Ok, naona Membe ameamua kufunguka ila ajue wengine aliowasema bado wako hai, hapa naona vita ya maneno itaenda kuanza very soon huko CCM, na zaidi zile kelele za "hawa wa kanda hii" na "wale wa kanda ile" zitazidi kushika kasi na hili litakuwa kikwazo kwenye serikali ya Samia hasa baada ya Rais kusikika akisema hamtumbui mtu kutokana na kabila lake.
Membe anachofanya kwa kifupi ni kuonesha zamu yao ya kujidai imerudi, ndio maana juzi amesikika Mzee Makamba akisema Mungu halishwi ugali analishwa maombi na akayasikia, leo Membe anakuja na hili, Kinana nae aliwahi ku tweet siku za nyuma akionesha sasa mambo yao safi, na Makamba mdogo karudishwa serikalini, kwao ni mwendo wa kucheka cheka tu huku wakitudanganya wanatibu majeraha.
Katiba Mpya ndio suluhu yetu, ije kutuondoa kwenye haya makundi yanayojiona yana hati miliki ya kututawala, waroho wa madaraka wasioshiba, Membe alitaka kubebwa na Kikwete mambo yakagoma baada ya Lowassa kutemwa, ile vita ndio ikamzaa Magufuli, lakini japo alionekana "neutral" wakati ule, bahati mbaya nae akaja kutengeneza kundi lake.
Tuache kuishi kwa kutegemea fadhila za hawa walafi wanaojidai kutupenda, ni waongo na wanafiki wanaoyapenda zaidi matumbo yao.
Kumbe Membe alitaka kwenda kuwa KM Common wealth ili apate paundi bilion 7 wakati bado hajatuambia zile za Gaddaffi ilikuwaje. Basi Magufuli alimkataa kwasababu alizijua tabia zao hawa wapenda pesa, huu sio muda wao wa kutoka mafichoni na kuanza kupiga kelele kama wanavyodhani kwani bado ni wachafu kwa matendo waliyofanya siku za nyuma, Kinana pembe za ndovu....
Wacha niendelee kufuatilia kesi ya Mbowe naamini yule wanayelazimisha kumfunga mdomo ndie mwenye threat kwao, na wote kwa pamoja bila kujali makundi yao chamani huungana kumpiga vita ili waendelee kuitafuna nchi yetu kama ni mali ya baba yao, naamini iko siku taifa hili litaupata ukombozi wa kweli.