Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Wakati dalali wa Mahakama kampuni ya Yono (vijana wa kazi) ikihesabu siku zilizobaki katika 14 (siku za kazi) alizolewa mtukanaji Cyprian Majura Musiba kumlipa fidia Kachero Bernard Membe jumla ya shilingi 9.2 Bilioni, Bwana Musiba amewaangukia viongozi wa dini Askofu Alex Malasusa (KKKT Diyosisi ya Pwani) na Kardinali Porlycarp Pengo kumwombea msamaha kwa Membe asipige mnada mali zake.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Membe nyumbani kwake Mikocheni zinaeleza kwamba Jumatatu ya tarehe 24/4/2023 majira ya saa 10 alasiri mjumbe kutoka kwa Pengo alifika kwa Membe kumpa ujumbe wa Pengo kumsihi amsamehe Musiba.

"Alikuja hapa padre wa moja ya makanisa yetu kuleta ujumbe huo lakini naona Mzee alimkatalia na kumwambia 'namheshimu sana baba Askofu Pengo lakini kwenye hili anisamehe yeye (Pengo) huyu kijana lazima alipe gharama ya matusi yake' " anasema mwanafamilia aliyetajwa kwa jina la Colleta na kuongeza:

"Lakini jioni yake ya saa moja Askofu Malasusa naye alimpigia simu Mzee kuongelea suala hilo hilo lakini naye Mzee alimpa majibu yale yale aliyompa mjumbe wa Pengo." Hata hivyo kwa maelezo ya Colleta ni kwamba si tu ni msimamo wa Mwanadiplomasia huyo Bali ni msimamo pia wa familia.

Hii inakuja baada ya jitihada za Askofu Mwamakula pia kugonga mwamba baada ya kumwandikia barua Membe ya msamaha kwa Musiba.

Wakati hayo yakijiri hapa Mikocheni, tayari kampuni ya Yono imeshatua jijini Dodoma itakapoanzia kazi ya mnada kwa kuanza na apartments za Musiba zilizoko Ihumwa, nyumba yake ya Chamwino, guest house yake ya Msalato na shamba la hekari 10 njia ya Singida.

Baada ya hapo Yono atatimba apartment ya Kigamboni, shamba la hekari 5 Bagamoyo kabla ya kugeukia mitambo yake ya uchapaji iliyoko jengo la Exim ghorofa ya 8 jirani na Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba huko nyuma Musiba alichapa magazeti yake kampuni ya Malindi Printing huko Mbweni ambayo ni mali ya TISS. Jambo hili lilileta ukakasi wa kisheria kwani sheria ya vyombo vya habari (2016) inamtaka mlalamikaji kumshitaki Mwandishi, mhariri, mchapaji na msambazaji. Kwa mantiki hiyo DG wa TISS angetakiwa kusimama kortini. Ili kuokoa jahazi Musiba "alinunuliwa" mitambo mingine Mpya kutoka Ujerumani na kwa "huruma" mwana TISS Membe aliridhia. Nayo itanadiwa baada ya siku 14 kutamatika pamoja na nyumba na mashamba yake ya kijijini nakadhalika.

My take: Vijana tujifunze kitu katika sakata hili la Musiba na Membe kwamba tuwe na akiba ya maneno. Lakini pia akili ya kupewa changanya na zako. Waliokuwa wakimpa akili karibia wote wamemkimbia tena ndio wamekuwa jirani na Membe. Amtegemeae mwanadamu mwisho huwa kama hivi. Musiba kwishney!
kumbe Musiba ni tajiri hivi......alipe tu dadeki zake
 
Msamaha kwa huyu hapana,hapana, labda atuombe watanzania wengi tulioumizwa na unyama aliokuwa anatamba nao kwa uchochezi dhidi ya watz,tena kuna wakati alitamani wanaompinga mwendazake wauawe.
 
Kama alitegemea kutoboa kupitia hiyo njia Naona atakwama tu huyo musiba hana kitu.

Kufulia uzeeni kubaya sana kunamfanya mtu afanye mambo ya kumshushia hadhi kabisa.

