Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Mahakama kujihusisha kuamua kesi za madai zenye mlengo wa kisiasa kunaenda kuua demokrasia, uhuru wa kutoa habari na maoni na kunaenda kuziba watu midomo kuibua kashfa mbalimbali za uhujumu nchini kwa kuhofia kuamuriwa na mahakama kulipa fidia za bilioni 9!!!
Kwahiyo, wewe unaona Musiba aliibua kashfa gani? Au na wewe ni mwanamatusi mwingine?
 
Wakati dalali wa Mahakama kampuni ya Yono (vijana wa kazi) ikihesabu siku zilizobaki katika 14 (siku za kazi) alizolewa mtukanaji Cyprian Majura Musiba kumlipa fidia Kachero Bernard Membe jumla ya shilingi 9.2 Bilioni, Bwana Musiba amewaangukia viongozi wa dini Askofu Alex Malasusa (KKKT Diyosisi ya Pwani) na Kardinali Porlycarp Pengo kumwombea msamaha kwa Membe asipige mnada mali zake.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Membe nyumbani kwake Mikocheni zinaeleza kwamba Jumatatu ya tarehe 24/4/2023 majira ya saa 10 alasiri mjumbe kutoka kwa Pengo alifika kwa Membe kumpa ujumbe wa Pengo kumsihi amsamehe Musiba.

"Alikuja hapa padre wa moja ya makanisa yetu kuleta ujumbe huo lakini naona Mzee alimkatalia na kumwambia 'namheshimu sana baba Askofu Pengo lakini kwenye hili anisamehe yeye (Pengo) huyu kijana lazima alipe gharama ya matusi yake' " anasema mwanafamilia aliyetajwa kwa jina la Colleta na kuongeza:

"Lakini jioni yake ya saa moja Askofu Malasusa naye alimpigia simu Mzee kuongelea suala hilo hilo lakini naye Mzee alimpa majibu yale yale aliyompa mjumbe wa Pengo." Hata hivyo kwa maelezo ya Colleta ni kwamba si tu ni msimamo wa Mwanadiplomasia huyo Bali ni msimamo pia wa familia.

Hii inakuja baada ya jitihada za Askofu Mwamakula pia kugonga mwamba baada ya kumwandikia barua Membe ya msamaha kwa Musiba.

Wakati hayo yakijiri hapa Mikocheni, tayari kampuni ya Yono imeshatua jijini Dodoma itakapoanzia kazi ya mnada kwa kuanza na apartments za Musiba zilizoko Ihumwa, nyumba yake ya Chamwino, guest house yake ya Msalato na shamba la hekari 10 njia ya Singida.

Baada ya hapo Yono atatimba apartment ya Kigamboni, shamba la hekari 5 Bagamoyo kabla ya kugeukia mitambo yake ya uchapaji iliyoko jengo la Exim ghorofa ya 8 jirani na Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba huko nyuma Musiba alichapa magazeti yake kampuni ya Malindi Printing huko Mbweni ambayo ni mali ya TISS. Jambo hili lilileta ukakasi wa kisheria kwani sheria ya vyombo vya habari (2016) inamtaka mlalamikaji kumshitaki Mwandishi, mhariri, mchapaji na msambazaji. Kwa mantiki hiyo DG wa TISS angetakiwa kusimama kortini. Ili kuokoa jahazi Musiba "alinunuliwa" mitambo mingine Mpya kutoka Ujerumani na kwa "huruma" mwana TISS Membe aliridhia. Nayo itanadiwa baada ya siku 14 kutamatika pamoja na nyumba na mashamba yake ya kijijini nakadhalika.

My take: Vijana tujifunze kitu katika sakata hili la Musiba na Membe kwamba tuwe na akiba ya maneno. Lakini pia akili ya kupewa changanya na zako. Waliokuwa wakimpa akili karibia wote wamemkimbia tena ndio wamekuwa jirani na Membe. Amtegemeae mwanadamu mwisho huwa kama hivi. Musiba kwishney!
Hapo bado Tibaijuka 🤪🤪🤪
 
Viongozi wadini acheni kumbelembele.. wakati Membe anatukanwa mlikuwa wapi msimkemee Musiba? Ila wote mliufyata na kujifanya hamsikii
 
Msamaha ulitakiwa iombwe kabla ya hukumu ya kesi husika.
 
Kama alitegemea kutoboa kupitia hiyo njia Naona atakwama tu huyo musiba hana kitu.

Kufulia uzeeni kubaya sana kunamfanya mtu afanye mambo ya kumshushia hadhi kabisa.

Sasa kweli waziri wa mambo ya nje mstaafu ni mtu wa kungangania kuuza mali za Musiba??

Anajiabisha kuliko hata vile anavyodai kuaibishwa na musiba.
Unafikiri membe ni fala kama wewe
 
Mbona Musiba mwenyewe aombi msamaha ,inamaana hajutii alichokifanya ndio maana Membe anashangaa watu wapembeni wanamwombea msamaha wakati yeye muhusika wala hajali.
 
Halafu huyo ndio alitaka kuwa kiongozi wa nchi mwenye kinyongo cha kutu. Basi atakufa bila kusamehe na Mungu naye hatamsamehe kwa chochote hata kama akitubu kwa kutoa machozi ya damu.

Kuna sababu maalum Mungu amekusudia kwa Membe kuwa na kiburi cha umimi wa kibinadamu kwamba aabudiwe. Huyu inawezekana ndio alishiriki mchezo mchafu
Acha uzuzu wewe! Aliyetukana mwenyewe mnaemuombea msamaha, amegoma kuomba msamaha. Mnataka Membe amsamehe kwenye ground zipi?
 
Bado mabilioni ya Fatuma Karume.. Musiba mpaka awe mwehu mwaka huu. Na Fatuma ndo haingiliki na mashehe wala maaskofu
 
Membe ni failure anayetapatapa.

Aliwahadaa ACT wazalendo kwamba ataingia dakika ya 89 na kufunga goli alafu akaishia kufanya kampeni za urais kwenye kijiji cha Rondo
Yule Mzee ni msanii,ata hiyo hukumu imekaa kirushwa rushwa tu!
 
Tena Musiba akiwa analiburuza hilo li case na ma appeal pesa zita mwishia Membe
Na Musiba naye sijui vipi kwa nini hizo mali asiziandike kuwa ni za mtu mwingine?
Au kama inawezekana aende akaiombe Mahakama kuwa yeye anauwezo wa kumlipa Membe laki moja kila mwisho mwezi mpaka deni liishe.
 
Duh..., kama mwandishi huyu, ambaye mimi nilimuona kama ni mwandishi kilaza, kanjanja na kichaa kabisa Kichaa mmoja, anaweweseka sana juu ya Zitto, kamtungia uongo, umebuma, Zitto tuko nae hapa Dodoma, anamiliki mali kama hizo!, then huyu jamaa ni kichwa sana!. Ametuheshimisha sana, hivyo najiunga na Maaskofu, Membe amsamehe tuu!.

Kitendo cha Membe kutowatii maaskofu kitamgharimu sana!. Kuna kiongozi fulani aliwahi kuwadharau maaskofu, najua ni nini kilikuja kumtokea, hivyo sitaki Membe yamkute ya kumkuta!. Amsamehe tuu Musiba!.

P.
Acha kutishia watu..maaskofu sio Mungu. Wao wenyewe Wana scandal zao kibao. Kila siku wanatimuana
 
Back
Top Bottom