Textile(zamani Polyster) Morogoro na ndie anae zalisha Nguo za Jeshi la Tanzania na kwengineko. Technologia kila kukicha inabadilika.Kama ujui kitu usilete ujuaji na hasira zako za kipumbavu
Hujui kitu
 
We unashangaa hiko, hujiulizi kwanini mashamba ya mikonge kule Tanga walihodhi makubwa halafu wanaweka miche miwili mitatu kuzuga ila huo mkopo unaochukuliwa hiyo Ardhi ni balaa, then wanaenda ku-finance viwanda vyao huko kwingine

Mzee Baba alipoanza kufuta leseni na kuchukua mashamba yasiyoendelezwa (maeneo mengi yalikuwa yanamilikiwa na serikali kupitia zile mashirika ambayo yalikufa ) na kupewa wananchi akaonekana ana chuki na matajiri, je hii ni kweli?

Yaani ni kama hivi, umechukua shamba la hekari 300 Tanga, unapanda mikonge au kingine etc Hekari 30, afu heka 270 zinabaki vichaka vya miba, unaenda kuchukulia mkopo benki mamilioni ya fedha then unaenda kujenga/ kuendeleza kiwanda huko Mwanza

Wakazi wa maeneo jirani na shamba, ajira hawapati maana shughuli hakuna, kibarua hakuna, kulisha mifugo hawaruhusiwi, ka-eneo ka kulima hawana lakini ardhi ipo tu inawaangalia.
Sasa na wewe si uende ukanunue na ukachukue mikopo anzisha viwanda ajiri watu lipa kodi tena jitahidi viwanda vyako viuze nje ya Tanzania uingizie mapato Tanzania yetu ukifanya hivyo wewe ni mzalendo na raia bora ktk uchumi wa Tanzania kama huwezi wewe ni kama mimi tu tumeshindwa kufikiri na kutumia rasilimali za taifa ili kujiendeleza na kuliendeleza ila mnaleta maneno dhidi ya wale wanaojitahidi kujijenga na kulijenga kiuchumi siku zote raia masikini hutengeneza taifa masikini na raia wenye kipato husaidia kukuza pato la nchi siku zote itabakia kuwa hivyo, tuache kulalama fursa hizi ni za kila mtu zitumieni kulalama hakuondoi umasikini hapa kwetu ,sana sana raia matajiri walipa kodi vizuri ni nguzo imara ya kipato cha taifa tuamke. Ila raia wenye roho, akili,fikra na moyo wa kimasikini wataendelea kulifukarisha taifa lao.
 
:. Mo aombe radhi na kutekeleza pendekezo namba 3 nililotaja hapo juu.

Wananchi wote tuungane kuwapinga watu kama hawa Tanzania

Serikali ya mkoa itoe tamko juu ya hili na kuwaomba wananchi Radhi Kwa kutokuwa makini na kutofuatilia uwekezaji wa namna hii

Serikali ianzishe uchunguzi wa hili suala kama haitafanya wananchi tutaishitaki serikali na Kampuni husika.
I Second.
 
We unajua kiwanda cha bilioni 1000? Kilikuwa kinazalisha KWA kiasi gani? Halafu unaposema ajira za moja kea moja laki moja ni walioko kiwandani au mpaka wakulima wa pamba unawahesabu?

Dangote anasema kiwanda chake Mtwara katumia dola 600 milioni

"Aidha, Kampuni hiyo imesema kuwa imechagua kuwekeza Tanzania katika ujenzi wa Kiwanda hicho na huduma za upakiaji na upakuaji mizigo katika eneo lenye ukubwa wa hekta 25 katika Kijiji cha Mgao, kilichoko karibu na kiwanda hicho, kwa gharama ya dola za Marekani milioni 600 kwa sababu ya sera nzuri za Serikali na mazingira mazuri na rafiki ya kufanyia biashara yaliyojengwa na Serikali ya Tanzania."

Source Michuzi blog
Mie musoma hata sipahamu comments kulingana na contents za mleta Uzi, mo kakopea kiwanda bilioni 250 so obviously kiwanda kitakuwa na thamani zaidi ya bilioni 250 may be kinaweza kuwa tilioni moja, hivi bank yenye akili timamu unaleta dhamana ya thamani ya milioni mbili halafu ikupe mkopo wa milioni mbili? Ukisoma maelezo ya mleta kuhusu ajira kaeleza wazi kabisa ni ajira laki moja za moja Kwa moja yaani ni wafanyakazi kabisa pale kiwandani sio unaosema wewe hao sio wakulima watauza pamba mamantilie watauzia chakula wafanyakazi hapana hizo sio ajira za moja Kwa ni indirect, sasa Kwa logic ya kawaida kiwanda kinachoweza kuajiri wafanyakazi laki moja direct bila Shaka kitakuwa na thamani zaidi ya bilioni 250.
 
Miongoni mwa Mikoa masikini ni Mara ,japokua wana viwanda kama hicho cha nguo,nyama,maziwa,samaki,na rasimali nying kama dhahabu ,mbuga ya serengeti,Ziwa Victoria,ardhi yenye rutuba Kwa kilimo na Mifugo Mingi .mkoa umetoa viongoz wengi mashuhuri na waanzilishi wa taifa Hili kma vile Mwalimu nyerere,Jaj warioba,butiku ,wasira,Mkono,pro muhongo,na wasomi wengi tu , na wabunge Wao wengi wa ccm huwa wanakuwa mawaziri .makamanda wa jeshi la wananchi na polis, msuguri,Siro,wambura,nk ,wanasiasa wa upinzan Makini kama vile John heche,ester bulaya,Catherine ruge,ester matiku nk .

Tatzo huu mkoa watu wake hawapendi kwako wengi wamewekeza na Kujenga nje ya mkoa Wao Mfano wengi utakuta wamejenga mwanza nk . Ubinafsi na Roho mbaya za wana Mara ndo zimewachelewesha wana mara .
 
Bila ushahidi ni UONGO

MUTEX haikuwa na hiyo thamani, haina hiyo thamani, haitakuwa na hiyo thamani
Yawezekana isiewe na hiyo thamani kweli, lakini mleta hoja amesema kwamba Mo alivuta mtonyo kwa kigezo cha kufanya upanuzi wa kiwanda cha Mutex
 
Mkuu, kama alikinunua si ni mali yake na anaweza kufanya anavyotaka?? Mfano, mimi nimenunua nyumba Mbagala ilhalia tayari nina nyumba Mbezi Beach. Sasa nikiamua kuchukua mkopo Bank kwa kuweka rehani nyumba ya Mbagala ili nipanue ile ya Mbezi, kosa langu lipo wapi?

CC: peno hasegawa
Umesoma argument yake? Unachukuaje mkopo Kwa business plan A kisha unaenda kutekeleza plan B? Hujaelewa kuwa anakwambia huo ni uhujumi uchumi? Maana katika justification hizo ajira lazima ziliwekwa Kwa mfano etc
 
1. Hakuna ushahidi maneno matupu.
2. Umeandika kwa Chuki kuu.
3. Waliomkopesha hawajaona kuwa kiwanda hakiendelezwi? Au ni wajinga kwamba wanadanganyika kizembe hivyo.
4. Vipi unataka aendeleze kiwanda ili wana musoma Mfurahi afu ashindwe kulipa mkopo mumcheke?
Kama amewapa rushwa kwamfano? Si na hao waliotoa pesa watawajibishwa?
 
Back
Top Bottom