Sasa kweli waziri wa mambo ya nje mstaafu ni mtu wa kungangania kuuza mali za Musiba??

Anajiabisha kuliko hata vile anavyodai kuaibishwa na musiba.
Hayo hayatowasaidia.
Kinachotakiwa anzisheni harambee, chawa mwenzenu anaadhirika huko.
 
Kama alitegemea kutoboa kupitia hiyo njia Naona atakwama tu huyo musiba hana kitu.

Kufulia uzeeni kubaya sana kunamfanya mtu afanye mambo ya kumshushia hadhi kabisa.

Sasa kweli waziri wa mambo ya nje mstaafu ni mtu wa kungangania kuuza mali za Musiba??

Anajiabisha kuliko hata vile anavyodai kuaibishwa na musiba.
Acha kuropoka kama mwendawazimu wewe huyo musiba aliyekuwa mpayukaji anamiliki mali zote hizo itakuwa mtu aliyekuwa wazir kwa miaka 10 tena chini ya JK? yani wewe unaamini membe anaweza kufilisika ? Unajua kwa mwaka anapata shiling ngapi kwenye korosho tu? Unaandika ujinga mtu mzima Huna aibu?
 
Membe membe usiwakatalie watumishi wa mungu kitachokupata hiyo ni kwa faida yako hunijui wala sikujui mimi nakuona tu kwenye tv
 
Nyumbani kwao Musiba ni kati ya moja ya vijiji hivi vilivyoko wilayani Bunda, mkoa wa Mara: Kijiji cha Igundu, Mwiruruma, Isanju au Mugara ndani ya kata ya Iramba.

Nimevitaja ili niisaide Yono Auction kukamata na kupiga mnada mali chache za Musiba zilizoko huko kijijini (kama zipo), hata kama ni hekari 2 za mihogo.
 
Alimwambia niguse ninuke....uone. sasa naamini Musiba ameelewa somo la niguse ninuke.

Unapoona umekosa omba radhi mapema badala ya kushupaza shingo matokeo ndio hayo. Kwa namna alivyofanya Musiba naunga mkono familia ya Membe
Musiba hakuwa na kosa maana alichokuwa anakisema walikitenda ila kwa kuwa ndio wenye nchi hawataki kudhalilishwa hadharani kwamba walikengeuka. Akiendelea kulipiza kisasi juu ya Musiba Mungu naye atalipiza kisasi kwa kuwa baya halilipwi kwa ubaya ili umfundishe aliyekunda ubaya ajifunze kuwa na kiasi.
1. Musiba alimtenda vibaya mlalamikaji
2. Musiba aliwatendea wema Watanzania wengi kwa kuweka wazi uovu wa viongozi wa kisiasi wanapopewa dhamana ya kuwatumikia wanajinufaisha wenyewe
 
Membe membe usiwakatalie watumishi wa mungu kitachokupata hiyo ni kwa faida yako hunijui wala sikujui mimi nakuona tu kwenye tv
Watumishi wale wako pamoja na Musiba?
Mbona Musiba alipokosea hwakumuonya?
Mbona hawakukemea Mwenndo wake wakati wa Kesi kabla kuisha?

Ushauri wangu.
Bw.Membe wacha HUKUMU kufuata mkondo wake ,Afilisiwe fedhuli yule li wengine wajifunze kwa kupitia yeye na itakuwa Faida kubwa sana Kwa taifa na Dunia kwa Ujumla.
Utamsamehe baada ya kutekelezwa hukumu ukitaka.

