Uchaguzi 2020 Membe ameanza kukanyaga kwenye uwanja wa uchaguzi kwa mguu wake mbovu

MwanaPekee

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
382
Reaction score
385
Hivi karibuni Mwanasiasa BM amekuwa akitumia uwingi pale anapoeleza azma au nia yake kwa jamii. Mara kadhaa amesikika akitumia maneno kama vile Tutagombea, Tutachukua fomu, Tutashinda, nk.

Watu wengi na hasa wachambuzi wa mambo ya siasa wamekuwa wakijiuliza maana halisi ya matumizi hayo ya uwingi, na wengine kufikia hatua ya kusema kwamba huwenda analenga kuonesha kuwa anaendesha siasa jumuishi (inclusive politics).

Jana BM ametegua kindewawili hicho. Matumizi hayo ya uwingi yana yanaonesha UKABILA alionao Membe, kwani yeye mwenyewe kwa kinywa chake alisema Mabaraza ya Vyama anavyotaka kupeperusha bendera yao yanajadili suala la Rondo. Kauli hiyo inaonesha kuwa BM anaingia na gia ya Ukabila, na mara zote amekuwa akitumia wafuasi toka kwao Rondo. Amekuwa akiongea na wana-Rondo, Amewatumia wana-Rondo kucheza movie ya kurejesha kadi za CCM, katika ujumbe wa sauti mitandaoni akimtukana Rais JPM alikuwa akiongea na Katibu Kata ya Rondo n.k.

Siasa hizi za kiubaguzi hazitakiwi kupewa nafasi kwa sasa. Leo anakuja na ukabila, kesho atakuja na udini, ukanda, itikadi za kisiasa, n.k. Watanzania tuamke na tuseme "Hapana huko unakotaka kutupeleka siko."
 

Siongezi neno hapo...
 
Kwa ulicho kiandika apa..Huna kazi nyingine ya kufanya ?
 
Membe ndio tegemeo letu chadema
Hivi nani aliyewaloga? Mnafikiri bila tume huru ya uchaguzi mwaweza kushinda? Magufuli keshashinda kwa zaidi ya 80%.

Computer zao tayari zinasoma hivyo, wanangoja kusoma tu matokeo ya uraisi. Mpige kura msipige keshashinda. Si Membe wala Lissu. Mtakumbuka hili ninalosema mie Mshunami, mke wa mfalme Sulemani.
 

uchaguzi huru na haki upo. Self-evaluation ndo zinazowasumbua upinzani. Deeper inside wanajua kwamba they nothing to sell to voters.
 
Kada mwenzako huyo sema ameandika kinafiki tu hapo
 
Tanzania au Africa in general hakuna kiongozi ambae hawez kujali ukabila au udini au undugu, Africa iko hivyo

Wakati wa mkapa watu wa kusini walipata Sana vyeo, wakati wa kikwete watu wa pwani walikula Sana shavu so kwa Africa ni mambo ya kawaida Sana
 
Tume ni huru ndio maana tunashiriki kila chaguzi Kama sio huru tungekuwa tunashiriki vipi? Hii kusema sio huru Ni kujihami tu[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…