Hivi karibuni Mwanasiasa BM amekuwa akitumia uwingi pale anapoeleza azma au nia yake kwa jamii. Mara kadhaa amesikika akitumia maneno kama vile Tutagombea, Tutachukua fomu, Tutashinda, nk.
Watu wengi na hasa wachambuzi wa mambo ya siasa wamekuwa wakijiuliza maana halisi ya matumizi hayo ya uwingi, na wengine kufikia hatua ya kusema kwamba huwenda analenga kuonesha kuwa anaendesha siasa jumuishi (inclusive politics).
Jana BM ametegua kindewawili hicho. Matumizi hayo ya uwingi yana yanaonesha UKABILA alionao Membe, kwani yeye mwenyewe kwa kinywa chake alisema Mabaraza ya Vyama anavyotaka kupeperusha bendera yao yanajadili suala la Rondo. Kauli hiyo inaonesha kuwa BM anaingia na gia ya Ukabila, na mara zote amekuwa akitumia wafuasi toka kwao Rondo. Amekuwa akiongea na wana-Rondo, Amewatumia wana-Rondo kucheza movie ya kurejesha kadi za CCM, katika ujumbe wa sauti mitandaoni akimtukana Rais JPM alikuwa akiongea na Katibu Kata ya Rondo n.k.
Siasa hizi za kiubaguzi hazitakiwi kupewa nafasi kwa sasa. Leo anakuja na ukabila, kesho atakuja na udini, ukanda, itikadi za kisiasa, n.k. Watanzania tuamke na tuseme "Hapana huko unakotaka kutupeleka siko."