Shetani alipomkosea Mungu Hakuomba msamaha hadi dakika ya Mwisho Mungu anamuuliza Kwanini hukutii Amri?
Unajua alivyojibu? Alisema ''Mimi ni Mtukufu na Bora zaidi kuliko Adamu kwa kuwa yeye kaumbwa kwa Udongo na Mimi nimeumbwa kwa Moto''
Mungu akamlaani.

bab yetu Adam alipoulizwa kwa nini umepinga amri yangu? Unajua alivyojibu?
''Alisema '' Bwana wetu Mimi na Mke wangu tumekosea na kuzidhulumu nafsi zetu kwa kuvunja Amri yako, basi tusamehe, kwani usipotusamehe tukuwa wenye kuangamia''

Mungu akasema ''Nimewasamehe'',
''lakini sasa Haiwafalii tena nyinyi kuishi humu Peponi, bal Mutashuka Duniani ,huko Mutaishi kwa taabu na Mutakufa, na Kisha Mutafufuliwa siku ya Kiama ili kupimwa matendo yenu, atakayefaulu atarejea Humu peponi na atakaye feli ataingia Jahannam''

NB

Pamoja na kusamehewa kwake Adamu lakini Adhabu ya Dhambi haikuondoka, nayo ni kushuka duniani na kuishi kwa jasho lake na kufa na halafu kuhesabiwa matendo yake.

Mwacheni Musiba afaidi malipo ya matendo yake.
 
Watumishi wale wako pamoja na Musiba?
Mbona Musiba alipokosea hwakumuonya?
Mbona hawakukemea Mwenndo wake wakati wa Kesi kabla kuisha?

Ushauri wangu.
Bw.Membe wacha HUKUMU kufuata mkondo wake ,Afilisiwe fedhuli yule li wengine wajifunze kwa kupitia yeye na itakuwa Faida kubwa sana Kwa taifa na Dunia kwa Ujumla.
Utamsamehe baada ya kutekelezwa hukumu ukitaka.

Shetani alipomkosea Mungu Hakuomba msamaha hadi dakika ya Mwisho Mungu anamuuliza Kwanini hukutii Amri?
Unajua alivyojibu? Alisema ''Mimi ni Mtukufu na Bora zaidi kuliko Adamu kwa kuwa yeye kaumbwa kwa Udongo na Mimi nimeumbwa kwa Moto''
Mungu akamlaani.

bab yetu Adam alipoulizwa kwa nini umepinga amri yangu? Unajua alivyojibu?
''Alisema '' Bwana wetu Mimi na Mke wangu tumekosea na kuzidhulumu nafsi zetu kwa kuvunja Amri yako, basi tusamehe, kwani usipotusamehe tukuwa wenye kuangamia'' Mungu akasema ''Nimewasamehe'',
''lakini sasa Haiwafalii tena nyinyi kuishi humu Peponi, bal Mutashuka Duniani ,huko Mutaishi kwa taabu na Mutakufa, na Kisha Mutafufuliwa siku ya Kiama ili kupimwa matendo yenu, atakayefaulu atarejea Humu peponi na atakaye feli ataingia Jahannam''

Mwacheni Musiba afidfi malipo ya matendo yake.
Musiba hakuwa na kosa ila huu ni utawala wa visasi ila ukiendekeza visasi huwa haviishi maana na yeye siku akipata upenyo na nafasi atakulipizia kisasi kama Mungu hata aingilia kuamaua ugomvi
 
Ki

Kinyongo mmekiona leo kuliko waliokuaa wanateka watu?
Musiba alikuwa anasema ukweli ila hakujua aliokuwa anawasema ni waharifu waliobobea kimataifa na kwa kuwa utawala uliokuwa unachukia uharifu kwa wananchi haupo ndio maana wanamwonea Musiba kama 'Scapegoat'. Kwanini chanzo cha taarifa hakijafanywa chochote?
Ukilipiza kisasi na wewe utalipiziwa kisasi ila ukijishusha heshima itapanda. Kwa sasa Membe heshima imeshuka sana hawezi kuaminika kwa chochote kama kiongozi maana hasamehi
 
Mahakama kujihusisha kuamua kesi za madai zenye mlengo wa kisiasa kunaenda kuua demokrasia, uhuru wa kutoa habari na maoni na kunaenda kuziba watu midomo kuibua kashfa mbalimbali za uhujumu nchini kwa kuhofia kuamuriwa na mahakama kulipa fidia za bilioni 9!!!
 
Back
Top Bottom