Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
Akihojiwa na idhaa ya kiswahili ya UJERUMANI aliyekuwa mwanaCCM MWENZETU mh. Benard Camillius Membe anatapatapa kwa kujinasibu kuwa na WENZAKE SITA. Akihofia kutowataja majina kwa kuogopa kutimuliwa ndani ya CCM mh. huyu asiyeridhika kwa yote mema na mapungufu aliyotufanyia watanzania akiwa mhudumu wetu pale foreign affairs ametamba kutaka kugombea URAIS kwa njia yoyote atakayoweza
Natoa rai kwa vijana wa ccm waelewe kuwa yale aliyoyaasisi baba wa taifa na yanayotekelezwa kiufasaha na mh.rais magufuli sasa yako msambweni kutoweka kwa kuwiwa na maadui wasioamini katika muktadha mpana wa kujiamulia mambo sisi wenyewe.
Mabeberu na makuwadi wao hawajalala na hawatoacha kutuandama kwa visingizio vya domokrasia,uwazi,tume huru na uliberali koko
Shime wananzengo tuilinde itikadi adhimu ya chama hiki cha wanyonge na kinachosimamia misingi ya uafrika wetu na kisichokubali kupiga magoti kwa mabeberu na makuwadi wao