Uchaguzi 2020 Membe ahsante sana, karibu rasmi CHADEMA. Karibu utuvushe

Uchaguzi 2020 Membe ahsante sana, karibu rasmi CHADEMA. Karibu utuvushe

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Ile kiu ya wapinzani(wapinzani halisi) wa Tanzania kupata mkombozi wa kutuvusha hatimaye imefikia pazuri baada ya Membe kukaribishwa ndani ya chadema na hatimaye kusubiri kuwa mgombea wa urais.

CHADEMA katika siku ambayo mmefanya jambo la maana na umuhimu sana basi ni hii ya kumpa Membe nafasi ya kutuvusha 2020.

Membe ni mwanamkakati na mbobezi kwenye masuala yote ya intelijensia, hivyo ni mtu sahihi kabisa na muhimu kwa wakati huu kuliko wakati wowote ule.

Membe sio Lissu, Membe ana ushawishi, ana mtaji wa watu wengi sana kitu ambacho Lissu hana na kamati kuu imeona hili suala.
Karibu Membe chadema, karibu utupiganie, karibu utuvushe.

#2020 upinzani tunaenda na Membe#
 
Daah Tundu lissu ashatoka kwenye utukufu Tena Ila kwakwel inahitaji nguvu nyingi chadema kuwaelewa wanapenda Nini na hawapendi Nini ?

Na nilichogundua Watanzania huwa hatujifunzi kutokana na makosa tuliyoyafanya nyuma.

Yani mtu alipigwa risasi Zaid ya 16 akikipigania chama leo hii mmemuona Hana umuhimu tena kisa kachero mmoja aliefukuzwa uanachama ndani ya chama chake.

Dhambi ya usaliti itaendelea kuwatafuna Sana CHADEMA.
 
Mnaimbishana wenyewe mataga hapa.
 
Na kwahali hii itachukua miaka Mingi Sana CCM kuitoa madarakani,
Maana wanao onekana hawafai CCM(Makapi) ndo wanaonekana dhahabu upande wa pili..
Safari bado tunayo Tena siyo kidogo.
 
Back
Top Bottom