View attachment 1488133View attachment 1488134
Kwa wakristo watanielewa kirahisi sana...
Bibblia Takatifu katika kitabu cha Nabii Isaya (ISAYA 29:13) inasema, nanakuu;
".....
Bwana akanena, KWA KUWA WATU HAWA HUNIKARIBIA NA KUNIHESHIMU KWA VINYWA VYAO, BALI MIOYO YAO WAMEFARAKANA NAMI , na kicho chao walicho nacho ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa....."
Hili ni andiko/mstari wa Neno la Mungu (Biblia) ni wa onyo na tahadhari kwa watu ama mtu yeyote "mnafiki" ambaye kimwili na kwa maneno ya kichwa chake anakubali kuwa mko pamoja katika misheni ama mipango fulani, lakini deep inside, NAFSI na MOYO wake viko kinyume na mbali kabisa na wewe....
Mara zote hali na mahusiano ya namna hii ya kinafiki, huwa haidumu sana na kamwe haizai matunda mema.....
Na siku kilichomo ndani ya mioyo ya watu hawa kikija kudhihirika wazi, mara zote hali huwa tete sana. Huwa pana kuwa na patashika nguo kuchanika kila mmoja akimkamata uchawi mwenzake bila kujua kuwa wao wote ni wachawi kwa tofauti ya viwango tu...!!
CCM ya sasa kwa kiwango kikubwa imebeba watu wa namna hii akiwemo mpaka M/kiti wao taifa ndugu John Pombe Magufuli...
Roho ya "unafiki" aliyonayo ndiyo inayoanbukiza na kuathiri wafuasi wake, wanachama wenzake na viongozi wenzake ndani ya chama hadi serikalini na inaathiri taifa zima hata wasiohusika..
Ndugu Bernard K. Membe ni mtu jasiri wa hali ya juu. Hamwogopi binadamu. Ameamua kuukataa unafiki. Kaamua kusimama upande ukweli. Mungu muumba yeye ndiye kweli. Kaamua kukiweka wazi kilichomo moyoni mwake kwa kinywa chake....
Tatizo moja kubwa la binadamu ni hili. Wengi tuna asili ya kuikataa NURU na kukumbatia GIZA kwa mikono yetu yote miwili bila hofu. Mtu yeyote asiye mkweli toka ndani ya NAFSI yake huyo ni wa GIZANI. Giza na Nuru kamwe havipatani....
Bernard K. Membe kwa ukweli wake, wana wa GIZANI wanamshambulia kwelikweli. Lakini hakika nawaambia, kwa Mungu huyu ndiye anayehesabiwa haki maana kinachotoka kupitia kinywa chake, ndicho kilichomo moyoni mwake. Maana yake anamkaribia Mungu kwa dhati na kwa vyote kama alivyo...!!